Misaada ya Kujifunza
Hezekia


Hezekia

Mfalme mwenye haki wa taifa la Yuda katika Agano la Kale. Alitawala kwa miaka ishirini na tisa, wakati ambao Isaya alikuwa nabii katika Yuda (2 Fal. 18–20; 2 Nya. 29–32; Isa. 36–39). Isaya alimsaidia katika kulirekebisha kanisa na taifa. Alikomesha ibada za masanamu na kurejesha ibada za hekalu. Uhai wa Hezekia uliongezwa kwa miaka kumi na mitano kwa njia ya sala na imani (2 Fal. 20:1–7). Sehemu ya kwanza ya utawala wake ilikuwa yenye kustawi, lakini uasi wake dhidi ya mfalme wa Ashuru (2 Fal. 18:7) ilileta kuvamiwa na Waashuru mara mbili: wa kwanza unaelezwa katika Isaya 10:24–32, na wa pili katika 2 Wafalme 18:13–19:7. Katika uvamizi wa pili, Yerusalemu iliokolewa na malaika wa Bwana (2 Fal. 19:35).