2019
Manabii na Mitume Wetu
Aprili 2019


Manabii na Mitume wetu

Picha

Yesu Kristo anaongoza Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kupitia manabii na mitume. Soma kuhusu wao hapa chini. Kisha kata na uondoe picha kwenye ukurasa wa R23 na uzigandishe mahali pake katika chati. Weka gundi juu ya kila picha ili uweze kuziinua kwa ajili ya kusoma kweli zilizoko chini!

Rais Russell M. Nelson

Rais wa 17 wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho

  • Alikuwa daktari mpasuaji wa moyo

  • Alijifunza lugha nyingi, ikiwemo Kichina

  • Ana watoto kumi: 9 mabinti na 1 wa kiume

Rais Dallin H. Oaks

Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza

  • Alisafisha duka la ufundi redio kama kazi yake ya kwanza

  • Alikuwa mwanasheria na hakimu wa Juu wa Mahakama ya Utah

  • Alikuwa rais wa Chuo Kikuu cha Brigham Young

Rais Henry B. Eyring

Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza

  • Alicheza mpira wa kikapu akiwa shule ya upili

  • Alijifunza fizikia kutoka kwa baba yake kwenye ubao wa chaki wa familia yao

  • Alikuwa rais wa Chuo cha Ricks, sasa Chuo Kikuu cha Brigham Young–Idaho

Rais M. Russell Ballard

Kaimu Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili

  • Alipewa jina la utani la “askofu” alipokuwa chuoni kwa sababu ya viwango vyake vya juu

  • Alikuwa mfanyabiashara wa magari

  • Alitumikia kama mmisionari huko Uingereza na kama rais wa misheni huko Toronto, Kanada

Mzee Jeffrey R. Holland

Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili

  • Alikuwa mwenza mmisionari wa Mzee Cook huko Uingereza

  • Alifanya kazi kwenye Mfumo wa Elimu wa Kanisa

  • Alikuwa rais wa Chuo Kikuu cha Brigham Young

Mzee Dieter F. Uchtdorf

Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili

  • Alikuwa mkimbizi mara mbili alipokuwa mtoto

  • Alikuwa rubani wa ndege

  • Hufurahia kuteleza kwenye theluji na watoto wake pamoja na wajukuu

Mzee David A. Bednar

Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili

  • Alikuwa mlinzi kwenye timu yake ya mpira ya shule ya upili

  • Baada ya kutumikia misheni huko Ujerumani, alimbatiza baba yake kuwa muumini wa Kanisa

  • Alikuwa rais wa Chuo cha Ricks wakati kilipokuwa Chuo Kikuu cha Brigham Young–Idaho

Mzee Quentin L. Cook

Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili

  • Alipata ushuhuda baada ya kusoma maandiko na kuomba pamoja na kaka yake mkubwa

  • Alimwona mkewe mtarajiwa kwenye onyesho la vipaji katika shule ya upili.

  • Alitumikia kama kiongozi wa Kanisa huko Ufilipino na Visiwa vya Pasifiki

Mzee D. Todd Christofferson

Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili

  • Alioka mkate wa nyumbani kwa ajili ya familia yake changa

  • Alishiriki katika tamasha la Mlima Cumorah huko New York akiwa kijana aliyebalehe

  • Alifanya kazi kama mwanasheria kabla ya kuitwa kama Mtume

Mzee Neil L. Andersen

Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili

  • Alikulia katika shamba la kufugia ng’ombe huko Idaho, Marekani

  • Alitumikia kama mmisionari na rais wa misheni huko Ufaransa

  • Anazungumza Kifaransa, Kireno, Kihispania, na Kiingereza

Mzee Ronald A. Rasband

Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili

  • Alikuwa rais wa misheni huko New York, Marekani

  • Kauli mbiu yake ni “Ni watu ndio wenye umuhimu mkubwa”

  • Aliweka wakfu jengo la kwanza la Watakatifu wa Siku za Mwisho huko Jamhuri ya Cheki

Mzee Gary E. Stevenson

Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili

  • Alitumikia kama mmisionari na baadaye kama rais wa misheni ya Japani

  • Alianzisha biashara ya kutengeneza na kuuza vifaa vya mazoezi

  • Alitumikia kama askofu wa Kanisa lote

Mzee Dale G. Renlund

Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili

  • Jina lake la katikati, Gunnar, linamaanisha “askari shujaa”

  • Alihama na familia yake kutoka Utah kwenda Sweden alipokuwa na miaka 11

  • Alifanya kazi kama daktari wa moyo

Mzee Gerrit W. Gong

Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili

  • Anapenda wanyama, ikijumuisha pengwini

  • Hupenda kukutana na watu katika kila nchi

  • Ana rekodi ya historia ya familia inayorudi nyuma mpaka kwa Dragon Gong wa kwanza miaka 837 Baada ya Kristo.

Mzee Ulisses Soares

Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili

  • Anatokea Brazil na alitumikia kama mmisionari huko na kama rais wa misheni ya Urusi

  • Alijifunza kuhusu Kanisa pamoja na familia yake kama mvulana mdogo

  • Alianza kujiandaa kwa umisionari alipokuwa na miaka 12