Misaada ya Kujifunza
Timotheo, Nyaraka Kwa


Timotheo, Nyaraka Kwa

Vitabu viwili katika Agano Jipya. Vyote mwanzoni vilikuwa ni barua ambazo Paulo alimwandikia Timotheo.

1 Timotheo

Paulo aliandika waraka wa kwanza baada ya kifungo chake cha kwanza gerezani. Alikuwa amemwacha Timotheo huko Efeso, akitarajia baadaye arudi (1 Tim. 3:14). Hata hivyo, Paulo alihisi kwamba angeliweza kucheleweshwa, hivyo alimwandikia Timotheo, huenda kutoka Makedonia (1 Tim. 1:3), ili kumpa ushauri na kumtia moyo katika kutekeleza kazi yake.

Mlango wa 1 una salamu za Paulo na pia mafundisho yake juu ya watu walioeneza mafundisho ya kipumbavu katika Kanisa. Mlango wa 2–3 anaandika mwongozo juu ya ibada ya hadharani na juu ya tabia na mwenendo wa wahudumu. Mlango wa 4–5 anaelezea juu ya ukengeufu wa siku za mwisho na ushauri kwa Timotheo juu ya jinsi ya kuhudumu kwa wale anaowaongoza. Mlango wa 6 anamsihi kuthibitisha uaminifu na kuepuka utajiri wa kilimwengu.

2 Timotheo

Paulo aliandika barua ya pili wakati wa kufungwa kwake mara ya pili, muda mfupi kabla ya kifo chake cha kishahidi. Ina maneno ya mwisho ya Mtume na inaonyesha ujasiri na uaminifu wa ajabu ambao kwa huo alikabiliana na mauti.

Mlango wa 1 una salamu za Paulo na amri kwa Timotheo. Mlango wa 2–3 inatoa maonyo na maelekezo mbalimbali, pamoja na kumtia moyo ili kukabili hatari zinazokuja. Mlango wa 4 ni ujumbe kwa marafiki wa Paulo, wenye ushauri juu ya jinsi ya kuwatendea wakengeufu.