Mkutano Mkuu
Kuwakubali Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo na Maafisa Wakuu
Mkutano mkuu wa Aprili 2024


Kuwakubali Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo na Maafisa Wakuu

Akina kaka na akina dada, sasa itakuwa ni heshima kwangu kuwawasilisha kwenu Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo na Maafisa Wakuu wa Kanisa kwa ajili ya kura yenu ya kuwakubali.

Tafadhali onesha kuwaunga mkono kwako katika njia ya kawaida. Kama kuna wale waliopinga mapendekezo yoyote, tunaomba kwamba muwasiliane na rais wenu wa kigingi.

Inapendekezwa kwamba tumkubali Russell Marion Nelson kama nabii, mwonaji na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho; Dallin Harris Oaks kama Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza; na Henry Bennion Eyring kama Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza.

Wale wanaounga mkono, waoneshe.

Wale wanaopinga, kama wapo, wanaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tumkubali Dallin H. Oaks kama Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili na Jeffrey R. Holland kama Kaimu Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.

Wale wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: Jeffrey R. Holland, Dieter F. Uchtdorf, David A. Bednar, Quentin L. Cook, D. Todd Christofferson, Neil L. Andersen, Ronald A. Rasband, Gary E. Stevenson, Dale G. Renlund, Gerrit W. Gong, Ulisses Soares na Patrick Kearon.

Wale wanaounga mkono, tafadhali onyesheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonyesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali washauri katika Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji na wafunuzi.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Kinyume, kama kuna yeyote, kwa ishara hiyo hiyo.

Viongozi Wakuu wenye Mamlaka wafuatao watapumzishwa kutoka kwenye majukumu yao na kupatiwa hadhi ya heshima, kuanzia tarehe 1 Agosti, 2024: Wazee Ian S. Ardern, Shayne M. Bowen, Paul V. Johnson, S. Gifford Nielsen, Brent H. Nielson, Adrián Ochoa, Gary B. Sabin na Evan A. Schmutz.

Wale ambao wangependa kuonyesha shukrani kwa ndugu hawa na kwa wake zao kwa miaka mingi ya kujitolea katika utumishi Kanisani kote wanaweza kufanya hivyo kwa kuinua mkono juu.

Pia tunampumzisha Mzee Carlos A. Godoy kutumikia kama mshiriki wa Urais wa Sabini, kuanzia Agosti 1, 2024.

Wale wanaopenda kuonyesha shukrani kwa Mzee Godoy kwa huduma yake ya kujitolea, tafadhali onyesheni.

Tunatambua kwa shukrani Sabini wa Maeneo ambao watamaliza huduma yao na ambao majina yao yanaweza kupatikana katika tovuti ya Kanisa.

Wale wanaopenda kuungana pamoja nasi katika kuonyesha shukrani kwa ndugu hawa kwa huduma yao isiyo ya ubinafsi wanaweza kuonyesha.

Tunaupumzisha Urais Mkuu wa Shule ya Jumapili ifikapo Agosti 1, 2024, kama ifuatavyo: Mark L. Pace kama Rais, Milton Camargo kama Mshauri wa Kwanza na Jan E. Newman kama Mshauri wa Pili.

Wale wote wanaopenda kuungana nasi katika kutoa shukrani kwa akina kaka hawa kwa huduma yao ya kujitolea, tafadhali waoneshe.

Imependekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama washiriki wa Urais wa Sabini, kutoka sasa: Mzee Marcus B. Nash, ambaye alianza huduma yake Januari 2024, na Wazee Michael T. Ringwood, Arnulfo Valenzuela na Edward Dube, ambao wataanza huduma yao kuanzia Agosti 1, 2024.

Wale wanaounga mkono, waoneshe.

Yeyote anayepinga anaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali Sabini Viongozi Wakuu wenye Mamlaka wafuatao: David L. Buckner, Gregorio E. Casillas, Aroldo B. Cavalcante, I. Raymond Egbo, D. Martin Goury, Karl D. Hirst, Christopher H. Kim, Sandino Roman, Steven D. Shumway, Michael B. Strong na Sergio R. Vargas.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Wale wanaopinga, kwa ishara hiyo hiyo.

Tunawapeni taarifa kwamba Sabini wa Maeneo wapya 64 walikubaliwa wakati wa mikutano ya mkutano mkuu wa uongozi iliyofanyika Alhamisi, Aprili 4, na baadaye kutangazwa kwenye tovuti ya Kanisa. Tunawaalikeni muwakubali ndugu hawa katika majukumu yao mapya.

Wale wanaounga mkono, tafadhali dhihirisheni.

