2019
Vijana
Aprili 2019


Vijana

Picha
Nyame S.

Mara ya kwanza nilipoenda kwenye shule ya upili, kuna jambo moja nilihangaika nalo: pale somo jipya lilipotambulishwa, nilipata ugumu kuelewa. Jioni moja niliomba kwa Baba wa Mbinguni anisaidie nielewe na kushinda changamoto ile. Nilikuwa na imani, na niliweza kuelewa vizuri zaidi. Tangu hapo, sala na imani vimekuwa kwenye orodha yangu ya mambo ya kufanya shuleni na kila mahali ninapokwenda. Kuwa katika shule ya wavulana kuna changamoto kwa sababu ya baadhi ya mambo yaliyo kinyume na maadili ambayo wanafunzi hufanya. Hilo linapotokea, maneno ya wazazi wangu huja akilini mwangu: “Usifanye jambo ambalo litamfukuza Roho Mtakatifu.” Nina shukrani kwa ajili ya mama yangu, ambaye daima hunikumbusha kumsikiliza Roho Mtakatifu. Tunapofanya kile kilicho chema, Mungu hutubariki.

Nyame S., miaka 16, Ghana