Misaada ya Kujifunza
Kumbukumbu la Torati


Kumbukumbu la Torati

Kitabu cha tano katika Agano la Kale.

Kumbukumbu la torati inazo hotuba tatu za mwisho za Musa, ambazo alizitoa katika nyanda za Moabu muda mfupi kabla ya kuhamishwa kwake. Hotuba ya kwanza (mlango wa 1–4) ni utangulizi. Hotuba ya pili (mlango wa 5–26) ina sehemu mbili: (1) mlango wa 5–11—ni zile Amri Kumi na maelekezo ya utekelezaji wake; na (2) mlango 12–26—ni mfumo wa sheria, ambazo zinaunda kiini cha kitabu chote. Hotuba ya tatu (mlango wa 27–30) zina marudio ya moyo wa dhati ya agano kati ya Israeli na Mungu na tangazo la baraka ambazo zinafuata utiifu na laana ambazo hufuatia kutotii. Mlango wa 31–34 inaelezea kutolewa kwa sheria kwa Walawi, wimbo wa Musa na baraka ya mwisho, na kuondoka kwa Musa.