Misaada ya Kujifunza
Musa


Musa

Nabii wa Agano la Kale aliyewaongoza Waisraeli kutoka utumwa wa Misri na akawapa vifungu vya sheria za kidini, kijamii na kilishe kama zilivyofunuliwa na Mungu.

Utumishi wa Musa unaendelea hata ngʼambo ya mipaka ya uhai wake mwenyewe katika mwili wenye kufa. Joseph Smith alifundisha kwamba, wakiwa pamoja na Eliya, alikuja katika Mlima wa Kugeuka Sura na kutunuku funguo za ukuhani juu ya Petro, Yakobo, na Yohana (Mt. 17:3–4; Mk. 9:4–9; Lk. 9:30; M&M 63:21).

Musa aliwatokea Joseph Smith na Oliver Cowdery hapo 3 Aprili 1836, katika hekalu la Kirtland, Ohio, na akawatunukia funguo za kukusanyika kwa Israeli (M&M 110:11).

Ufunuo wa siku za mwisho unazungumzia sana juu ya Musa. Ametajwa mara kwa mara katika Kitabu cha Mormoni, na kutoka katika Mafundisho na Maagano tunajifunza juu ya utumishi wake (M&M 84:20–26) na kwamba alipata ukuhani kutoka kwa baba mkwe wake Yethro (M&M 84:6).

Ufunuo wa siku za mwisho pia unathibitisha historia ya kibiblia ya utumishi wake miongoni mwa wana wa Israeli na unasisitiza ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa mwandishi wa vitabu vitano vinavyoanzisha Agano la Kale (1 Ne. 5:11; Musa 1:40–41).

Kitabu cha Musa

Ni Kitabu katika Lulu ya Thamani Kuu ambamo imo tafsiri ya Joseph Smith ya Maongozi ya Mungu ya milango saba ya kwanza ya kitabu cha Mwanzo.

Mlango wa 1 unaandikwa ono ambalo ndani yake Musa alimwona Mungu, ambaye alimfunulia mpango mzima wa wokovu. Mlango wa 2–5 ni maelezo ya Uumbaji na Anguko la mwanadamu. Mlango wa 6–7 ina ono juu ya Henoko na utumishi wake duniani. Mlango wa 8 unalo ono juu ya Nuhu na Gharika kuu.

Vitabu vitano vya Musa

Vitabu vitano vya kwanza vya Agano la Kale vinajulikana kama vitabu vya Musa. Mabamba ya shaba nyeupe ambayo Nefi aliyachukuwa kutoka kwa Labani yalikuwa na vitabu vya Musa (1 Ne. 5:11).