2019
Uchaguzi: Kuwa Msanii Maarufu au Mama Maarufu?
Aprili 2019


Kidijitali Pekee

Uchaguzi: Kuwa Msanii Maarufu au Mama Maarufu?

Kila mtu aliniambia kuwa ilikuwa haiwezekani kuwa maarufu kwenye vyote viwili. Lakini ilikuwa kweli?

Ninakumbuka nikihisi kukosa raha nilipojifunza chuoni kuhusu maisha ya wasanii maarufu. Ilionekana kama wale wenye kukumbukwa na kusifika walikuwa wasanii maarufu kwa kutelekeza familia zao na kutoa mhanga utimamu wao. Wasanii maarufu walichora asubuhi ya Krismasi huku watoto wao wakifungua zawadi zao. Mmoja alifunga ndoa mara sita. Mwingine alikata sikio lake na kuwatumia wapendwa wake. Na mwingine hata alimuua mtu! Nilianza kujiuliza ikiwa kuwa msanii maarufu na wakati huo huo kuwa mke maarufu na mama (vyote wakati nikitunza kuendelea kutunza utimamuwangu!) kama kuliwezekana.

Wakufunzi wangu walifundisha kuwa kama tungetaka kuwa maarufu, tulipaswa kujitolea kwa ajili ya hilo. Tungepaswa kufanya kazi zaidi ya mtu yeyote yule. Tungepaswa kuweka mbele usanii katika maisha yetu. Akili yangu kila mara ingejiuliza, “Lakini ikiwa msanii alishika amri, kuweka vitu vya kwanza kwanza, na kuwa na Roho wa Bwana akielekeza kazi yao, je hawangeweza kuwa maarufu au hata maarufu zaidi? Swali hili lilikaa nami kipindi chote katika masomo yangu.

Kufikia wakati mimi na mume wangu tulipohitimu, tulikuwa kwenye ndoa kwa mwaka moja. Mzee Russell M. Nelson (kwa wakati huo, alikuwa mshiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili) alikuja kuongea kwenye sherehe yetu ya kuhitimu. Karamu ilifuatia, na wanafunzi 16 tu walialikwa kuhudhuria. Ajabu vya kutosha, wote mimi na mume wangu tulichaguliwa kuwa pale. Wakati majadiliano yalipofunguliwa kwa maswali na majibu. Niliinua mkono wangu, nikamtazama Mzee Nelson machoni, na kueleza wasiwasi wangu kuhusu kuwa vyote msanii na mama. Nilikuwa nimefanya kazi sana kukuza talanta zangu shuleni, na nilitaka kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuwa bora, lakini pia nilijua kuwa umama ulichukua kipaumbele. Je, kulikuwa na njia ya kufanya vyote? Macho ya Mzee Nelson yaling’aa alipojibu, “Bila shaka!” Alinihimiza kuboresha talanta zangu na kumwomba Baba wa Mbinguni usaidizi katika kufahamu jinsi gani ningeweza kufanya vyote na kwamba pamoja Naye, ningeweza kufanya mambo ambayo mwanzo nilifikiri hayakuwezekana. Nilichukua ushauri huo moyoni.

Kujitolea kwa Madhumuni Yake

Mume wangu na mimi sasa tuna watoto wanne. Tumejifunza changamoto za uzazi. Mwanzoni, mara nyingi nilianza siku saa 10.00 alfajiri kufanya michoro yangu kadhaa kabla ya watoto wangu kuamka. Nilijaribu kuchora siku sita kwa wiki, hata kama siku zingine ziliruhusu dakika 30 tu. Nilianza kila mchoro kwa sala, nikijua hapakuwa na mengi ambayo ningeweza kufanya bila usaidizi wa Bwana. Nilisali si tu kuwezeshwa kwenye usanii wangu lakini pia kujua kile kilicho muhimu zaidi siku hiyo na kujitolea kuweka madhumuni Yake mbele. Maendeleo hayakuwa ya haraka lakini yalikuwa imara.

Mbele miaka 12 toka siku ya kuhitimu kwangu. Nilikuwa na hali ya kuvunjika moyo. Maisha yalionekana kujaa. Umama ulikuwa zaidi ya kile nilichotarajia. Niliketi kwenye kiegemeza picha changu nikilia, nikijiuliza kama ningeweza kweli kuwa msanii maarufu niliyeota kuwa. Nilihisi msukumo kutoa shajara yangu kutoka kwenye rafu, na nikageukia maandishi ya Aprili 30, 2006, siku baada ya kuhitimu kwangu. Nilikuwa nimesahau kabisa uzoefu wangu wa ajabu na Rais Nelson! Kwa namna fulani kimbunga cha maisha kilikuwa karibu kuufuta kutoka kwenye kumbukumbu yangu. Pale mbele yangu yalikuwa maneno kutoka kwa nabii wa sasa “Bila shaka!” Machozi yakageuka kuwa ya shukrani nilipotazama nyuma kwenye yale yote niliyoweza kutimiza tangu wakati huo, na nikatazama mbele kwa matumaini.

Kufanya Kisichowezekana

Miezi michache baadaye, nilipata simu kutoka kwa wabunifu wa jarida la Ensign wakiuliza kama wangeweza kutumia mojawapo ya michoro yangu kwenye jalada la ndani la toleo la Mkutano Mkuu wa Novemba 2018. Nilishangaa! Nilipokuwa ninakua, jambo la kwanza ambalo nilikuwa nikifanya nilipopata majarida ya Kanisa ilikuwa ni kutafuta michoro. Sasa, mojawapo ya kazi zangu zingekuwepo mle ndani! Kisha, nilipoambiwa kuwa walitaka kuoanisha mchoro wangu na maneno kutoka kwa Rais Nelson, niliona mkono wa Bwana ukinitia moyo kwenda mbele.

Bado nina njia ndefu kwenye safari yangu ya usanii, lakini ninashukuru kwa matumaini ya Rais Nelson kwa Bwana na kwetu sisi. Ninashukuru kwa ajili ya mategemeo yake mema na kujiamini kwake. Ninajua kuwa tunapoonyesha imani katika Bwana tutaweza kufanya mambo makuu, hata mambo tuliyofikiria hayawezekani. “Hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.” (Luka 1:37).