2016
Mawazo kwa ajili ya Jioni ya Familia Nyumbani
April 2016


Mawazo kwa ajili ya Jioni ya Familia Nyumbani

Toleo hili lina makala na shughuli ambazo zinaweza kutumika kwa ajili ya jioni ya familia nyumbani. Ufuatao ni mfano mmoja.

Picha
family on a bench

“Hata Kama Unaona Haya,” ukurasa wa 60: Unaweza kuitumia jioni ya familia nyumbani kufundisha injili! Jadilianeni kama familia ni hofu ipi inayofanya uone vigumu kushiriki injili. Yawezekana mkasali kama familia ili Bwana akusaidie wewe kujisikia jasiri katika kushirikiana na wengine injili na kisha ombeni juu ya mtu wa kumwalika kwenye jioni ya familia. Fikiria kumwalika kila mwana familia kutoa ushuhuda wakati wa somo. Unaweza kuchagua kufundisha somo juu ya Urejesho au mpango wa wokovu. Fikirieni kuandika mliyoyafanya na hisia zenu katika shajara zenu.