Uasherati Ona pia Kupenda anasa, Matamanio ya anasa; Usafi wa Kimwili; Uzinzi Tendo la ngono lisilo la kisheria kati ya watu wawili wasiooana. Katika maandiko pia mara chache hutumika kama ishara ya ukengeufu. Jiepusheni na uasherati, Mdo. 15:20. Mwili si kwa ajili ya uasherati, bali ni kwa ajili ya Mungu, 1 Kor. 6:13–18. Kuepuka uasherati, acha kila mtu awe na mke wake mwenyewe, 1 Kor. 7:2–3. Haya ni mapenzi ya Mungu, kwamba yawapasa mjiepushe na uasherati, 1 The. 4:3. Yakobo waliwaonya watu wa Nefi dhidi ya uasherati, Yak. (KM) 3:12. Ninyi mnakomaa, kwa sababu ya mauaji yenu na uasherati, kwa kuangamizwa, Hel. 8:26. Washerati lazima watubu ili waweze kujiunga na Kanisa, M&M 42:74–78.