2019
Maisha ni Masafa Marefu: Vijana wa Ugiriki
Aprili 2019


Maisha ni Masafa Marefu

Vijana hawa Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaishi leo ambapo Mtume Paulo aliishi wakati wa kipindi cha Agano Jipya. Na wanaishi kwa maneno yake.

Picha
Bryana

“Nimejifunza kwamba injili inafanana kila mahali. Kuishi ughaibuni, nimejifunza kufokasi kwenye kweli za injili na kuhisi Roho badala ya kuvutwa na utamaduni.” —Bryana W., 15

Picha
Marie

“Niliandika neno kumbuka kwenye kioo changu ili kukumbuka yale yote yaliyotokea mwaka huu: KNV, kambi ya Wasichana, seminari. Inanisaidia kukumbuka wapi nimetoka.” —Marie H., 17

Picha
Lizzie

“Ninajua kwamba ninapoenda seminari ninaweza kuhisi kuridhika kujua kwamba ninafanya kile ninachohitaji kufanya, na ninajua kwamba kila kitu kitakuwa SAWA.” —Lizzie T., 17

Picha
Loukia

Loukia C., 15, alitoa ushuhuda wake kwa mara ya kwanza kwenye kambi ya Wasichana na baadaye alibatizwa.

Picha
Haig

“Sehemu niliyoipenda zaidi ya KNV ilikuwa michezo, dansi, na mikutano ya makundi, ambayo ilikuwa mikutano na tafakari ya ibada za asubuhi. Ilinisaidia kuwa mwenye msaada zaidi na mvumilivu na kushukuru zaidi kwa ajili ya maandiko.” —Haig T., 14

Picha
Alexis

“Kwenye KNV, tulianza kuwa kundi na ilituimarisha. Ilisaidia kubadilisha na kushawishi programu ya vijana wa Ugiriki kwa sababu sasa tunajuana vizuri zaidi.” —Alexis H., 18

Picha
Irini

“Kuimba jukwaani kwenye KNV ilikuwa ni mojawapo ya jambo la kijasiri nililowahi kufanya na moja ya nyakati za muujiza nilizowahi kuwa nazo. Kwa sasa, nimejifunza jinsi tulivyo wa muhimu katika ulimwengu huu wa kupendeza.” —Irini S., 17

Picha
Winifred

“Kwenye kambi ya Wasichana nilijifunza kwamba maisha ni kama mbio za masafa marefu. Ilisaidia kukuza imani yangu, kujua kwamba tunapaswa kuendelea katika njia iliyo sahihi, kama vile tunakimbia mbio za masafa marefu. Uzoefu huo unanisaidia kukuza ushuhuda wangu na kuendelea kuwa na imani na kubaki kwenye njia sahihi.” —Winifred K., 14

Picha
Pavlos

“Nilipenda sana kuona jinsi ilivyo kuwa pamoja na vijana walio na imani inayofanana. Nilihisi kama sote tulikuwa tumeunganishwa katika njia maalumu, zaidi tu ya kujua jina la kila mmoja.” —Pavlos K., 15

Picha
Joshua

“Ninafurahi kwamba nilipata fursa ya kukutana na vijana wengine ambao wanapitia mambo sawa na yale ninayofanya kila siku.” —Joshua K., 17

Picha
Olivia

“KNV na kambi ya Wasichana vina hisia zinazofanana bila kujali popote unapoenda ulimwenguni. Nilifurahia kambi ndogo ya Wasichana kwa sababu ilikuwa rahisi kuwa karibu na kila mmoja.” —Olivia H., 15

Picha
Irene

“Mimi si muumini wa Kanisa, lakini ninakuja kila wiki ninayoweza kuja. Ninapendezwa na kile wasichana wanachokisimamia.” —Irene C., 14

Picha
youth in Greece

Miezi michache iliyopita, darasa la seminari lilikutana katika Kilima cha Maazi, karibu na Atheni, Ugiriki, ambapo Mtume Paulo aliwahi kutoa mahubiri yenye nguvu (ona Matendo ya Mitume 17:22–34). Wanafunzi walizungumza kuhusu ushawishi wa seminari katika maisha yao, ikijumuisha mafundisho ya Paulo.

“Kuishi Ugiriki kunafanya Agano jipya kuwa halisi,” anasema Alexis H., miaka 18. “Baba yangu hupenda kwenda kwenye magofu tofauti ambapo Paulo alifundisha na angeshiriki andiko au kutusimulia hadithi kuhusu wapi tukio lilitendeka.

