Mkutano Mkuu
Kuwa na Umoja pamoja na Kristo
Mkutano mkuu wa Aprili 2024


Kuwa Wamoja na Kristo

Tunaunganishwa kwa upendo wetu juu ya na imani katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake. Umuhimu wa kuhisi kuwa sehemu ya ni kuwa wamoja na Kristo.

Nimehisi kwa kina kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo tangu nilipokuwa mdogo, lakini uhalisia wa Upatanisho wa Mwokozi ulinijia wakati nikiwa na miaka 25. Nilikuwa ndio nimetoka kuhitimu Shule ya Sheria ya Stanford na nilikuwa nikisoma kwa ajili ya mtihani wa California bar. Mama yangu aliniita na kusema kwamba babu yangu Crozier Kimball, ambaye alikuwa akiishi Utah, alikuwa akikaribia kuaga dunia. Alisema kama ningetaka kumuona, nilitakiwa kuja nyumbani. Babu yangu alikuwa na miaka 86 na mwenye kuumwa sana. Nilikuwa na maongezi ya kupendeza. Alifurahi sana kuniona na alishiriki ushuhuda wake pamoja nami.

Wakati Crozier alipokuwa na umri wa miaka mitatu, David Patten Kimball, baba yake, alifariki akiwa na miaka 44.1 Crozier alitumaini kwamba baba yake pamoja na Heber C. Kimball, babu yake, wangefurahishwa na maisha yake na kuhisi kwamba amekuwa mkweli kwa kizazi chake.

Ushauri wa msingi wa babu yangu kwangu ulikuwa ni kuepuka aina yoyote ya hisia za ukuu au fursa kwa sababu ya mababu hawa waaminifu. Aliniambia kwamba fokasi yangu ingepaswa kuwa kwa Mwokozi na Upatanisho Wake. Alisema kwamba sisi sote tu watoto wa Baba mpendwa wa Mbinguni. Bila kujali mababu zetu wa duniani ni nani, kila mmoja wetu atatoa ripoti kwa Mwokozi ya jinsi gani alizishika amri.

Babu alimrejelea Mwokozi kama “Mlinzi wa Lango,” rejeleo kutoka 2 Nefi 9:41. Aliniambia alitumaini kwamba alikuwa ametubu vya kutosha kustahili rehema ya Mwokozi.2

Niliguswa sana. Nilijua alikuwa mtu wa haki. Yeye alikuwa patriaki na alihudumu misheni kadhaa. Alinifundisha kwamba hakuna yeyote ambaye angerudi kwa Mungu kwa matendo pekee bila ufadhili wa Upatanisho wa Mwokozi. Ninaweza kukumbuka mpaka leo upendo na shukrani Babu aliokuwa nao kwa sababu ya Mwokozi na Upatanisho Wake.

Mnamo mwaka 2019 wakati nilipopangiwa jukumu huko Yerusalemu,3 nilitembelea chumba cha juu ambacho inawezekana kilikuwa karibu na sehemu ambapo Mwokozi aliwaosha miguu Mitume Wake kabla ya kusulubiwa. Niliguswa kiroho na kufikiria jinsi Alivyowaamuru mitume Wake kupendana.

Nilikumbuka sala ya dhati ya Mwokozi kwa ajili yetu. Sala hii ilitolewa saa za mwisho wa maisha Yake duniani kama ilivyoandikwa katika injili ya Yohana.

Sala hii ilielekezwa kwa wafuasi wa Kristo, ikijumuisha sisi sote.4 Katika sala ya Mwokozi kwa Baba Yake, alisihi “kwamba wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako, ili hao nao wawe na umoja ndani yetu.” Mwokozi kisha aliendelea, “Na utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.”5 Umoja ndicho kitu ambacho Kristo alikiomba kabla ya kusalitiwa Kwake na Kusulubiwa. Umoja na Kristo na Baba yetu wa Mbinguni unaweza kupatikana kupitia Upatanisho wa Mwokozi.

Rehema ya Bwana yenye kuokoa haitegemei kwenye uzao, elimu, hadhi ya kiuchumi au utaifa. Inategemea kwenye kuwa wamoja na Kristo na amri Zake.

