2019
“Hivyo Ndivyo Ilivyo!”
Aprili 2019


“Hivyo Ndivyo Ilivyo!”

Richard J. Anderson

Utah, Marekani

Picha
man working on car

Kielelezo na John Kachik

Nilifika nyumbani nikiwa nimechelewa usiku mmoja wa majira ya baridi baada ya kufanya usahili mwingi kama askofu. Nilikuwa nimechoka. Kazi ilikuwa na uzito mkubwa kwa wiki kadhaa, na familia na majukumu ya Kanisa vilinifanya nihisi kujinyoosha kupita kikomo changu.

Jioni ile, ilinibidi kurekebisha gari yangu ili niweze kufika kazini asubuhi iliyofuata. Nilipovaa nguo zangu za kazi, nilibadilisha majukumu kutoka kuwa askofu na kuwa makanika. Nililala juu ya sakafu ya baridi ya gereji chini ya gari na kuanza kazi. Kwa nini ilikuwanipate baridi, uchovu, na kuvunja konzi zangu baada ya kuwa tayari nimefanya kazi kwa bidii siku hiyo? Nilikuwa nikipoteza subira yangu na kuanza sala ya kulia, kumsihi Baba wa Mbinguni.

“Je, inawezekana Ungeweza kunisaidia kidogo?” nilisema. “Ninajaribu kila niwezalo kuwa baba, mume, na askofu mwema na kuishi kulingana na amri. Je, nisingeweza kuhudumu vizuri zaidi ikiwa ningepata mapumziko kidogo? Tafadhali nisaidie nifanikishe hili ili niende kulala.”

Ghafla, maneno matatu dhahiri, ya kipekee yalikuja kwa ushujaa kwenye akili yangu: “Hivyo ndivyo ilivyo!”

“Nini?” Nilijibu.

Maneno yalikuja tena: “Hivyo Ndivyo Ilivyo!”

Uelewa ulianza kuijaza akili na moyo wangu wakati maneno yalipokuja kwa mara ya tatu: “Hivyo ndivyo ilivyo!” Maneno yalipeleka ujumbe kwenye moyo wangu. “Yalikuwa” ni maisha ya dunia, na nilikuwa nikipitia muda wa ukuaji uliokusudiwa kunisaidia mimi kuwa kile Baba wa Mbinguni anataka niwe. Ilikuwa ni kama Roho aliniambia, “Je, ulitegemea safari hii ya dunia kutokuwa na mahangaiko?” Niliponyanyuka kutoka kwenye ile sakafu ngumu ya baridi, sikuwa vilevile.

Kutegemeana na jinsi tunavyoitikia, majaribu yanaweza kuonekana kama zawadi kutoka kwa Baba wa Mbinguni mwenye upendo. Anatupatia fursa ya kupata majaribu ili tuweze kujifunza kumgeukia. Tunapofanya hivyo, tunabarikiwa kwa ukuaji wa kujifunza na kiroho.

Maneno matatu yaliyokuja akilini mwangu usiku ule wenye baridi juu ya sakafu ngumu ya gereji yangu yamenibariki kwa zaidi ya miaka 35. Najaribu kwa bidii kuona kwamba hakuna jaribu lisilofaa. Ninaona majaribu kama fursa za kujifunza mambo ambayo nisingeweza kujifunza kwa njia nyingine yoyote.