Misaada ya Kujifunza
Mafundisho na Maagano


Mafundisho na Maagano

Mkusanyiko wa mafunuo matakatifu na maazimio ya kuongozwa na Mungu katika siku za mwisho. Bwana aliyatoa haya kwa Joseph Smith na wengine kadhaa waliomrithi kwa ajili ya kuanzisha na kusimamia ufalme wa Mungu hapa duniani katika siku hizi za mwisho. Mafundisho na Maagano ni moja ya vitabu vitakatifu vya maandiko katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho pamoja na Biblia, Kitabu cha Mormoni, na Lulu ya Thamani Kuu. Mafundisho na Maagano ni cha kipekee, hata hivyo, kwa sababu hiki siyo tafsiri ya maandiko ya zamani; Bwana ametoa mafunuo haya kwa manabii Wake wateule katika siku hizi za sasa ili kuurejesha ufalme Wake. Katika mafunuo mtu husikia sauti laini lakini iliyo imara ya Bwana Yesu Kristo (M&M 18:35–36).

Historia ya Joseph Smith inasema kwamba Mafundisho na Maagano ni msingi wa Kanisa katika siku za mwisho na ni kwa manufaa ya ulimwengu (M&M 70 kichwa cha habari). Mafunuo yaliyomo yanaianzisha kazi ya kuitengeneza njia kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Bwana, katika utimilifu wa maneno yote yaliyonenwa na manabii tangu ulimwengu kuanza.