Nabii Joseph Smith na Oliver Cowdery walipokea ufunuo juu ya muundo na utawala wa Kanisa na uongozi wake mnamo mwaka 1830, muda mfupi baada ya Kanisa kuanzishwa. Kile ambacho sasa ni sehemu ya 20 ilisomwa na nabii Joseph Smith kwenye mkutao wa kwanza wa Kanisa na ulikuwa ufunuo wa kwanza kukubaliwa na wote.6

Kilichomo kwenye ufunuo huu kweli ni cha kushangaza. Hutufundisha kuhusu umuhimu na kazi ya Upatanisho wa Mwokozi na jinsi ya kufikia nguvu na baraka Zake kupitia neema Yake ya kulipia dhambi. Nabii Joseph alikuwa na umri wa miaka 24 na tayari alikuwa amekwisha kupokea mafunuo mengi na kumaliza tafsiri ya Kitabu cha Mormoni kupitia kipawa na nguvu za Mungu. Wote Joseph na Oliver wanatambulika kama Mitume waliotawazwa, hivyo kuwa na mamlaka ya kuliongoza Kanisa.

Mstari wa 17 hadi 36 una ufupisho wa mafundisho muhimu ya Kanisa ikijumuisha uhalisia wa Mungu, Uumbaji wa mwanadamu, Anguko, na mpango wa Baba wa Mbinguni wa wokovu kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo. Mstari wa 37 unabeba vigezo muhimu kwa ajili ya ubatizo kwenye Kanisa la Bwana. Mstari wa 75 hadi 79 unaonyesha sala za sakramenti ambazo tunazitumia kila Sabato.

Mafundisho, kanuni, sakramenti na kaida ambazo Bwana alizianzisha kupitia Joseph Smith, Nabii wa Urejesho, kwa kweli ni za msingi.7

Vigezo vya ubatizo, ingawa ni vya maana sana, vina urahisi wa kipekee. Kimsingi vinajumuisha unyenyekevu mbele za Mungu, moyo uliovunjika na roho iliyopondeka,8 kutubu dhambi zote, kujichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo, kuvumilia hadi mwisho, na kuonyesha kwa matendo kwamba tumepokea Roho wa Kristo9

Ni muhimu kwamba vigezo vyote kwa ajili ya ubatizo ni vya kiroho. Hakuna mafanikio ya kiuchumi au kijamii yanayohitajika. Fukara na tajiri wote wanahitajika kuwa na vigezo sawa vya kiroho.

Hakuna utaifa, jinsia au utamaduni vinavyohitajika. Kitabu cha Mormoni kinaweka wazi kwamba wote wanaaalikwa kupokea wema wa Bwana, “weusi kwa weupe, wafungwa na walio huru, wake kwa waume; … wote ni sawa kwa Mungu.”10 “Lakini wanadamu wote wana fursa sawa, na hakuna yeyote anayekatazwa.”11

Kwa “mfanano” wetu mbele za Mungu, haileti maana kusisitiza tofauti zetu. Baadhi kimakosa wanatuhamasisha “kuwafikiria watu kuwa wa utofauti sana na sisi na kila mmoja kuliko jinsi ukweli ulivyo. [Baadhi] huchukua tofauti ndogo, ingawa halisi na kuzikuza kuwa kubwa.”12

Kwa nyongeza, baadhi kimakosa wamedhania kwamba kwa sababu watu wote wamealikwa kupokea wema Wake na uzima wa milele hakuna vigezo kimaadili vinavyohitajika.13

Hata hivyo, maandiko yanashuhudia kwamba watu wote wanao wajibika wanahitajika kutubu dhambi na kushika amri Zake.14 Bwana ameweka wazi kwamba wote wana haki ya kujiamulia na “wako huru kuchagua uhuru na uzima wa milele, kupitia yule Mpatanishi mkuu wa wanadamu wote, … na kutii amri zake kuu; na kuwa waaminifu kwa maneno yake, na kuchagua uzima wa milele.”15 Ili kupokea baraka za Upatanisho wa Mwokozi, lazima kwa uthabiti tutumie haki yetu ya kujiamulia kumchagua Kristo na kutii amri Zake.

