Mkutano Mkuu
Hamu Halisi ya Nafsi
Mkutano mkuu wa Aprili 2024


Hamu Halisi ya Nafsi

Mungu husikia kila sala tunayotoa na hujibu kila moja kulingana na njia ambayo Yeye ameibainisha kwa ajili ya ukamilifu wetu.

Akina kaka na akina dada, nimejifunza somo linaloumiza tangu niliposimama katika mimbari hii mnamo Oktoba ya 2022. Somo hilo ni: ikiwa hutoi hotuba inayokubalika, unaweza kuzuiwa kwenye mikutano kadhaa ijayo. Mnaweza kuona nimepangiwa mapema katika kikao cha kwanza cha mkutano. Kile msichokiona ni kwamba niko kwenye mlango wenye kuning’inia ulio na kombeo lililo karibu kufyatuka. Kama hotuba hii haitaenda vizuri, sitawaona kwa mikutano kadhaa ijayo.

Katika roho huyo wa muziki mzuri pamoja na kwaya hii, nimepata kujifunza baadhi ya masomo hivi karibuni ambayo, kwa msaada wa Bwana, ninatamani kushiriki nanyi leo. Hiyo itafanya hotuba hii iwe binafsi sana.

Uzoefu binafsi na wa kuumiza zaidi kati ya uzoefu huu wa karibuni umekuwa kufariki kwa mke wangu kipenzi, Pat. Yeye alikuwa mwanamke mkuu niliyewahi kumfahamu—mke na mama mkamilifu, mtakatifu, mwenye kipawa cha kujieleza na uwezo mkubwa wa kiroho. Aliwahi kutoa hotuba yenye kichwa cha habari “Kutimiza Kipimo cha Uumbaji Wako.” Kwangu mimi inaonekana kwamba alitimiza kipimo cha uumbaji wake kwa ukamilifu zaidi kuliko ambavyo yeyote angeweza kutarajia. Alikuwa binti aliyejitoa kikamilifu kwa Mungu, mwanamke mwenye mfano wa Kristo. Nilikuwa mwanaume mwenye bahati sana kuishi miaka 60 ya maisha yangu pamoja naye. Ikiwa nitastahili, kuunganishwa kwetu kunamaanisha ninaweza kuishi naye milele.

Uzoefu mwingine ulianza saa 48 baada ya mazishi ya mke wangu. Wakati huo, nilikimbizwa hospitalini kutokana na hali mbaya ya kiafya. Kisha nilitumia wiki nne za mwanzo kati ya wiki sita nikiwa ndani na nje ya kitengo cha wagonjwa mahututi na katika hali ya kuwa na fahamu na kukosa fahamu.

Kimsingi uzoefu wangu wote ndani ya hospitali wakati wa kipindi hicho haupo kwenye kumbukumbu yangu. Kile ambacho hakikupotea ni kumbukumbu yangu ya safari nje ya hospitali, nje ya kile kilichoonekana kama ukingo wa umilele. Siwezi kuzungumza yote hapa kuhusu uzoefu huo, lakini ninaweza kusema sehemu ya kile nilichopokea kilikuwa himizo la kurejea kwenye huduma yangu kwa uharaka zaidi, wakfu zaidi, fokasi zaidi kwa Mwokozi na kwa imani zaidi katika neno Lake.

Nilihisi kwamba nilikuwa nikipokea toleo langu binafsi la ufunuo uliotolewa kwa Kumi na Wawili karibia miaka 200 iliyopita.

“Nawe utalishuhudia jina langu … [na] utalipeleka neno langu hata miisho ya dunia. …

“… Asubuhi hadi asubuhi; na siku hadi siku na acha sauti yako ya kuonya isikike; na usiku uingiapo usiache wakazi wa dunia walale, kwa sababu ya maneno yako. …

“Inuka[,] … chukua msalaba wako, [na] ukanifuate.”1

Akina dada na kaka zangu wapendwa, tangu uzoefu huo, nimejaribu kuuchukua msalaba wangu kwa dhati, na kuwa na azimio la kutafuta wapi ninaweza kupaza sauti ya kitume ya upendo na onyo asubuhi, mchana na usiku.