Yeyote anayepinga kwa ishara hiyo hiyo.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama Urais Mkuu mpya wa Shule ya Jumapili, utakaoanza kazi Agosti 1, 2024: Paul V. Johnson kama Rais, Chad H Webb kama Mshauri wa Kwanza na Gabriel W. Reid kama Mshauri wa Pili.

Wale wanaounga mkono, waoneshe.

Yeyote anayepinga anaweza kuonesha vivyo hivyo.

Tunawajulisha kwamba Kaka Reid kwa sasa anatumikia kama rais wa Misheni ya Australia Sydney na kwa hivyo hayupo Jijini Salt Lake kwa ajili ya mkutano mkuu.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali Viongozi wengine Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo na Maafisa wakuu kama ilivyo sasa.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onesheni kwa kuinua mkono.

Wale wanaopinga, ikiwa kuna yeyote.

Tunawashukuru, akina kaka na akina dada kwa imani na sala zenu endelevu kwa niaba ya viongozi wa Kanisa.

Mabadiliko kwa Sabini wa Eneo

Sabini wa Eneo wafuatao waliidhinishwa wakati wa kikao cha uongozi kilichofanyika kama sehemu ya mkutano mkuu:

Daniel A. Abeo, Mauricio A. Araújo, Randy T. Austin, Michel D. Avegnon, Philip J. Barton, Bradley S. Bateman, Eber Antônio Beck, Eric D. Bednar, Jared Black, Bryan G. Borela, Jaime A. Bravo, Juan G. Cardenas, Sancho N. Chukwu, Mark J Cluff, Danilo F. Costales, Daniel A. Cruzado, Gregorio Davalos, Julio N. Del Sero, Ryan E. Dobbs, Stephen W. Dyer, Brik V. Eyre, Denny Fa‘alogo, Timothy L. Farnes, Martín P. Fernández, Luis A. Ferrizo, Ángel J. Gómez, Georgie E. Guidi, Shinjiro Hara, Daniel L. Harris, Todd D. Haynie, Thomas Hengst, John R. Higgins, Niels O. Jensen, Fritzner A. Joseph, Kyoni Kasongo, John S. K. Kauwe III, Dan Kawashima, J. Joseph Kiehl, Carl F. Krauss, Yew Mun Kwan, Woo Cheol Lee, Wai Hung Mak, David R. Marriott, Ignatius Maziofa, Derek B. Miller, Albert Mutariswa, Marvin I. Palomo, Kyung Yeol Park, Domingo J. Perez, Oscar A. Perez, Raul Perez, Gayle L. Pollock, Pierre Portes, Marco A. Quezada, Stephen T. Rockwood, Guillermo Rojas, Kgomotso T. Sehloho, Sandro Alex Silva, Juswan Tandiman, Asuquo E. Udobong, Dwayne J. Van Heerden, Shih Ning (Steve) Yang, Juan F. Zorrilla, Leopoldo Zuñiga.

Sabini wa Maeneo wafuatao watapumzishwa mnamo au kabla ya Agosti 1, 2024:

Solomon I. Aliche, Guillermo A. Alvarez, Daren R. Barney, Julius F. Barrientos, James H. Bekker, David L. Buckner, Glenn Burgess, Marcos Cabral, Gregorio E. Casillas, Dunstan G. B. T. Chadambuka, Alan C. K. Cheung, Paul N. Clayton, Michael Cziesla, Hiroyuki Domon, Mernard P. Donato, I. Raymond Egbo, Zachary F. Evans, Sapele Fa‘alogo Jr., Saulo G. Franco, David Frischknecht, John J. Gallego, Efraín R. García, Robert Gordon, Mark A. Gottfredson, D. Martin Goury, Michael J. Hess, Bhanu K. Hiranandani, Richard S. Hutchins, Tito Ibañez, Eustache Ilunga, Akinori Ito, Anthony M. Kaku, Christopher H. Kim, H. Moroni Klein, Stephen Chee Kong Lai, V. Daniel Lattaro, Thabo Lebethoa, Tarmo Lepp, Itzcoatl Lozano, Kevin Lythgoe, Clement M. Matswagothata, Edgar P. Montes, Luiz C. D. Queiroz, Ifano Rasolondraibe, Eduardo D. Resek, Tomás G. Román, Ramon E. Sarmiento, Steven D. Shumway, Luis Spina, Jared W. Stone, Michael B. Strong, Djarot Subiantoro, Carlos G. Süffert, Voi R. Taeoalii, Karim Del Valle, Sergio R. Vargas, Helmut Wondra.