Wakati wa maisha yangu, tafsiri ya “haki ya kujiamulia” na “uhuru wa kutenda” vimetafakariwa na kujadiliwa. Kumekuwepo na kutaendelea kuwepo mawazo mengi ya wasomi kuhusu mada hizi.

Kwenye moja ya jalada la chapisho maarufu la hivi karibuni la wanachuo wa zamani, profesa maarufu wa baiolojia alitilia mkazo, “Hakuna nafasi kwa ajili ya hiari.”16 Haishangazi, profesa alinukuliwa kwenye makala hiyo akisema, “Hakuna Mungu, … na hakuna uhuru wa kujiamulia, … na huu ni ulimwengu mpana, usio na zuri wala baya na mtupu.”17 Sikuweza kukubaliana naye zaidi.

Fundisho la msingi la imani yetu ni kwamba tunayo haki ya kujiamulia,18 hiyo ikijumuisha uhuru wa kutenda kwa hiari.19 Haki ya kujiamulia ni uwezo wa kuamua na kutenda. Hilo ni muhimu kwa mpango wa wokovu. Bila maadili ya haki ya kujiamulia, tusingeweza kujifunza, kupiga hatua na kuchagua kuwa na umoja pamoja na Kristo. Kwa sababu ya maadili ya haki ya kujiamulia, “tuko huru kuchagua uhuru na uzima wa milele.”20 Kwenye baraza kabla ya maisha haya huko mbinguni, mpango wa Baba ulijumuisha haki ya kujiamulia kama sehemu muhimu. Lusiferi aliasi na “kutafuta kuharibu haki ya kujiamulia ya mwanadamu.”21 Vivyo hivyo, fursa ya kuwa na mwili wa nyama na mifupa iliondolewa kwa Shetani na wale walio mfuata.

Roho wengine walitumia haki yao ya kujiamulia katika kufuata mpango wa Baba wa Mbinguni. Roho waliobarikiwa kupitia kuzaliwa kwenye maisha haya ya duniani wanaendelea kuwa na haki ya kujiamulia. Tuko huru kuchagua na kutenda, lakini hatuna uwezo wa kuchagua matokeo. “Chaguzi nzuri na za haki hutuongoza kwenye furaha, amani na uzima wa milele, wakati chaguzi za dhambi na uovu hatimaye hutuongoza kwenye maumivu ya moyo na huzuni.”22 Kama Alma alivyosema, “Uovu kamwe haujawa furaha.”23

Kwenye ulimwengu huu wenye ushindani mkubwa, kuna juhudi endelevu za kufaulu. Kujitahidi kuwa bora kadiri tunavyoweza kuwa ni lengo la haki na lenye thamani. Huendana na mafundisho ya Bwana. Jitihada za kufifisha au kuwashusha thamani wengine au kutengeneza mipaka kwenye mafanikio yao ni kinyume na mafundisho ya Bwana. Hatuwezi kulaumu hali au wengine kwa uchaguzi wa kutenda kinyume na amri za Mungu.

Katika ulimwengu wa leo, ni rahisi kufokasi kwenye vitu vya muda na mafanikio ya kikazi. Baadhi hupoteza uwezo wa kuona kanuni za milele na chaguzi ambazo zina matokeo muhimu ya milele. Tungekuwa wenye hekima kufuata ushauri wa Rais Russell M. Nelson wa “kufikiria selestia.”24

Chaguzi muhimu zaidi zinaweza kufanywa karibia na kila mtu bila kujali vipaji, uwezo, fursa au hali za kiuchumi. Msisitizo wa kuweka chaguzi za familia kwanza ni muhimu. Hili ni wazi kupitia maandiko. Fikiria kuhusu hadithi iliyoko katika Nefi wa kwanza wakati Lehi “alipoelekea nyikani. Na aliacha nyumba yake, na nchi yake ya urithi, na dhahabu yake, na fedha yake, na vitu vyake vya thamani, na hakubeba cho chote, isipokuwa familia yake.”25

