2019
Mzee Bednar Anazuru India
Aprili 2019


Mitume kote Ulimwenguni

Mzee Bednar Anazuru India

Picha
Elder Bednar Visits India

Mzee David A. Bednar alisafiri na mke wake, Susan Bednar, ili kushiriki ushuhuda wa Yesu Kristo pamoja na waumini wa Kanisa huko India. India ni mojawapo ya nchi kubwa ulimwenguni. Na karibuni itakuwa na hekalu lake la kwanza!

Mzee na Dada Bednar walikwenda jiji la Rajahmundry. Mtume hajawahi kufika huko awali.

Watoto waliweza kusalimiana kwa mikono na Mzee Bednar.

Katika mkutano kwenye jiji la Hyderabad, msichana huyu alipata nafasi ya kumuuliza Mzee Bednar swali.

Kila mmoja alikuwa na furaha kusikia ushuhuda wa mtume wa Mungu!

“Kadiri kwa wingi ninavyosafiri ulimwenguni, ndivyo ninavyozuru mataifa mengi, ndivyo ninavyopata watu wengi zaidi ninaobarikiwa kujifunza kutoka kwao, ndivyo zaidi ninavyokuta kwamba ulimwenguni kote watu ni kama wanafanana.”

—Mzee David A. Bednar