Kama vile Paulo alivyopata changamoto katika siku zake, vijana wa Ugiriki pia wanakabiliana na masuala ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi. Mikutano ya vijana na kambi ya Wasichana havitokei kwa wingi huko Ugiriki, na hata kuhudhuria seminari kunaweza kuwa vigumu sana. Licha ya hizi na changamoto zingine, vijana wa Ugiriki hufanyia mazoezi maneno ya kutia moyo ya Paulo ya “kusimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili” (Wafilipi 1:27).

Kuishi Ugiriki humaanisha waumini hawa vijana wanapata kufurahia hali ya hewa ya joto, fukwe, chakula, na dansi. Pia wao hufurahia sana kukutana pamoja wao kwa wao. Pale wanapokutana katika seminari na shughuli za tawi, wamekuwa imara katika imani na urafiki.

Seminari katika Kilima cha Maazi

Picha
Seminary students

Kundi la seminari mbele ya jumba lla mkutano a Atheni.

Picha kwa hisani ya Leeann Heder

Wakati seminari ilipoanza Ugiriki miaka michache iliyopita, kulikuwa na wanafunzi watano tu. Walikutana asubuhi tatu kwa wiki, pamoja na wengine wakijiunga kupitia mkutano wa video wa mtandaoni. Wanakutana pia jumatano mchana kwa ajili ya seminari, ikifuatiwa na shughuli. Wamekuwa karibu na kila mmoja na kuwa nuru kwa rafiki zao, ambao wanauona mfano wao. Pale rafiki zao wanapouliza maswali, vijana wanawaleta seminari na kwenye Shughuli za pamoja.

Mvulana mmoja, Pavlos K., 15, anasema, “Kwenda seminari ni njia nzuri ya kuianza siku na hunisaidia kuwa imara. Kunaniweka katika hali ya mawazo ya kuwa mfano kwa wengine. Kunanisaidia kuanza siku nikitafakari kuhusu Yesu Kristo.”

Pale vijana wanapokua katika nguvu na umoja, baraka na fursa huja. Kwa mfano, mnamo 2017 walibarikiwa kuhudhuria Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana (KNV), mkutano mkubwa wa vijana wa kanda. Wasichana pia walishiriki kwenye Kambi yao ya kwanza kabisa ya Wasichana huko Ugiriki. Kama matokeo, wamekuwa karibu zaidi kama kundi, na wasichana wawili walijiunga na Kanisa.

Mkutano wa Kimataifa wa KNV

Picha
youth spelling out youth theme at FSY

Kwenye mkutano wa KNV, matamshi ya tahajia ya neno “Omba,” kutoka Yakobo 1:5

Mkutano, uliofanyika huko Ujerumani, uliwaleta pamoja vijana Watakatifu wa Siku za Mwisho kutoka Ulaya yote. Vijana kutoka Ugiriki na Cyprus walikuja kutoka mamia ya maili, na uzoefu wa mkutano ulikuwa na matokeo makubwa kwao. Kwa Maximos A., 14, “kitu cha kukumbukwa sana kwenye KNV ilikuwa ni pale tuliposhiriki shuhuda zetu. Kila mmoja alihisi Roho, na ilinipa msukumo wa kupata ushududa wangu mwenyewe.”

“Mwanzoni vijana wanne tu walikuwa waende,” anaongeza Loukia C., 15, “lakini mwishoni, tulikuwa na 15 waliohudhuria—rekodi ya Ugiriki—ikijumuisha 3 marafiki wasio waumini.”

“Ilikuwa ya kupendeza kuwa pamoja mahali fulani ambapo mnashiriki injili inayofanana na wewe si tofauti. Tulikuwa wote pamoja, na tulikuwa tukihisi Roho mmoja. Mambo haya yananisaidia.”

“Baba yangu si muumini na asingeniruhusu niende kwenye KNV au kubatizwa,” anasema Jesiana, 16. “Lakini waumini wa tawi walifunga kwa ajili yangu, na bibi yangu alizungumza na baba yangu. Baada ya hilo alisema ningeweza kwenda!”

Kwenye KNV, nilipitia uzoefu wa mara ya kwanza kwa wingi, kama vile, “kushiriki katika masomo na shughuli na kushiriki ushuhuda wangu kulinisaidia kuelewa vile ilivyo hasa kuhisi Roho Mtakatifu. Sikuwahi kumhisi Roho kama vile hapo mbeleni, na nilikuwa na furaha na kuvutiwa. Nilitoa ushuhuda wangu kwa mara ya kwanza.”

