2019
Ninaporudi Kwake
Aprili 2019


Nikirudi Kwake

Kwa upendo = 90

Picha
When I Return to Him

1. Mchunga hupenda kondoo wake wadogo,

Na wakipotea,

Yeye huwatafuta pale wanapotanga tanga;

Huwaita kila mmoja kwa jina.

Wanasikiliza sauti ya Mchungaji;

Wanamkimbilia Yeye, na kisha

Naye huwakaribisha kwa mikono ya upendo

Wanaporudi Kwake.

2. Mwokozi huwapenda watoto Wake wadogo,

Na kama nikienda mbali Naye,

Yeye hunitafuta pale ninapotanga tanga

Mchana au usiku wa giza.

Nitasikiliza sauti ya Mwokozi.

Nitaenda Kwake, na kisha

Atanikaribisha kwa mikono ya upendo

Ninaporudi Kwake.

3. Mwokozi hunionyesha njia;

Hunionyesha jinsi ya kuishi.

Na kama nikipotea au kutanga tanga,

Najua Yeye atasamehe.

Hivyo nitasikiliza sauti ya Mwokozi;

Nitatubu dhambi,

Na Yeye atajaza moyo wangu kwa shangwe

Ninaporudi Kwake.