2016
Nafasi Yetu
April 2016


Nafasi Yetu

Nimebarikiwa kwa Kutii Sheria ya Zaka

Sabrina T., São Paulo, Brazil

Picha
young woman with cell phone

Nilipokuwa mdogo, familia yangu ilipitia katika changamoto nyingi za kifedha ambazo zilidumu hadi nilipokuwa na umri wa miaka 10. Baba yangu hakuweza kupata kazi nyingine, kwa hivyo alifanya kazi kama mchuuzi wa mitaani na alipata pesa kidogo sana. Mama yangu alikaa nyumbani kunitunza mimi pamoja na kakangu mdogo.

Lakini hata tukipitia katika taabu hizo nyingi, tulikuwa na ushuhuda wa kulipa zaka na kutoa matoleo mengine. Tulilipa zaka yetu kila mwezi na hatukukosa chochote. Tunajua kwa uhakika kwamba tunazidi kubarikiwa kwa sababu ya wema Wake Bwana usio na mwisho na kwa sababu Yeye hutimiza ahadi Zake tunapokuwa waaminifu kwa amri Zake.

Siku zetu za majaribu ya kifedha hatimaye ziliisha. Baraka ambazo Bwana ametupa katika miaka hii michache iliyopita zimekuwa za ajabu.

Ninajua kwa wale ambao hulipa zaka kwa uaminifu pamoja na kulipa matoleo yao kwa upendo na lengo la kubariki maisha ya wengine, hakuna watakachokosa na jambo bora zaidi laweza kuwatokea, kama ilivyotufanyikia kwangu mimi na familia yangu. Baraka zitazidi. Ninajua hili. Niliishi hivi.

Mwaminifu Katika Kila Kitu

Alivsi H., Jalisco, Mexico

Mwanzoni mwa kila muhula shuleni, sisi hupata seti za bure za bidhaa vikiwamo daftari, ajenda, na sampuli moja ya bidhaa ngeni bila mpango maalumu. Mwaka mmoja nilikuwa kwenye foleni kupokea seti yangu na nikagundua kuwa sampuli niliyopata ilikuwa hasa ya manufaa kwangu.

Mwishowe niliona kuwa walikuwa wakitoa sampuli mbili za bidhaa aina moja. Ingekuwa rahisi kurudi tena foleni na kupokea seti ya pili na niliamua kufanya hivyo. Licha ya yote, ilikuwa ya bure, na mimi nilihitaji bidhaa hiyo.

Nilipitia msalani kwa haraka, ambako niliona simu ya mkononi ambayo msichana fulani alikuwa amesahau kwa bahati mbaya. Ilikuwa mojawapo ya aina ya kisasa, na nilikuwa nimeipoteza simu yangu wiki moja kabla siku hiyo. Lakini hata sikuwazia kuichukua. “Huo ni wizi,” Nilijiambia.

Kisha, njiani kwenda kupokea seti yangu ya pili ya bidhaa za bure, niligundua kuwa hiyo ingekuwa udanganyifu kama kuchukua ile simu kwa sababu ningedanganya na kusema kuwa sikuwa nimepewa mbeleni.

Nilikuwa na shukrani kwa tukio hili dogo ambalo lilinifundisha somo kubwa. Niliirudisha simu na kwenda nyumbani na daftari moja pekee, ajenda moja, na sampuli moja ya bidhaa, lakini nilijisikia vizuri kwa kuwa mwaminifu na mkweli katika mambo yote, bila kujali ni kidogo kiasi gani.