Misaada ya Kujifunza
Hosea


Hosea

Nabii wa Agano la Kale aliyekuwa akitoa unabii katika ufalme wa kaskazini wa Israeli katika kipindi cha mwisho cha utawala wa Yeroboamu Ⅱ. Aliishi katika wakati wa kuporomoko kwa taifa na maangamizi, kama matokeo ya dhambi ya Israeli.

Kitabu cha Hosea

Mada kuu ya kitabu hiki ni upendo wa Mungu kwa watu Wake. Kuwatia adabu Kwake kote kulifanyika katika upendo, na urejesho wa Israeli utatokana na upendo Wake (Hos. 2:19; 14:4). Kinyume chake, Hosea anaonyesha udanganyifu na uzinzi wa Israeli. Lakini Mungu bado anaweza kuangalia hatima ya ukombozi wa Israeli (Hos. 11:12–14:9).