2016
Alma Anabatiza Watu Wengi
April 2016


Hadithi za Kitabu cha Mormoni

Alma Anabatiza Watu Wengi

Kutoka Mosia 16–18.

Picha
Alma baptizes many people 1
Picha
Alma baptizes many people 2
Picha
Alma baptizes many people 3

Abinadi alikuwa nabii. Alifundisha watu kumwamini Yesu na kuacha kufanya matendo mabaya. Mfalme muovu aitwaye Nuhu alikasirishwa na Abinadi. Nuhu hakutaka kutubu.

Mtu mmoja aliyeitwa Alma alimwamini Abinadi. Alitoroka na kujificha mbali na mfalme mwenye hasira. Alisikitika kwa kufanya matendo mabaya, na alitubu, kama vile Abinadi alivyokuwa amefundisha.

Watu wengi walikuja kumsikiliza Alma akifundisha kuhusu Yesu Kristo. Alma alifundisha kuwa ikiwa wangetubu na kumfuata Yesu, wangeweza kubatizwa.

Watu walipiga makofi kwa shangwe. Waliahidi kuwafariji wengine. Waliahidi kumpenda Mungu na kuwaeleza watu wengine kumhusu Yeye. Walikuwa tayari kubatizwa.

Mmoja baada ya mwingine, Alma aliwabatiza. Walikuwa watu wenye furaha sana kuwa sehemu ya Kanisa la Yesu.

Tunapobatizwa, tunatoa ahadi sawa na zile ambazo Alma na watu wake walitoa. Na sisi tunakuwa sehemu ya Kanisa la Yesu pia!