Tunapokabiliana na changamoto za maisha, matukio mengi hutokea ambayo kwayo tuna uwezo kidogo juu yake au hatuna udhibiti. Matatizo ya kiafya na ajali bila shaka yanaweza kuwa kwenye kundi hilo. Janga la ulimwengu la hivi karibuni la UVIKO-19 kwa kiasi kikubwa lilileta madhara kwa watu ambao walifanya kila kitu kwa usahihi. Kwa sehemu kubwa ya chaguzi muhimu, tuna uwezo juu yake. Nikirejelea siku zangu za umisionari, Mzee Marion D. Hanks, rais wetu wa misioni alitufanya sote kukariri sehemu ya shairi lililoandikwa na Ella Wheeler Wilcox:

Hakuna nafasi, hakuna kudra, hakuna hitimisho

Linaweza kuzunguka au kuzuia au kushikilia

Ari thabiti ya dhati ya nafsi.26

Kuhusu mambo yahusuyo kanuni, tabia, dini na maisha ya haki, tuna uwezo juu yake. Imani yetu na kumwabudu kwetu Mungu Baba na Mwanae, Yesu Kristo, ni uchaguzi ambao tunaufanya.27

Tafadhali eleweni kwamba sihamasishi kutotilia maanani elimu au kazi. Ninachokisema ni kwamba wakati juhudi kuhusu elimu na kazi vinatiliwa mkazo zaidi kuliko familia au kuwa na umoja pamoja na Kristo, juhudi hizo ambazo hazikukusudiwa zinaweza kuwa na madhara hasi makubwa.

Fundisho la wazi na rahisi lililoko kwenye Mafundisho na Maagano 20 ni la kugusa na kutia msukumo kwani hukuza na kuweka wazi mambo matakatifu ya kiroho. Hufundisha kwamba wokovu huja wakati Kristo anapowahesabia haki na kutakasa nafsi za wenye kutubu kwa sababu ya neema ya Mwokozi.28 Huweka jukwaa kwa ajili ya umuhimu wa juu wa kazi ya Upatanisho Wake.

Tujitahidi kujumuisha wengine kwenye mduara wetu wa umoja. Ikiwa tutafuata ushauri wa Rais Nelson wa kukusanya Israeli iliyotawanyika, kote pande mbili za pazia, tunahitajika kuwajumuisha wengine kwenye mduara wetu wa umoja. Kama ambavyo Rais Nelson kwa uzuri alifundisha: “Katika kila bara na visiwa vya bahari watu waaminifu wanakusanywa katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Tofauti za kitamaduni, lugha, jinsia, rangi, asili na utaifa hufifia kuwa zisizo muhimu wakati waaminifu wakiingia kwenye njia ya agano na kuja kwa Mkombozi wetu mpendwa.”29

Tunaunganishwa kwa upendo wetu juu ya na imani katika Yesu Kristo na kama watoto wa Baba mpendwa wa Mbinguni. Umuhimu wa kuhisi kuwa sehemu ya ni kuwa wamoja na Kristo. Ibada za ubatizo na sakramenti zilizopo katika Mafundisho na Maagano 20, pamoja na maagano yetu ya hekaluni, hutuunganisha katika njia maalum na kuturuhusu kuwa na umoja katika kila njia muhimu ya umilele na kuishi kwa amani na utulivu.

Ninatoa ushuhuda wangu wa hakika na kweli kwamba Yesu Kristo anaishi, na kwa sababu ya Upatanisho Wake, tunaweza kuwa na umoja pamoja na Kristo. Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. David, katika umri wa miaka 17, alisaidia kubeba baadhi ya Watakatifu kuvuka mto ulioganda wa Sweetwater wakati walipokuwa wamekwama kwenye nyanda za juu za Wyoming (ona Saints: The Story of the Church of Jesus Christ in the Latter Days, volume 2, No Unhallowed Hand, 1846–1893 [2020], 237).

  2. Ona Moroni 7:27–28.

  3. Chifu Rabbi wa Norway, Rabbi Michael Melchior pamoja nami tulikuwa wazungumzaji wakuu kwenye mazungumzo ya wanazuoni wa Kiyahudi–Watakatifu wa Siku za Mwisho mnamo Juni 5,2019 kwenye tawi la BYU hukoYerusalemu.

