Mkutano Mkuu
“Tulieni na Jueni Kuwa Mimi ni Mungu”
Mkutano mkuu wa Aprili 2024


“Tulieni na Jueni Kuwa Mimi ni Mungu”

Tunaweza kutulia na kujua kwamba Mungu ni Baba yetu wa Mbinguni, sisi ni watoto Wake na Yesu Kristo ni Mwokozi wetu.

Hivi karibuni wakati wa ziara ya wazi kwa kila mtu na shughuli ya siku ya vyombo vya habari kwa ufunguzi wa nyumba mpya ya Bwana, niliongoza kundi la waandishi wa habari kwenye matembezi kwenye jengo hili takatifu. Nilielezea lengo la mahekalu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho na kujibu maswali yao mengi mazuri.

Kabla ya kuingia kwenye chumba cha selestia, nilifafanua kwamba chumba hiki maalumu kwenye nyumba ya Bwana kwa ishara kinawakilisha amani na uzuri wa nyumba ya mbinguni ambayo tunaweza kurudi huko baada ya maisha haya. Nikielekeza kwa wageni kwamba hatutapaswa kuzungumza wakati tukiwa kwenye chumba cha selestia, lakini ningekuwa na furaha kujibu maswali yo yote baada ya kuwa tumefika kwenye sehemu inayofuata ya matembezi yetu.

Baada ya kutoka chumba cha selestia na wakati tumekusanyika kwenye sehemu iliyofuata, niliwauliza wageni wetu kama walikuwa na maoni yo yote ambayo wangependa kuyashiriki. Mmoja wa waandihsi wa habari alisema kwa hisia, “sijawahi kupitia kitu cho chote kama hicho maisha yangu yote. Sikujua kama ukimya wa namna ile unapatikana ulimwenguni; kiufupi sikuamini kwamba utulivu ule ungewezekana.”

Nilishangazwa na vyote uaminifu wake na uwazi wa kauli ya mtu huyu. Na uzoefu wa mwandishi wa habari ulidondoa moja ya mambo muhimu kuhusu utulivu—kushinda na kuondoa dhoruba za mazingira yetu ya nje.

Wakati baadaye nikitafakari maoni ya mwandishi wa habari na kufikiria juu ya mwenendo wa kuchosha wa maisha yetu ya kisasa—uwepo wa shughuli nyingi, kelele, ukiukaji, vipotosha mawazo na njia zisizo halali ambavyo mara nyingi huonekana kuvuta umakini wetu—andiko lilikuja mawazoni mwangu: Tulieni na jueni kuwa Mimi ni Mungu.”1

Ninasali kwamba Roho Mtakatifu atuangazie kila mmoja wetu wakati tukifikiria utakatifu na thamani ya juu ya utulivu katika maisha yetu—utulivu wa ndani wa kiroho wa nafsi ambao hutuwezesha kujua na kukumbuka kwamba Mungu ni Baba yetu wa Mbinguni, sisi ni watoto Wake, na Yesu Kristo ni Mwokozi wetu. Baraka hii kuu inapatikana kwa waumini wote wa Kanisa ambao wanajitahidi kwa uaminifu kuwa “watu wa maagano wa Bwana.”2

Tulieni

Mnamo 1833, Watakatifu huko Missouri walikuwa kwenye mateso makali. Makundi ya wahuni yalikuwa yamewafukuza kutoka majumbani mwao katika Wilaya ya Jackson, na baadhi ya waumini wa Kanisa walijaribu kuanzisha makazi yao katika Wilaya za karibu. Lakini mateso yaliendelea, na vitisho vya kifo vilikuwa vingi. Katika hali hizi zenye changamoto, Bwana alifunua maelekezo yafuatayo kwa Nabii Joseph Smith huko Kirtland, Ohio:

“Kwa hiyo, mioyo yenu na ifarijike juu ya Sayuni; kwa kuwa wenye mwili wote wako mikononi mwangu; tulieni na jueni kuwa Mimi ni Mungu.”3

Naamini maonyo ya Bwana ya “tulieni” yana maana zaidi kuliko tu kutozungumza au kutojongea. Pegine kusudi Lake ni kwa sisi kumkumbuka na kumtegemea Yeye na nguvu Zake “kwa nyakati zote na katika vitu vyote na katika mahali popote ambapo [tunaweza] kuwa.”4 Hivyo, “kutulia” kunaweza kuwa njia ya kutukumbusha kufokasi kwa Mwokozi kwa uthabiti kama chanzo kikuu cha utulivu wa kiroho wa nafsi ambao hutuimarisha ili tufanye na tushinde mambo magumu.

Jenga juu ya Mwamba

Imani ya kweli daima hufokasi katika Bwana Yesu Kristo—katika Yeye kama Mwana Mtakatifu na wa Pekee wa Baba wa Milele na katika Yeye na misheni ya ukombozi ambayo Yeye aliitimiza.

