Misaada ya Kujifunza
Wagalatia, Waraka kwa


Wagalatia, Waraka kwa

Kitabu katika Agano Jipya. Mwanzoni ilikuwa ni barua ambayo Mtume Paulo aliwaandikia Watakatifu waliokuwa wakiishi Galatia. Mada ya barua hii ni kwamba uhuru wa kweli unaweza kupatikana tu katika kuishi kulingana na injili ya Yesu Kristo. Kama Watakatifu wangeyachukua na kuishi kulingana na mafundisho ya Wakristo wa Kiyahudi ambao walisisitiza juu ya kuziangalia torati ya Musa, wangelijizuia au kuharibu uhuru walioupata katika Kristo. Katika waraka Paulo alielezea nafasi yake yeye mwenyewe kama Mtume, alielezea mafundisho ya haki kwa njia ya imani, na akathibitisha thamani ya dini ya kiroho.

Katika mlango wa 1 na wa 2, Paulo alihuzunishwa na habari aliyoipokea juu ya ukengeufu miongoni mwa Wagalatia na akaelezea kwa ufasaha nafasi yake miongoni mwa Mitume. Mlango wa 3 na wa 4 inajadili mafundisho ya imani na matendo. Mlango wa 5 na wa 6 ina mahubiri juu ya matokeo yanayoweza kutendeka ya mafundisho ya imani.