2019
Bob na Lori Thurston—Misheni ya Cambodia Phnom Penh
Aprili 2019


Taswira za Imani

Bob na Lori Thurston

Walitumikia Misheni ya Cambodia Phnom Penh

Picha
senior missionary couple

“Tulipogundua tulikuwa tumeitwa kutumikia huko Misheni ya Cambodia Phnom Penh, tulilia machozi. Tulikuwa na furaha! Kaka Bob Thurson anasema. “Tusingeichagua Cambodia, lakini ni zawadi iliyoje! Ni baraka iliyoje!” Dada Thurston anasema.

Picha
senior missionary hugging Cambodian woman

Akina Thurstons wanahisi muunganiko maalumu na watu wa Cambodia. “Tunawapenda, na tumehisi upendo huo kwetu pia,” Dada Thurston anasema. “Watu wa Cambodia wametuonyesha ukarimu mkubwa.”

Picha
senior couple visiting members

Kati ya vyote akina Thurstons walivyokuwa navyo katika misheni yao, wanathamini sana fursa ya kuwatembelea waumini katika nyumba zao.

Picha
senior missionary with Cambodian woman

Dada Thurston anakumbuka kuwatazama wale aliowatumikia huko Cambodia na kufikiri, “siwezi kusubiri mpaka nikuone katika maisha yajayo, kisha nitaweza kweli kukuambia mambo yote ninayohisi kwa ajili yako na upendo nilionao kwako.”

Katika misheni yao ya kwanza pamoja, Bob na Lori Thurston walijifunza kwamba kuhudumu kwenye maana kunaweza kufanyika licha ya vikwazo vya lugha na tofauti za utamaduni kwa sababu sote tu watoto wa Mungu.

Leslie Nilsson, Mpiga picha

Picha
Sister Thurston hugging grieving girl

Bob:

Kabla ya mimi na Lori kuoana, tulizungumzia kuhusu kutumikia misheni wakati tutakapokuwa tumestaafu. Sote tulikuwa tumetumikia misheni kabla. Lori alitumikia huko Kobe, Japan, na mimi nilitumikia Brisbane, Australia. Wakati hatimaye tulipofika kwenye mzunguko wa kuwa tayari kustaafu, tuliwaambia watoto wetu kwamba tulitaka kutumikia misheni nyingi.

Tulikuwa na bahati ya kuweza kustaafu tukiwa bado vijana. Tulipokuwa tumesikia kwamba baadhi ya wanandoa wazee hawawezi kutumikia katika baadhi ya maeneo kama vile katika nchi zinazoendelea kwa sababu ya masuala ya kiafya na changamoto zingine, tuliwaza, “Sisi bado hata hatujafika miaka 60. Tuna afya nzuri, hivyo tutumieni!”

Nilistaafu siku mbili tu baada ya miaka yangu 56 ya kuzaliwa. Kwa kweli tulipokea wito wetu wa misheni wakati bado nikiwa kazini. Tulipofungua wito wetu na kukuta kwamba tulikuwa tumeitwa kutumikia huko Misheni ya Cambodia Phnom Penh, tulilia machozi. Tulikuwa na furaha!

Lori:

Cambodia haikuwa hasa kwenye rada yetu. Nilidhani tungeenda Afrika au pengine. Tulianza kujiuliza wenyewe, “SAWA, ni uzoefu gani unatusubiri?” Tusingeichagua Cambodia, lakini ni zawadi iliyoje! Ni baraka iliyoje! Bwana ni mwerevu kuliko sisi tulivyo. Anatupeleka pale tunapopaswa kuwa.

Tulitumikia misheni inayoshughulikia masuala ya kibinadamu. Tulifanyia kazi miradi ya Misaada ya Hisani ya Kanisa, kujaza ripoti, na kuomba miradi mipya. Tulipitia pia miradi ya awali kama vile visima ambavyo vilikuwa vimechimbwa miaka miwili kabla. Tuliishia kutumikia katika njia zingine pia.

Tulihudhuria mikutano ya vigingi na kata ili kusaidia kuwapa mafunzo viongozi na wamisionari, tulikagua nyumba za wamisionari na kuwatembelea waumini katika nyumba zao. Tulifanya mambo kadha wa kadha kusaidia misheni ifanye kazi vizuri.