Picha
youth at FSY

Kwa kuongezea kwenye kushibishwa kiroho, vijana waliweza kupumzika na kuburudika pamoja kwenye mkutano. Haig T., 14, alikuja kwenye mkutano kutoka Cyprus. “Nilijifunza kuchangamana, kuwa na urafiki wa kweli, na kuburudika, hata katika nyakati ngumu.”

Kambi kwa Wasichana

Picha
young women at Marathon Greece

Wasichana kwenye Mbio za Masafa Marefu, Ugiriki.

Kambi ya Wasichana ilikuwa na matokeo ya kufanana. Wasichana kumi na wawili walikutana na viongozi wao karibu na eneo la kale la vita la Masafa Marefu. Walitumia siku tatu pamoja, wakijifunza kutegemeana kwa ajili ya nguvu na kujipa moyo.

“Nilipokuwa na miaka 12,” anasema Loukia, “nilikwenda kanisani kwa mara ya kwanza na nilikuwa mwenye furaha, lakini kisha niligundua kwamba nilikuwa peke yangu wa miaka 12. Sasa, miaka miwili baadaye, tuna wasichana wengi ambao kwa mara ya kwanza tuliweza kuwa na kambi ya Wasichana. Walipokutana pamoja, anasema, “niligundua kile inachomaanisha kuwa Mtakatifu wa Siku za Mwisho. Tunapoishi injili, nuru inatuzingira.”

Picha
young women holding flag

Kambi ya Wasichana, 2017—ya kwanza kabisa huko Ugiriki.

Kwa Bryana W., 15, KNV na kambi ya Wasichana vilimsaidia kuvunja ukimya na kuzungumza na wengine. “Familia yangu inahama mara kwa mara, na nilipata wakati mgumu kuwa karibu na wengine kwa sababu nilikuwa na aibu,” anasema. “Lakini kwa kuwa nilikuwa karibu na kundi letu kwenye KNV, nilipata marafiki wazuri. Wakati wa mkutano wa ushuhuda, tulishiriki hisia zetu, na nilitambua kwamba wengine walihisi sawa na vile nilivyohisi.”

Marie H., 17, anakumbuka dhamira ya kambi, “Maisha ni mbio za masafa marefu, siyo mbio fupi.” Wasichana na viongozi wao walijadili umuhimu wa kuvumilia na kumaliza mbio, anasema. “Ilinikumbusha kwamba ninaweza kuvumilia, kupiga hatua mwenyewe, na kubaki nimefokasi mwisho wa mstari. Kisha ninaweza kifikia mambo ambayo Baba wa Mbinguni ananitaka nifanye.”

Picha
young woman at girls camp

“Kutazama mawio ya jua kulileta roho wa utulivu, wa kupendeza.” —Lizzie T.

Mojawapo ya mambo ya kuvutia kambini ilikuwa ni mkutano wa ibada asubuhi wakati wa jua kuchomoza kwenye ufuko asubuhi yao ya mwisho. Lizzie T., 17, anasema, “Tulichukua maandiko yetu, tulikuwa na mkutano wa ibada, na kutazama machweo ya jua. Sote tulihisi upendo wa Mungu. Lilikuwa ni hitimisho la kupendeza kwa muda tuliotumia na kila mmoja wetu.”

Kuukabili Wakati Ujao Bila Woga

“Kutoka kwenye KNV na kambi ya Wasichana, nilijifunza mengi kuhusu injili na jinsi inavyoweza kunisaidia katika maisha yangu,” anasema Irini S., 17. “Nilipata marafiki wengi na kujifunza jinsi ilivyo muhimu kuelezea mawazo na hisia zangu. Nilihisi Roho Mtakatifu kwa kiasi kikubwa na upendo wa Mwokozi wetu, Yesu Kristo.”

Kuwa pamoja na vijana wengine Watakatifu wa Siku za Mwisho, anasema, kuliimarisha ujasiri wake. “Kabla ya KNV sikuweza kuona wema na mambo mazuri ambayo Mungu amefanya kwa ajili yetu na mipango ambayo Yeye bado anafanya kwa ajili yetu.”

“Hatupaswi kuathiriwa na yeyote au chochote kile kinachotuzunguka ambacho kitajaribu kutuvuta mbali kutoka kwenye kuishi injili,” Manasseh A., 17 anasema. “Injili inafanana kila mahali na tunapaswa daima kubaki kwenye njia sahihi.”

Na iwe ni Ugiriki au popote pale ulimwenguni, kushiriki njia hiyo pamoja kunaturuhusu kuwa wamoja katika roho.