2016
Kujipa sharti la Kuacha
April 2016


Kujipa sharti la Kuacha

Mwandishi anaishi New York, Marekani.

Ujuzi wangu wa kucheza kinanda haukuwa ukiongezeka, hata baada ya mazoezi ya miaka mingi. Wazazi wangu walisema ningeweza kuacha kwa sharti moja tu: Nilihitaji kujifunza nyimbo 50 za injili.

Picha
playing piano

Niliingia nyumbani kwa fujo, macho yangu yakifurika machozi baada ya kushindwa somo lingine la kinanda. Ulikuwa ni mwaka wangu wa nne nikijifunza kucheza kinanda, na kwa shida sana nilikuwa nimeboresha kupiga kupita “Meremeta, Nyota Ndogo.” Mwalimu wangu alikuwa amejaribu kutafuta jambo zuri la kusema kuhusu kucheza kwangu kunakotisha, lakini nilijisikia tu vibaya zaidi. Wazazi wangu walikuwa wakilipia masomo yangu ya kinada ambayo sikutaka na nilikuwa nimekwishapoteza matumaini.

Nilitaka wazazi wangu waniruhusu niache. “Tafadhali,” niliwasihi. Nitafanya chochote. Nifanye nini?

Baada ya kufanya majadiliano baina yao, walisema, “Kama ukijifunza nyimbo 50, tutakukubalia uache.”

Nilianza kufanya mazoezi mara moja. Nilitaka vibaya sana kuacha kiasi kwamba nilikuwa tayari kutumia muda wa ziada kwenye kinanda. Wimbo wa kwanza, “Asante Ee Mungu kwa Nabii” (Kitabu cha Nyimbo, na. 19), ulinichukua karibu mwezi mmoja kuwa stadi. Bado nilikuwa na dhamira ya kuacha, kwa hiyo niliendelea kufanya mazoezi.

Kitu cha kupendeza kilifanyika: ilianza kuwa rahisi kuwa stadi katika nyimbo za injili. Nilijisikia mwenye furaha zaidi wiki mzima. Nilijipata nikivuma nyimbo za injili wakati wa mchana na nikiimba kwa sauti ya juu wakati wa mkutano wa sakramenti.

Hatimaye, niliacha kuhesabu ni nyimbo ngapi nilikuwa nimezijua. Kadiri nilivyokuwa nikiongeza ujuzi kwenye kinanda, niligundua kuwa nilikuwa na uwezo wa kujifunza wimbo mpya kikamilifu katika karibu muda wa chini ya dakika 30.

Wakati mwishowe nilipozijumlisha, nilikuwa nimejifunza zaidi ya nyimbo 50. Na hapakuwa na jinsi ambavyo ningeacha kucheza kinanda. Nilikuwa nimekuwa hodari katika uwezo wangu wa kucheza na nilikuwa nimeona nguvu za nyimbo za injili maishani mwangu.

Nyimbo za injili ni kama maandiko; zinaongea ukweli. Ninapocheza nyimbo za injili, ninajisikia kama kwamba ninajizamisha mwenyewe ndani ya maandiko. Kujifunza kucheza nyimbo za injili imekuwa kama kichocheo cha kujenga ushuhuda wangu na kujifunza ukweli. Ninajiona mwenyewe nikipitia maneno ya nyimbo tofauti tofauti ili kunisaidia siku mzima. Kucheza kinanda kumeimarisha ushuhuda wangu na kumenifungulia milango popote niendapo.