Hakuna siku mbili zilizofanana katika misheni yetu. Baadhi ya siku tulikuwa nje msituni, magoti yakiwa ndani kabisa ya maji au matope. Siku zingine zilitumika katika ofisi ya misheni. Pamoja na wamisionari wa Masuala ya Umma, tulitembelea Wizara ya Madhehebu na Dini. Huko Cambodia, neno “dhehebu” siyo lazima liwe kitu kibaya. Dini rasmi ni Budha—kingine chochote kinachukuliwa kama dhehebu. Tulitembelea wizara kusaidia kuweka kitangulizi kwamba Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni taasisi nzuri na inaweza kuaminiwa.

Tulijenga maelewano mazuri na wao, na walikuwa wepesi kutuita kwa ajili ya usaidizi. Wangetuita na kusema, “Tumepata mafuriko, na tunahitaji chakula kwa ajili ya familia 200 ambazo zimehamishwa. Walijua wangeweza kutegemea Kanisa kupata vitu ambapo vilihitajika haraka na kuongezea vitu ambavyo walikosa.

Ni uzoefu gani tuliopata Cambodia? Taja wowote, yawezekana tuliupata! Tumekaa kwenye sakafu duni—mara nyingi za mchanga tu au mwanzi—ndani ya nyumba za kawaida. Tumeingia pia kwenye nyumba za kifahari za viongozi wa serikali. Bob hata alitumikia katika urais wa tawi kwa muda.

Bob:

Rais wa misheni aliniita na kusema, “Wewe, nataka uwe mshauri wa pili katika tawi.” Mwaka mmoja na nusu baadaye, nilikuwa kwenye chumba cha ibada ya kufunganishwa cha Hekalu la Hong Kong China pamoja na rais wa tawi niliyetumikia pamoja naye. Alikuwa akienda hekaluni kwa mara ya kwanza! Yeye na familia yake walikuwa wamewekaakiba pesa na kujaribu mara saba kufika hekaluni, lakini kungekuwa na ajali, au mtu angeugua. Kitu fulani daima kingetokea. Baada ya miaka saba, walikuwa wameweka akiba dola 40 tu.

Mara tatu katika misheni yetu, tuliweza kuwasaidia Watakatifu wa Siku za Mwisho huko Cambodia kuhudhuria hekaluni. Tuliwachukua marais wengi wa matawi ambao walikuwa wakifanya usahili kwa ajili ya vibali vya hekaluni lakini wao wenyewe hawakuwahi kufika hekaluni. Angalau huko Cambodia, wanandoa wazee wangeweza kuzisaidia familia hizi katika njia yao kwenda hekaluni. Wanahitaji kuwa na mtu pamoja nao kwa sababu hawajui jinsi ya kusafiri kwa ndege. Wengi wahakuwahi hata kusafiri kwa basi! Na sasa wanatakiwa kusafiri kwa ndege kwenda Hong Kong na kuelekea hekaluni. Ilikuwa vigumu kwao kufanya hivyo peke yao. Tunashukuru kwa ajili ya Mfuko wa Usaidizi wa Hekaluni ambao ulisaidia kuwashughulikia.

Lori:

Kuwa muumini wa Kanisa huko Cambodia kunaweza kuwa changamoto. Kama nchi, Cambodia haina utamaduni wa Sabato. Kila mtu anayekuja kanisani hana budi kujitoa ili kuwa pale.

Pia, Cambodia ina asilimia sita ya Waislamu na asilimia mbili tu ya Wakristo—waliobaki ni Wabudha. Kuhama kutoka mtindo wa maisha wa Kibudha kwenda mtindo wa maisha wa Kikristo ni vigumu sana. Baadhi ya watu bado wanapoteza kazi zao, na mara nyingi wanatengwa na wengine katika maeneo yanayowazunguka.

Zaka pia ni suala kubwa. Viongozi wa Kibudha watazunguka kila asubuhi na kuomba mchele na kiasi cha pesa, na watu wamezoea hilo. Lakini kuchukua hundi yako ya malipo na kutoa sehemu yake kwa ajili ya zaka ni suala kubwa.

Wengi wamekuwa na kiwewe katika maisha yao. Kwa sababu ya Khmer Rouge, mfumo wa kikomunisti ambao ulitawala Cambodia mwishoni mwa miaka ya ’70, kila mtu mwenye zaidi ya miaka 40 ana hadithi yake binafsi ya kutisha. Sikukutana na yeyote ambaye hakuathiriwa na mfumo huo. Kila mmoja alikuwa na wanafamilia waliouwawa. Japokuwa wamepitia mengi, sikuweza kuamini jinsi walivyokuwa imara, jinsi walivyokuwa tayari kujaribu. Lakini nyuma ya uponaji wao, wengi bado wanajiona hawafai. Wengi hawahisi kama wao ni wa muhimu au wenye thamani yoyote.

