2019
Hadithi ya Pasaka
Aprili 2019


Hadithi za Maandiko

Hadithi ya Pasaka

Picha
Picha
Picha

Yesu aliwapenda rafiki Zake. Yeye aliosha miguu yao. Kisha Aliwapa sakramenti. Aliwaambia wamkumbuke Yeye. Aliwaambia wapendane.

Baadaye, Yesu alikwenda Bustanini. Aliomba kwa ajili yetu sote. Alihisi maumivu ya magonjwa yetu. Alihisi maumivu ya dhambi zetu.

Watu wenye hasira walimchukua Yesu. Walimuumiza. Alikufa msalabani kwa ajili yetu. Rafiki Zake waliuweka mwili Wake katika kaburi.

Siku tatu baadaye, rafiki Zake walirudi. Kaburi lilikuwa tupu! Malaika waliwaambia, “Amefufuka.” Yesu alikuwa hai tena! Kwa sababu ya Yesu, sisi sote tutaishi baada ya kufa.

Yesu ananipenda. Ninaweza kuifanya Pasaka kuwa maalumu kwa kumkumbuka Yeye. ●