Misaada ya Kujifunza
Filemoni, Waraka kwa


Filemoni, Waraka kwa

Kitabu katika Agano Jipya, kilichochukuliwa kutoka katika barua iliyoandikwa na Paulo. Barua ya Paulo kwa Filemoni ni barua binafsi juu ya Onesimo, mtumwa aliyemwibia Bwana wake, Filemoni, na akatorokea Roma. Paulo alimrudisha tena kwa Bwana wake huko Kolosai akiwa pamoja na Tikiko, aliyebeba barua ya Paulo kwa Wakolosai. Paulo aliomba kwamba Onesmo asamehewe na kupokelewa tena kama Mkristo mwenzao. Paulo aliandika barua hii wakati akiwa gerezani Roma kwa mara ya kwanza.