Ilikuwa ya kupendeza kuona jinsi gani injili ya Yesu Kristo ilivyowasaidia kustawi. Wakati ambapo wangegundua kwamba hawakuwa tu wa kupendeza lakini pia mtoto wa Mungu, wangesema, “Unatania? Sasa nina kitu cha kuchangia.”

Kanisa kweli linakwenda kustawi huko Cambodia. Watu wa kupendeza wamekuwa wakiongozwa Kanisani. Watakatifu huko ni waanzilishi, na wale ambao kweli wanaikubali injili wanabarikiwa katika njia nyingi kwa sababu wanapata kumjua Mwokozi. Ni ya kupendeza sana.

Tuna waumini wengi na kata imara kuzunguka eneo linaloitwa “Trash Mountain,” ambalo ni jalala la wazi ambapo watu wanaishi. Waumini katika eneo hilo ni waokotaji na wakusanyaji. Wanajipatia pesa kwa kutengeneza upya taka za plastiki na alumini ambazo wanazipata jalalani. Wanaishi kwenye vijumba vidogo sana ambavyo tumeingia ndani yake mara nyingi sana.

Bob:

Siku moja tuliweza kusikia sauti ya muziki, na tuligundua hema lilikuwa likipigwa. Huko Cambodia, hiyo aidha humaanisha mtu anafunga ndoa au mtu amefariki.

Lori:

Tuligundua kwamba mama wa watoto watano au sita alikuwa amefariki punde. Hakukuwa na mume wa kumzungumzia. Watoto waliamka tu na kugundua mama yao alikuwa amefariki.

Binti mmoja alikuwa tu akilia kwa sauti ya makelele. Kupitia mtafsiri, binti alisema, “mimi ndiye mtoto wa kwanza. Nina wadogo zangu hawa wote. Sijui nitafanya nini.”

Nilimnyanyua juu kwenye mikono yangu. Ningewezaje kutofanya hivyo? Msichana huyu punde tu alikuwa amempoteza mama yake. Nilizungumza naye kwa kiingereza na kusema, “najua hunielewi, lakini ninaahidi utamwona mama yako tena. Utakuwa SAWA. Hutaachwa peke yako.”

Uzoefu wa aina nyingi kama huu umetupatia muunganiko maalumu na watu wa Cambodia.

Tulihisi upendo ule kwetu pia. Watu wa Cambodia walituonyesha ukarimu mkubwa. Tunawapenda kwa sababu wao ni watoto wa Mungu. Wao ni kaka na dada zetu.

Kwa baadhi ya watu, nakumbuka kufikiria, “siwezi kusubiri mpaka nikuone katika maisha yajayo, kisha nitaweza kweli kukuambia mambo yote ninayohisi kwa ajili yako na upendo nilionao kwako, na kile ninachovutiwa nacho kuhusu wewe, kwa sababu siwezi kusema hilo sasa.”

Misheni yetu imetubariki katika njia nyingi. Baadhi ya watu husema, “sijui kama ninaweza kutumikia misheni. Siwezi kuwaacha wajukuu zangu.” Tulikuwa na wajukuu wa kiume wadogo watano wakati tulipoondoka, miaka mitano, minne, mitatu, miwili na mwaka mmoja. Wajukuu wawili wa kike walizaliwa tulipokuwa tumeondoka. Nitatunza beji zangu mbili za umisionari huko Cambodia na kuwapatia watoto wangu wawili wa kike ili waje wajue kwamba Bibi hakuwepo kwa sababu Bibi alikuwa akifanya kile Bwana alichomtaka afanye.

Bob:

Kuna njia nyingi za kumtumikia Bwana kama wamisionari. Tunaweka moyoni kile Mzee Jeffrey R. Holland alichosema kuhusu huduma ya mmisionari mzee. Alisema, “ninaahidi utafanya mambo kwa ajili ya [familia yako] katika huduma ya Bwana ambayo, dunia zisizo na mwisho, usingeweza kufanya kama ungebaki nyumbani kusubiri kuyafanya. Ni zawadi gani kuu mabibi na mababu wangeweza kuwapa kizazi chao zaidi ya kusema kwa matendo vile vile kwa maneno, “katika familia hii tunatumikia misheni!’ “We Are All Enlisted,” Liahona, Nov. 2011, 46.]”