2016
Ushuhuda wa Ethan.
April 2016


Ushuhuda wa Ethan

Mwandishi anaishi Utah, Marekani.

Ilionekana kama kwamba kila mtu isipokuwa Ethan alikuwa na ushuhuda.

“Sikiliza, sikiliza. Roho Mtakatifu atanong’ona. Sikiliza, sikiliza sauti ndogo tulivu” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 106).

Picha
ethans testimony

Ethan aliketi katika mkutano wa mfungo na ushuhuda na kutazama juu kwenye mimbari. Rafiki yake wa dhati, Sam, alikuwa akitoa ushuhuda. Rafiki yake Sarah alikuwa ameketi kwenye jukwaa, akisubiri nafasi yake. Sam aliongea kuhusu mradi wa huduma alioufanya. Alisema alikuwa na ushuhuda kuhusu huduma. Sarah alitoa ushuhuda kuhusu familia. Babake Ethan pia alienda kwenye jukwaa. Aliongea kuhusu kazi ya hekalu. Wote walishuhudia kuwa Kanisa ni la kweli. Ilionekana kama kwamba kila mtu isipokuwa Ethan alikuwa na ushuhuda.

“Nina ushuhuda kuhusu nini?” Ethan aliwaza.

Alifikiria kuhusu miaka michache iliyopita wakati ambapo yeye na marafiki zake walibatizwa. Mwalimu wake wa Msingi Dada Calder, alikuwa ametoa hotuba kuhusu Roho Mtakatifu.

“Roho mtakatifu anaweza kukufanya ujisikie kuwaka moyoni mwako. Anaweza kukusaidia ujue kile kilicho cha kweli,” alikuwa amesema. “Na hivyo ndivyo unavyopata ushuhuda wa kile ambacho unaamini.”

Ethan alijaribu kutenda haki ili aweze kumsikia Roho Mtakatifu. Alisoma maandiko na kusali. Lakini hakuwa amewahi kuwa na hisia ile ya kuwaka ambayo watu huiongelea. Je, hilo lilimaanisha hakuwa na ushuhuda?

Swali hili lilikwama akilini mwa Ethan siku nzima iliyofuata. Alikuwa bado anafikiria wakati ambapo yeye na Sam walikuwa wakicheza mchezo wa kibao cha kuteleza baada ya shule. Aliwaza jinsi ambavyo angemuuliza Sam kuhusu swali hilo.

“Halo, Sam,” Ethan hatimaye aliuliza, “je, ulikuwa na hofu wakati ulipotoa ushuhuda wako jana?”

Sam aliruka kutoka kwenye ubao mtelezo na kutembea hadi kwenye nyasi. “Sio kweli,” alisema, huko akiketi chini. “Nimetoa ushuhuda wangu kwenye mkutano wa jioni ya familia kabla yake.”

Ethan alijiunga naye na kuweka ubao mtelezo wake mapajani pake. “Lakini ni namna gani ulijua kuwa una ushuhuda?”

“Basi, niliomba na nikajisikia vizuri juu ya jambo hilo.”

Ethan aliitikia polepole kwa kichwa na kuzungusha gurudumu kwa mkono wake. Kwa namna fulani alitaka naye ajisikie hivyo pia.

Usiku huo, wakati ambapo nyumba ilikuwa na giza na tulivu, Ethan alipiga magoti kando ya kitanda chake kuomba.

“Baba wa Mbinguni,” alisema, “tafadhali nisaidie nipate ushuhuda. Nisaidie nijue kuwa Kanisa ni la kweli. Kuwa Joseph Smith alikuwa Nabii. Na kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli.”

Katikati ya maombi yake, Ethan alitulia. Alifikiri kwa dakika chache. Kisha akajiuliza, “Je, ninajua chochote hadi sasa?”

Na kisha hisia ya utulivu na amani ikaja juu yake. Haikuwa hisia ya nguvu na yenye kuwaka. Lakini Ethan alijua, huyo alikuwa Roho Mtakatifu.

Wazo lilikuja akilini mwa Ethan. “Ninajua kwamba ninajua.” Na alipofikiria kuhusu hayo, aligundua kuwa alikuwa amewahi kuwa na hisia hii ya amani hapo awali.

Wakati wowote aliposoma Kitabu cha Mormoni, alijisikia vizuri na sahihi. Sasa alijua kuwa hisia ile ilikuwa ni Roho Mtakatifu akimshuhudia. Alipoenda kanisani na alijisikia vizuri na ni sahihi kuwa pale, huyo alikuwa ni Roho Mtakatifu pia. Alikuwa tayari ameanza kupata ushuhuda.

Hakuhitaji kujua kila kitu kwa wakati huu. Lakini alijua ya kwamba Roho Mtakatifu alikuwa halisi na angeweza kumsaidia kuendelea kujenga ushuhuda wake.

Ethan akaanza kuomba tena. Lakini wakati huu ilikuwa ni kusema asante.