“Kwani amejibu mwisho wa sheria, na anawataka wale wote ambao wana imani ndani yake; na wale ambao wana imani ndani yake watajishikilia kwa kila kitu kizuri; kwa hivyo anatetea teto la watoto wa watu.”5

Yesu Kristo ni Mkombozi wetu,6 Mpatanishi wetu,7 na Mwombezi wetu8 kwa Baba wa Milele na mwamba ambao juu yake tunapaswa kujenga msingi wa kiroho wa maisha yetu.

Helamani alifafanua, “Kumbukeni, kumbukeni kwamba ni juu ya mwamba wa Mkombozi wetu, ambaye ni Kristo, Mwana wa Mungu, kwamba lazima mjenge msingi wenu; kwamba ibilisi atakapotuma mbele pepo zake kali, ndiyo, mishale yake katika kimbunga, wakati mvua yake ya mawe na dhoruba kali itapiga juu yenu, haitakuwa na uwezo juu yenu kuwavuta chini kwenye shimo la taabu na msiba usioisha, kwa sababu ya mwamba ambao juu yake ninyi mmejengwa, ambao ni msingi imara, msingi ambao watu wote wakijenga hawataanguka.”9

Kufananishwa kwa Kristo na “mwamba” ambao juu yake tunapaswa kujenga msingi wa maisha yetu ni ya kuvutia. Tafadhali zingatia kwamba kwenye mstari huu Mwokozi siyo msingi. Isipokuwa, tunaaswa kujenga msingi wetu wenyewe wa kiroho juu Yake.10

Msingi ni sehemu ya jengo ambayo huliunganisha na ardhi. Msingi imara hutoa ulinzi dhidi ya majanga ya asili na kani zingine nyingi za kuharibu. Msingi mzuri pia hutoa msawazo wa uzito wa jengo kwenye eneo kubwa ili kuepusha kuzidiwa kwa udongo na hutoa sehemu iliyo tambarare kwa ajili ya ujenzi.

Picha
Nyumba yenye msingi imara.

Muunganiko imara na wa kuaminika kati ya ardhi na msingi ni muhimu kama jengo linatakiwa kubakia imara na thabiti kwa muda mrefu. Na kwa aina fulani ya ujenzi, pini za nanga na nondo vinaweza kutumika ili kuunganisha msingi wa jengo kwenye “mwamba” mgumu, mwamba ulioko chini ya uso wa vitu vilivyoko juu ya ardhi kama udongo na kokoto.

Picha
Nyumba yenye nanga juu ya mwamba

Katika njia sawa na hiyo, msingi wa maisha yetu lazima uunganishwe kwenye mwamba wa Kristo kama tunataka kubakia imara na thabiti. Maagano na ibada takatifu za injili ya urejesho ya Mwokozi inaweza kulinganishwa na pini za nanga na nondo vitumikavyo kuunganisha jengo kwenye mwamba. Kila mara kwa uaminifu tunapopokea, kurejelea, kukumbuka na kufanya upya maagano matakatifu, nanga zetu za kiroho zinaimarishwa hata kuwa imara zaidi na thabiti kwenye “mwamba” wa Yesu Kristo.

“Kwa hivyo, ye yote aaminiye katika Mungu angeweza kwa hakika kutumaini ulimwengu bora, ndiyo, hata mahali katika mkono wa kulia wa Mungu, tumaini ambalo huja kutokana na imani, hutengeneza nanga kwa nafsi za watu, ambayo ingewafanya kuwa imara na thabiti, wakizidi sana kutenda kazi njema, wakiongozwa kumtukuza Mungu.”11

Kwa kuongezeka na kukua “baada ya muda,”12 “wema [unayapamba] mawazo yetu bila kukoma,” kujiamini kwetu “[kunakuwa imara] katika uwepo wa Mungu,” na “Roho Mtakatifu ni mwenzi [wetu] daima.”13 Tunakuwa imara zaidi, wenye kina, thabiti na tusiotikisika.14 Wakati msingi wa maisha yetu unapojengwa juu ya Mwokozi, tunabarikiwa kuwa “watulivu”—kuwa na uhakika kiroho kwamba Mungu ni Baba yetu wa Mbinguni, sisi ni watoto Wake na Yesu Kristo ni Mwokozi wetu.

Nyakati Takatifu, Mahali Patakatifu na Nyumbani

Bwana hutoa vyote, nyakati takatifu na mahali patakatifu ili kutusaidia tupate uzoefu na tujifunze utulivu huu wa ndani wa nafsi zetu.

Kwa mfano, Siku ya Sabato ni siku ya Mungu, wakati mtakatifu ulitengwa ili kumkumbuka na kumuabudu Baba katika jina la Mwana Wake, kushiriki katika ibada za ukuhani na kupokea na kufanya upya maagano matakatifu. Kila wiki tunamwabudu Bwana katika kujifunza kwetu nyumbani na kama “wenyeji pamoja na watakatifu”15 wakati wa sakramenti na mikutano mingine. Katika siku Yake takatifu, mawazo yetu, matendo, na mwenendo ni ishara kwa Mungu na kielelezo cha upendo wetu Kwake.16 Kila Jumapili, kama tutataka, tunaweza kutulia na kujua kwamba Mungu ni Baba yetu wa Mbinguni, sisi ni watoto Wake na Yesu Kristo ni Mwokozi wetu.