Hiyo inaniongoza kwenye ukweli wa tatu ambao ulikuja katika miezi hiyo ya kupoteza, ugonjwa na huzuni. Ulikuwa ushahidi uliofanywa upya wa shukrani zisizo na mwisho kwa sala za Kanisa hili—sala zenu—ambazo mimi ndiye mnufaika wake. Nitakuwa na shukrani milele kwa sala za maelfu ya watu ambao, kama yule mjane aliyeomba sana,2 mara kwa mara nilitafuta mbingu kuingilia kati kwa niaba yangu. Nilipokea baraka za ukuhani, na kuwaona wenzangu wa darasa la upili wakifunga kwa ajili yangu, kama zilivyofanya kata tofauti tofauti kote Kanisani. Na jina langu lazima lilikuwa kwenye orodha ya sala ya kila hekalu katika Kanisa.

Katika shukrani zangu kuu kwa yote haya, ninaungana na G. K. Chesterton, ambaye aliwahi kusema “kwamba shukrani ni hali ya juu ya fikra, na … shukrani ni furaha iliyoongezwa kwa hisia za kustaajabu.”3 Kwa “furaha yangu mwenyewe iliyoongezwa kwa hisia za kustaajabu,” ninawashukuruni nyote na kumshukuru Baba yangu wa Mbinguni, ambaye alisikia sala zenu na kuyabariki maisha yangu.

Akina kaka na akina dada, ninashuhudia kwamba Mungu husikia kila sala tunayotoa na anajibu kila moja kulingana na njia ambayo Yeye ameibainisha kwa ajili ya ukamilifu wetu. Ninatambua kwamba takribani wakati uleule ambapo wengi walikuwa wakisali kwa ajili ya urejesho wa afya yangu, idadi sawa na hiyo—ikiwa ni pamoja na mimi—tulikuwa tukisali kwa ajili ya urejesho wa afya ya mke wangu. Ninashuhudia kwamba sala zote zilisikika na zilijibiwa na Baba wa Mbinguni mwenye huruma ya kiungu, hata kama sala kwa ajili ya Pat hazikujibiwa jinsi nilivyoomba. Ni kwa sababu zijulikanazo kwa Mungu pekee kwa nini sala hujibiwa kinyume na tunavyotumaini—lakini ninawaahidi zinasikika, na zinajibiwa kulingana na upendo Wake usioshindwa na ratiba Yake ya ulimwengu.

Ikiwa “tutaomba bila kizuizi,”4 hakuna ukomo kwenye lini, wapi au kuhusu nini tukiombee. Kulingana na mafunuo, tunapaswa “kuomba daima.”5 Sisi tunapaswa kuomba, Amuleki alisema, kwa ajili ya “wale ambao wako karibu nanyi,”6 tukiamini kwamba “Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana.”7 Sala zetu zinapaswa kuwa za sauti pale tunapokuwa na faragha ya kuzitoa kwa sauti.8 Ikiwa hilo haliwezekani, zinapaswa kutolewa kama maneno ya kimyakimya katika mioyo yetu.9 Tunaimba kwamba sala ni “hamu halisi ya nafsi,”10 daima hutolewa, kulingana na Mwokozi Mwenyewe, na Mungu Baba wa Milele katika jina la Mwanawe Mzaliwa wa Pekee.11

Marafiki zangu wapendwa, sala zetu ni saa yetu tamu,11“hamu yetu ya dhati,”14 mfumo rahisi, safi wa kuabudu kwetu.13 Tunapaswa kusali binafsi, katika familia zetu, na katika mikusanyiko ya ukubwa wowote.15 Tunapaswa kutumia sala kama ngao dhidi ya majaribu,16 na ikiwa kuna wakati hatuhisi kusali, tunaweza kuwa na uhakika kwamba kusita hakutoki kwa Mungu, ambaye anatamani kuwasiliana na watoto Wake wakati wowote na muda wote. Hakika, baadhi ya juhudi za kutuzuia kusali huja moja kwa moja kutoka kwa adui.17 Wakati hatujui jinsi ya kusali au tusali kwa ajili ya kitu gani hasa, tunapaswa kuanza, na kuendelea, hadi Roho Mtakatifu anapotuongoza kwenye sala tunayopaswa kuitoa.18 Mbinu hii inaweza kuwa ndiyo tuliyonayo ya kuomba wakati tunaposali kwa ajili ya adui zetu na wale wanaotuudhi.19

