2016
Asante kwa huduma yako.
April 2016


Kuhudumu katika Kanisa

Asante kwa huduma yako

Wewe ni mfano wa wale wanawake ambao, tangu siku za Nauvoo, wametumikiana wao kwa wao kupitia ualimu wa kutembelea kwa upendo na kuinuana.

Picha
visiting teachers

Sijui jina lako, una umri gani, wala sijui cho chote juu yako. Ninachokijua tu ni kwamba wewe ni mwalimu wa kumtembelea Joann, na ninakushukuru kwa moyo wangu wote kwa huduma yako yenye kujali.

Ninajua kwamba kumtembelea dada asiye hudhuria kanisani kama Joann (jina halisi limebadilishwa), binti mkwe wangu, siyo rahisi, hususani pale anapokuwa si mkarimu. Ni na shaka hata kama alitaka umtembelee kwanza. Lakini Joann ameniambia kwamba wewe umekuwa rafiki wa kweli kwake, ukipita kumjulia hali na kumkubali yeye kama alivyo.

Katika miaka 19 tangu Joann aolewe na mwanangu, hii ni mara ya kwanza yeye kutamka kuwa anaye mwalimu mtembeleaji. Hivi karibuni ameniambia jinsi unavyomtembelea mara kwa mara na jinsi unavyomjali na mkarimu daima. Ameniambia umemsaidia mara nyingi wakati alipokuwa mgonjwa na hata umeomba umpeleke mjukuu wangu kwenye darasa la wasichana.

Kwa miaka 10 iliyopita, yeye, mwanangu, na familia yao wameishi umbali wa mamia ya maili kutoka kwetu. Nimekuwa nikiomba kwamba watu wengine wawapende na kuwajali kama mimi nifanyavyo, na nimeomboleza kwa machozi kwa Baba wa Mbinguni kwamba wengine wawafikie kama ambavyo mimi ningefanya kama wangeishi jirani na sisi. Kutokana na kile asemacho Joann wewe umekuwa jibu la maombi yangu.

Hata kama Joann na mwanangu hawatii Neno la Hekima na hawahudhurii kanisani, bado wao ni watu wema na wanawependa watoto wao. Kwa namna fulani macho yako hayakugubikwa na moshi wa sigara ya Joann. Ukumhukumu yeye kama atahudhuria kanisa au la. Uliweza kumjua na kujifunza kuwa yeye ni mama mwenye upendo ambaye anataka binti yake ahudhurie kanisa na kupata ushuhuda. Na Joann alipofanyiwa upasuaji, ulimletea chakula badala ya kushangaa na kuwaza kuwa labda amejiletea mwenyewe matatizo hayo ya kiafya.

Ni shukrani iliyoje kwangu kwamba wewe umekuwa mfano kwa binti-mkwe wangu huyu. Anaweza kuiga mfano wako huu kama mtu anayemjali kila mtu na mwenye kujitolea kuonyesha upendo. Aliniambia kwamba siku moja ulipokuwa huna gari, ulitembea kwa miguu zaidi ya maili moja kwenda nyumbani kwake pamoja na watoto wako kumpelekea biskuti.

“Nimekuwa nikikuwaza wewe na mama yako na nilitamani kufanya kitu kizuri kwa ajili yenu—kwa sababu tu,” ulimwambia.

Natamani ningeweza kukuambia ni kiasi gani ninashukuru kwa kujitoa kwako katika wito wako kama mwalimu wa kutembelea. Wewe ni mfano wa wale wanawake ambao, tangu siku zile za Nauvoo, wametumikiana wao kwa wao kupitia ualimu wa kutembelea kwa upendo na kuinuana. Umeonyesha huduma na upendo huo kwa namna uliyomtembelea kwa upendo binti-mkwe wangu asiyehudhuria kikamilifu kanisani.

Asante.