2016
Alma Alitubu
April 2016


Mashujaa wa Kitabu cha Mormoni

Alma Alitubu

Picha
Alma repented

Alma alikuwa kuhani wa Mfalme muovu Nuhu. Alimsikiliza nabii Abinadi akifundisha kuhusu amri. Alma alijua alihitaji kubadili maisha yake na kumfuata Mungu badala ya kufanya mambo maovu. Aliandika yale ambayo Abinadi alifundisha. Alianza kuwafundisha wengine injili. Baadaye alikuwa na familia na akampa mwanawe mmoja jina la Alma.