Hali ya Kufa, enye Kufa Ona pia Anguko la Adamu na Hawa; Mauti ya Kimwili; Mwili; Ulimwengu Muda tangu kuzaliwa hadi kifo cha kimwili. Hii wakati mwingine huitwa hali ya pili. Siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika, Mwa. 2:16–17 (Musa 3:16–17). Katika mauti roho itarudi kwa Mungu na mwili katika mavumbi ya dunia, Mh. 12:7 (Mwa. 3:19; Musa 4:25). Msiache dhambi itawale katika miili yenu yenye kufa, Rum. 6:12. Mwili huu wenye kufa lazima uvae kutokufa, 1 Kor. 15:53 (Eno. 1:27; Mos. 16:10; Morm. 6:21). Hali ya mwanadamu ikawa hali ya majaribio, 2 Ne. 2:21 (Alma 12:24; 42:10). Adamu alianguka ili wanadamu wawepo, 2 Ne. 2:25. Je, ninyi mnatazamia na kuona mwili huu wenye kufa ukiinuliwa katika kutokufa, Alma 5:15. Maisha haya ndiyo wakati wa kujitayarisha kukutana na Mungu, Alma 34:32. Msiogope mauti, kwani shangwe yenu si kamilifu katika ulimwengu huu, M&M 101:36. Wale wanaoitunza hali yao ya pili watakuwa na utukufu, Ibr. 3:26.