2016
Wakati Ambapo Pornografia Inaipiga Nyumba—Wake na Waume Wote Wanahitaji Kupona .
April 2016


Wakati Ambapo Pornografia Inaipiga Nyumba—Wake na Waume Wote Wanahitaji Kuponywa

Nimeshuhudia mimi mwenyewe kuwa nguvu za Mwokozi za kuponya zinaweza kuwafikia wake na vilevile waume wakati ambapo waume wanapambana na utawaliwa wa pornografia.

Picha
husband, wife, and Christ

Picha za kielelezo ni za mifano

Katika muda wa miezi sita ya kwanza kama askofu, nilikuwa na wanandoa kadhaa katika kata yangu waliokuja kwangu katika imani kunieleza kuhusu mapambano ya waume zao na matumizi ya pornografia. Katika baadhi ya visa, mke alikuwa bado angali katika mshituko wa kutambua siri hiyo ya kusikitisha; wengine walikuwa na habari kwa miezi au miaka mingi.

Nimemwonea huruma kila mmoja wa wanandoa hawa na nimejionea nguvu za Mwokozi za ukombozi kadiri nilivyokuwa nikishauriana mara kwa mara na kwa uangalifu na kila mmoja wa ndugu hao ili kuwasaidia “kuikata minyororo … ambayo ingewafunga [wao]” (2 Nefi 9:45)

Pengine mibubujiko mikuu ya Roho imekuja, hata hivyo, pale nilipokutana na wake zao. Nimegundua kwamba, huku baadhi ya vidonda vikiwa ni vya hivi karibuni na vingine vimekuwa makovu kutokana miaka mingi ya kuathiriwa, kina dada hawa wote hukabiliana na maumivu makubwa ya kiroho yanayosababishwa na maswali kama vile, “Mimi nimefanya nini kilichosababisha yeye asivutiwe na mimi?” au “Ni kwa nini yeye anataka kudhania kuwa yuko na mtu mwingine badala kuwa na mimi?”

Kwa sababu ni mume ambaye amefanya makosa, ni rahisi kwa askofu kuonelea kuwa ni mume ndiye anayehitaji zaidi funguo za kufungua nguvu za Mwokozi za uponyaji, lakini nimejifunza kuwa mahitaji ya mke kuponywa uchungu na maumivu ni makubwa kama vile yalivyo mahitaji ya mume kuponywa dhambi na tamaa zisizotulizika.

Katika mahubiri yake kwa Wanefi, nabii Yakobo aliwashutumu wanaume kwa kukosa kuwa waaminifu kwa wake zao, “ambao wengi wao mawazo yao [yalikuwa] ya upole sana na wasafi kimwili na wadhaifu mbele ya Mungu, kitu ambacho ni cha kupendeza kwa Mungu” (Yakobo 2:7). Aliendelea: “Mmevunja mioyo ya wake zenu wapole … kwa sababu ya mifano miovu mbele yao; na vilio vya mioyo yao kwa sababu yenu vinamfikia Mungu” (Yakobo 2:35). Nimeshuhudia vilio hivi kwa macho yangu. Mara nyingi vinatokana sio tu na hisia za kina za mke kusalitiwa zilizosababishwa na mumewe kutawaliwa na pornografia lakini pia kutokana na maneno ya kudhalilisha na tabia ya ugomvi au ukali inayotokea mara nyingi kama athari ya mapambano yake ya ndani ya mume mwenyewe. Sio jambo geni, kwa kweli, kwa mwanaume ambaye tabia zake zimejulikana kumtupia mkewe lawama kwa sababu ya hizo tabia zake, akidondoa vitendo mbalimbali ambavyo amefanya au kukosa kufanya. Cha kusikitisha zaidi, si ajabu pia kwa mkewe kuanza kutafakari haya na pengine hata kuamini lawama hizi.

Mojawapo ya wanandoa kama hawa waliketi ofisini mwangu baada ya mume kufichua mazoea yake ya kutazama pornografia aliyokuwa nayo tangu ujana wake. Wakati alipokuwa akisikiliza somo la Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama juu ya mahubiri ya Dada Linda S. Reeves katika Mkutano Mkuu wa Aprili 2014, “Ulinzi dhidi ya Pornografia—Nyumbani Ambamo Kristo ni Kitovu Chake,” mkewe alianza kutambua katika tabia za ukorofi za mumewe kuja kwake mielekeo ambayo mwalimu alikuwa akieleza. Kufuatia somo hilo, mke alimkabili mumewe na swali hilo, na alikiri siri hiyo aliyokuwa akificha kwa muda mrefu sana. Kujistahi kwake ambako tayari kulikuwa kumeathirika mno sasa kulijumuishwa na chuki inayowaka. Wakati wa mkutano wao wa kwanza nami, walihangaika kuona ni kwa namna gani ndoa yao ingeweza kuendelea. Niliwahakikishia kuwa kulikuwa na matumaini, nikatoa ushauri wa kwanza, kisha nikawaalika tena waje na wakutane nami kila mmoja peke yake.

