2016
Amani Moyoni Mwangu
April 2016


Amani Moyoni Mwangu

Picha
peace in my heart

Nilipokuwa na miaka minane, nilimwona nabii, Rais David O. McKay (1873–1970). Alikuja kuweka wakfu jengo jipya la Kanisa huko Palmyra, New York, Marekani. Familia yangu ilienda kwenye ibada ya uwekaji wakfu huo. Watu wengine wengi walikuja pia. Sote tulisisimka kumuona nabii!

Nilikuwa mdogo sana, kwa hiyo ilikuwa vigumu kwangu kuona nikiwa nimezungukwa na watu wote hao. Lakini bado niliweza kuhisi upendo wa Rais McKay. Kwa dakika moja tu, niliona nywele zake nyeupe na uso wake mkarimu. Nilifikiria, “Hivi ndivyo nabii wa Mungu anavyoonekana.” Nilikuwa nimesoma kuhusu manabii katika maandiko, lakini huu ulikuwa wakati wangu wa kwanza kumwona nabii au Kiongozi yeyote Mkuu Mwenye Mamlaka kwa macho yangu. Nilitambua kwamba manabii ni watu halisi. Na wanatupenda! Nitakumbuka daima upendo na amani niliyojisikia siku ile.

Nilipokuwa na miaka 11, nilipata tukio jingine ambalo lilinisaidia kusikia amani moyoni mwangu. Mkutano wa kigingi ulikuwa unakaribia, na nilipata nafasi ya kuimba katika kwaya ya kigingi. Nilikuwa na furaha sana! Nilivaa shati zuri jeupe, na kujihisi mtu muhimu. Wimbo tulioimba ulikuwa na maneno kutoka Yohana 14:27, “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msiwe na wasiwasi moyoni mwenu, wala msifadhaike.”

Maneno hayo kweli yalinigusa moyo, na nimeyakumbuka tangu wakati huo. Nilipoimba maneno hayo, nilijua yalikuwa ya kweli. Nilihisi Roho Mtakatifu akiniambia kwamba kumfuata Yesu Kristo kunatusaidia kuona amani. Tangu wakati huo, kila mara ninapopata changamoto, maandiko haya huja akilini mwangu na kunipa amani. Ukweli niliojifunza nilipokuwa mdogo umebariki maisha yangu yote.