Hatimaye, tunaweza kutazama mfano wa Mwokozi, ambaye alisali mara nyingi sana. Lakini imekuwa ya kustaajabisha kwangu kwamba Yesu alihisi hitaji la kusali. Je, Yeye hakuwa mkamilifu? Yeye alihitaji kusali kuhusu nini? Nimekuja kutambua kwamba Yeye pia, pamoja nasi, anataka “kuona uso wa [Baba], kuamini neno lake, na kutumainia neema yake.” Muda baada ya muda, Yeye alijitenga na jamii ili kuwa peke yake kabla ya kuifikia mbingu kwa sala Zake.21 Nyakati zingine, Yeye alisali kwenye uwepo wa watu wengine wachache. Kisha angeitafuta mbingu kwa niaba ya umati ambao ungejaza upande wa mlima. Nyakati zingine sala iliyapa utukufu mavazi Yake.22 Nyakati zingine iliupa utukufu uso Wake.23 Nyakati zingine alisali akiwa amesimama, nyakati zingine alipiga magoti, na angalau mara moja alianguka kifulifuli katika sala.24

Luka anaelezea dhiki ya Yesu Kristo katika Bustani ya Gethsemane kama ilimhitaji “azidi sana kuomba.”25 Ni kwa jinsi gani mtu ambaye alikuwa mkamilifu azidi sana kuomba? Tunakisia kwamba sala Zake zote zilikuwa za dhati, lakini katika kutimiza dhabihu Yake ya kulipia dhambi na kupitia maumivu ambayo yaliubeba ulimwengu wote, alihisi kusali hata kwa kusihi zaidi, na uzito wa dhabihu Yake ukileta damu kwenye kila kinyweleo.

Katika muktadha huo wa ushindi wa Kristo juu ya mauti na zawadi Yake ya hivi karibuni kwangu ya wiki zaidi au miezi zaidi katika maisha haya, ninatoa ushahidi wa dhati wa uhalisia wa maisha ya milele na hitaji kwetu la kutokuwa na mzaha katika kuyawekea mpango.

Ninatoa ushahidi kwamba wakati Kristo atakapokuja, Yeye anahitaji kututambua sisi—siyo kama waumini waliorodheshwa tu kwenye kumbukumbu ya ubatizo iliyopauka bali kama wenye dhamira kamili, waaminifu kwa dhati, wanafunzi wenye kushika agano. Hili ni jambo la dharura kwetu sote, tusije tukasikia kukataliwa kwenye kuangamiza: “Sikuwajua ninyi kamwe,”26 au, kama Joseph Smith alivyotafsiri kirai hicho, “[Wewe] haukunijua kamwe.”27

Kwa bahati nzuri, tuna msaada kwa ajili ya kazi hii—msaada mwingi mno. Tunahitaji kuamini katika malaika na miujiza na ahadi za ukuhani mtakatifu. Tunahitaji kuamini katika kipawa cha Roho Mtakatifu, ushawishi wa familia nzuri na marafiki, na nguvu ya upendo halisi wa Kristo. Tunahitaji kuamini katika ufunuo na manabii, waonaji na wafunuzi na Rais Russell M. Nelson. Tunahitaji kuamini kwamba kwa sala na kusihi na uadilifu binafsi, tunaweza hakika kuukwea “Mlima Sayuni, … mji wa Mungu aliye hai, mahali pa mbinguni, patakatifu pa patakatifu.”28

Akina Kaka na Dada, tunapotubu dhambi zetu na kuja kwa ushupavu kwenye kile “kiti cha neema,”29 tukiacha mbele Yake thawabu zetu za maombi ya moyoni, tutapokea rehema na kupata msamaha kwenye mikono ya faraja ya Baba yetu wa Milele, na Mwanawe mtiifu na msafi kikamilifu. Basi, kama Ayubu na waaminifu wote waliotakaswa, tutautazama ulimwengu “unaostaajabisha sana,” kueleweka. Katika jina la Yesu Kristo, amina.