2016
Mitume hufanya nini?
April 2016


Majibu kutoka kwa Mtume

Je, Mitume hufanya nini?

Kutoka kwa Mzee na Dada Bednar wakati wa Matangazo yao ya Uso kwa Uso Kote Ulimwenguni.

Picha
what do Apostles do

Mitume ni watumishi wa Bwana. Wao husafiri kwenda kuwatembelea waumini wa Kanisa kote duniani.

Mara ya kwanza niliposafiri kama Mtume, nilikutana na bwana ambaye alikuwa na wakati mgumu kutii Neno la Hekima. Nilimwambia, “Bwana alinituma hapa kukupa ujumbe rahisi sana: ‘Unaweza kufanya hivi. Ninakuahidi utapata msaada Wake unapokabiliwa na changamoto hii.’”

Kuna uwezekano wa Bwana kutuma mmoja wa Mitume Kumi na Wawili nusu ya mzunguko wa dunia ili kumsaidia tu mtu mmoja? Jibu ni ndio. Yeye hufanya hivyo wakati wote.