2016
Baba wa Mbinguni Amesema Nami kwa Njia ya Hotuba ya Mkutano Mkuu
April 2016


Vijana

Baba wa Mbinguni Amesema Nami kwa Njia ya Hotuba ya Mkutano Mkuu

Mwandishi anaishi Sergipe, Brazili.

Nilikuwa na shaka juu kuhusu kile nitasoma Chuo kikuu. Watu wengi walizungumza vibaya juu ya kozi ambayo nilitaka kuichukua, hivyo nikaomba kwa Bwana ili kuona kama Yeye alikubaliana na uamuzi wangu.

Jibu langu lilikuja siku iliyofuata wakati nikiwa nasoma mahubiri ya mkutano mkuu katika Liahona. Nilijisikia kana kwamba Baba wa Mbinguni alikuwa akiniambia kwamba Yeye asingeweza kunichagulia—huu ulikuwa ni uamuzi wa kufanywa na mimi pekee yangu. Nilijua kwamba lolote nitakalochagua, nitapaswa kufanya kazi kwa bidii ili nifanikiwe.

Ninajua kuwa sala yangu ilijibiwa. Uthibitisho wa Roho Mtakatifu ulinisaidia kufanya uamuzi. Nimejifunza kutoa jitihada zangu zote na ninajua kwamba Baba wa Mbinguni atanisaidia.