Cha muhimu kwenye kuabudu kwetu siku ya Sabato ni “kwenda kwenye nyumba ya sala na kutoa sakramenti [zetu] katika siku takatifu ya [Bwana].”17 “Nyumba ya sala” ambamo ndani yake tunakusanyika siku ya Sabato ni nyumba zetu takatifu za mikutano na sehemu zingine zilizoidhinishwa—sehemu takatifu za utulivu, kuabudu na kujifunza. Kila nyumba ya ibada na mahali ambapo pamechaguliwa huwekwa wakfu kwa mamlaka ya ukuhani kama sehemu ambapo Roho wa Bwana anaweza kukaa na ambapo watoto wa Mungu wanaweza kuja “kwenye ufahamu wa Mkombozi wao”18 Kama tutataka, tunaweza kuwa “watulivu” kwenye sehemu zetu takatifu za kuabudu na kujua hata kwa uhakika zaidi kwamba Mungu ni Baba yetu wa Mbinguni, sisi ni watoto Wake na Yesu Kristo ni Mwokozi wetu.

Hekalu ni sehemu nyingine takatifu iliyotengwa mahususi kwa ajili ya kumwabudu na kumtumikia Mungu na kujifunza kweli za milele. Tunatafakari, kutenda na kuvaa kwa utofauti kwenye nyumba ya Bwana tofauti na sehemu yo yote ambayo huwa tupo. Ndani ya nyumba Yake takatifu, kama tutataka, tutanaweza kuwa watulivu na kujua kwamba Mungu ni Baba yetu wa Mbinguni, sisi ni watoto Wake na Yesu Kristo ni Mwokozi wetu.

Madhumuni ya msingi ya wakati mtakatifu na sehemu takatifu ni sawa: kurudia kufokasi umakini wetu juu ya Baba wa mbinguni na mpango Wake, Bwana Yesu Kristo na Upatanisho Wake, nguvu ya kuinua ya Roho Mtakatifu na ahadi zinazohusiana na ibada takatifu na maagano ya injili iliyorejeshwa ya Mwokozi.

Leo ninarudia kanuni ambayo awali nimeisisitiza. Nyumba zetu zapaswa kuwa muunganiko wa vyote wakati mtakatifu na mahali patakatifu ambapo watu na familia wanaweza “kutulia” na kujua kwamba Mungu ni Baba yetu wa Mbinguni, sisi ni watoto Wake, na Yesu Kristo ni Mwokozi wetu. Kuondoka nyumbani kwetu kwenda kuabudu siku ya Sabato na katika nyumba ya Bwana bila shaka ni muhimu. Lakini ni pale tu tunaporudi kwenye nyumba zetu tukiwa na mtazamo wa kiroho na nguvu vilivyopatikana kwenye sehemu na shughuli hizo takatifu ndipo tunaweza kuimarisha fokasi yetu kwenye lengo kuu la maisha ya duniani na kushinda majaribu ambayo yamezagaa sana kwenye ulimwengu wetu ulioanguka.

Uzoefu wetu endelevu wa siku ya Sabato, hekaluni, na nyumbani unatakiwa kutuimarisha kwa nguvu ya Roho Mtakatifu pamoja na muunganiko endelevu wa kimaagano na imara kwa Baba na Mwana, pamoja na “mng’aro mkamilifu wa tumaini”19 katika ahadi za milele za Mungu.

Wakati nyumbani na Kanisani vinapokuja pamoja katika Kristo,20 tunaweza kutatizwa kila kona, lakini hatutatatizwa mawazoni na mioyoni mwetu. Tunaweza kukanganywa kwa hali zetu na changamoto, lakini hatutakuwa wa kukatishwa tamaa. Tunaweza kuteswa, lakini pia tutatambua kwamba hatuko peke yetu.21 Tunaweza kupokea nguvu za kiroho za kuwa imara na kubakia imara, thabiti na wakweli.

Ahadi na Ushuhuda

Ninatoa ahadi kwamba wakati tunapojenga msingi wa maisha yetu kwenye “mwamba” wa Yesu Kristo, tunaweza kubarikiwa kwa Roho Mtakatifu kwa kupokea utulivu binafsi na wa kiroho wa nafsi ambao hutuwezesha tujue na tukumbuke kwamba Mungu ni Baba yetu wa Mbinguni, sisi ni watoto Wake, Yesu Kristo ni Mwokozi wetu na tunaweza kubarikiwa kufanya na kushinda mambo magumu.

Kwa shangwe ninashuhudia kwamba Mungu ni Baba yetu wa Mbinguni, sisi ni watoto Wake na Yesu Kristo ni Mkombozi wetu na “mwamba” wa wokovu wetu. Ninashuhudia hivyo katika jina takatifu la Bwana Yesu Kristo, amina.