  4. Ona Yohana 17:20.

  5. Yohana 17:21–22.

  6. Ona “The Conference Minutes and Record Book of Christ’s Church of Latter Day Saints, 1838–1839, 1844” (commonly known as the Far West Record), June 9, 1830, Church History Library, Salt Lake City; Steven C. Harper, Making Sense of the Doctrine and Covenants (2008), 75.

  7. Mafundisho na Maagano 20 ni ufunuo wa kwanza kuchapishwa katika gazeti la Kanisa na ulitumika na wamisionari kwa ajili ya vyote kwa mafundisho na mwongozo wa ibada ya ubatizo na sakramenti. (ona Harper, Making Sense of the Doctrine and Covenants, 75).

  8. Ona 2 Nefi 2:7.

  9. Ona Mafundisho na Maagano 20:37.

  10. 2 Nefi 26:33.

  11. 2 Nefi 26:28.

  12. Peter Wood, Diversity: The Invention of a Concept (2003), 20.

  13. Nehori alichukua nafasi yake (ona Alma 1:4).

  14. Ona Mafundisho na Maagano 29:49–50.

  15. 2 Nefi 2:27–28.

  16. Stanford (publication of the Stanford Alumni Association), Dec. 2023, cover.

  17. Katika Sam Scott, “As If You Had a Choice,” Stanford, Dec. 2023, 44. Makala hii inamtambua profesa kama Robert Sapolsky, profesa wa bailojia wa Stanford, mtaalamu wa neva na mpasuaji wa neva na mwandishi ambaye ameuza sana vitabu vya sayansi. Makala inabeba mawazo ya upingaji, ikijumuisha yale ya Alfred Mele, profesa wa filosofia wa chuo cha Florida State, ambaye aliongoza mradi mkubwa wa John Templeton kuhusu uhuru wa kutenda. Alieleza “Wanasayansi bila shaka hawajathibitisha kwamba uhuru wa kutenda—hata wa uhuru wa kimawazo—kwamba ni udanganyifu”(in Scott, “As If You Had a Choice,” 46).

  18. Ona D. Todd Christofferson, “Moral Agency” (Brigham Young University devotional, Jan. 31, 2006), speeches.byu.edu.

  19. Ona Mafundisho na Maagano 58:27.

  20. 2 Nefi 2:27.

  21. Musa 4:3.

  22. True to the Faith: A Gospel Reference (2004).

  23. Alma 41:10.

  24. Ona Russell M. Nelson, “Fikiria Selestia!,” Liahona, Nov. 2023, 117–20.

  25. 1 Nefi 2:4.

  26. Poetical works of Ella Wheeler Wilcox (1917), 129.

  27. Mara zote nimevutiwa na nukuu iliyotolewa na Mzee Neal A. Maxwell ambayo inasema hivi waziwazi: “kama hujachagua ufalme wa Mungu kwanza, hatimaye hakutakuwa na utofauti wa kile ambacho ulichagua badala yake”(attributed to William Law, an 18th-century English clergyman; quoted in Neal A. Maxwell, “Response to a Call,” Ensign, Mei 1974, 112).

  28. Ona Mafundisho na Maagano 8:29–31. Thiolojia ya Calvini husisitiza kwenye kuhesabiwa haki na kusafishwa kwa nafsi zilizoanguka kupitia neema ya Kristo. Hufundisha kwamba wakati Mungu akiwa ameamua kudra ya nafsi kwa ajili ya ukombozi, hakuna kitu kinachoweza kubadili matokeo. Mafundisho na Maagano 20 huonyesha utengano wa wazi na theolojia ya Calvini. Inasomeka, “Lakini upo uwezekano kwamba mwanadamu akaweza kuanguka kutoka katika hali ya neema, na kujitenga kutoka kwa Mungu aliye hai” (ona Mafundisho na Maagano 20:32–34; Harper, Making Sense of the Doctrine and Covenants, 74).

  29. Russell M. Nelson, “Kujenga Madraja,” Liahona, Des. 2018, 51.