Pamoja na maombi ya bidii ambayo nilitoa katika matayarisho ya mikutano hiyo, pia nilifanya mrejeo wa mapendekezo yaliyotolewa katika Ministering Resources katika LDS.org, hasa katika misaada kwa ajili ya kuwasaidia wanandoa ambao waume au wake zao ni watumiaji wa pornografia, ambapo nilisoma yafuatayo: “Onyesha upendo na masikitiko yako kwake binafsi, vilevile kwa mumewe au mkewe. Bainisha kuwa yeye si wa kulaumiwa kwa ajili utumiaji pornografia wa mwenza wake au tabia yake isiyo ya kuridhisha na hatarajiwi kuvumilia tabia ya unyanyasaji.”

Nilipokutana na dada huyu, nilitii ushauri huu na kuongezea hakikisho kuwa vitendo vya mumewe kamwe havikusababishwa na yeye, wala kuhusu kitu ambacho alikuwa amekifanya au amekosa kufanya, lakini yalikuwa yanahusu mapambano ndani ya mume mwenyewe. Nilitazama wimbi la ahueni na faraja likimfunika alipokuwa akimeza maneno haya na kusikia uthibitisho wa Roho kuwa hakika yalikuwa ya kweli. Mwishoni mwa mahojiano, aliomba ikiwa ningeweza kumpa baraka za ukuhani. Niligundua kuwa ilikuwa ni kwangu mimi pekee ndiko ambako angeweza kunijia kwa ajili ya baraka kama hizi, kwa vile alipendelea jambo lake hili lingesalia kuwa lake binafsi na si la familia wala marafiki.

Ili kusaidia katika mchakato wa uponyaji huu, nilimwalika mumewe kuhudhuria mkutano wa mtaani wa kikundi cha walio katika hatua za uponyaji cha Watakatifu wa Siku za Mwisho waliotawaliwa na mazoea mabaya, nilimhimiza mkewe kukutana na kikundi kama hicho cha waume au wake na wana familia. Alinielezea kuhusu faraja aliyokuwa akiisikia kutokana na kukutana na kina dada wengine ambao walielewa alivyokuwa akiteseka na matumaini iliyompa kuona wanandoa ambao walikuwa wamepitia majaribu kama yake na walikuwa wameweza kukabiliana nayo wakiwa pamoja.

Miezi kadhaa imepita sasa tangu mkutano wangu wa kwanza na wanandoa hawa, na upendo wangu na uhusiano wangu kwao umeongezeka kama matokeo ya mikutano yetu mingi. Huku nikitambua kuwa safari yao haitakosa changamoto, ni furaha kwangu kufahamishwa kila mwezi unapopita kuwa mumewe amejiepusha na tamaa na pornografia na kumwona mkewe akizidi kujiona mwenye kustahiki ndani yake na kujiamini, kitu ambacho tayari kinaonekana wazi.

Katika mahojiano ya hivi karibuni nao, uchungu na machozi yaliyokuwepo katika mikutano yetu ya awali yamebadilishwa na sasa ni tabasamu za mara kwa mara na hata vicheko. Lakini pengine matokeo makubwa zaidi yamekuwa matumaini—matumaini kuwa sio tu kuwa ndoa yao inaweza kuendelea lakini pia ina uwezo wa kuwa kitu kizuri na cha kuwainua.

Ninatambua kuwa, kwa bahati mbaya, sio wanandoa wote wanashuhudia matokeo haya. Baadhi ya ndoa huvunjika wakati mtawaliwa na pornografia anapokataa kuchukua hatua ya kurekebika. Bila kujali ni njia ipi mume atachagua, hata hivyo, nimejifunza kuwa ushauri wa kuwahudumia wake hawa umetokana na maongozi ya kiungu. Ninatumaini kuwa hakutakuwepo na dada yeyote katika hali hii atakayehisi kuwa hatiliwi maanani, anahukumiwa vibaya, au kukosa kueleweka na askofu wake. Huduma ya askofu ni njia muhimu ambayo kwayo Mwokozi anadhihirisha nguvu Zake kikamilifu ili kuponya kila moyo—hata ile ambayo “ilikuwa imejeruhiwa na vidonda vikubwa” (Yakobo 2:35).

Picha
family studying scriptures

Chini: Kerri alipata kuvunjika moyo alipogundua changamoto iliyomkamata mume wake kuhusu pornografia, lakini alipata matumaini na uponyaji kupitia kwa Yesu Kristo na Upatanisho Wake.