2019
Katika nyakati za Kuvunjika Moyo, Mkumbuke Mjane wa Naini
Aprili 2019


Katika nyakati za Kuvunjika Moyo, Mkumbuke Mjane wa Naini

Hasa tunapohisi kusahaulika au kutoonekana, lazima tukumbuke: Yesu alikuja kumsaidia mjane wakati uleule alipokuwa na hitaji, na Yeye atakuja kwetu vilevile.

Picha
the widow of Nain

Wakati mwingine katika kupanda na kushuka kwa maisha, tunaweza kuhisi kwamba Mungu hajishughulishi katika maisha yetu ya kila siku. Mipangilio yetu inaonekana kiasi ya kuchosha na ya kukinaisha. Hakuna mabadiliko mengi, na wakati mwingine ni vigumu kuonyesha eneo moja ambapo Mungu moja kwa moja ameingilia katika hali zetu. Wakati wowote ninaposhtushwa na hisia hizi za kutokuwa muhimu katika maisha yangu mwenyewe, mara nyingi namfikiria mwanamke katika Agano Jipya ambaye yawezekana alihisi hivi. Hakutajwa katika maandiko lakini anajulikana kirahisi kwa jina la kijiji chake na kwa wasifu wake wa ndoa.

Mwanamke ni mjane wa Naini, na ndiye mwinjilisti Luka tu anayeandika hadithi yake ya kupendeza. Kwangu mimi anawakilisha kiini cha huduma binafsi ya Mwokozi na jinsi Yeye alivyowafikia waliovunjika moyo, watu wa kawaida wa jamii Yake. Tukio hili kwa sauti linakamilisha suala kuhusu ikiwa Mungu anatufahamu na kutujali.

Muhtasari mfupi wa muujiza kutoka Luka sura ya 7 unafafanua Yesu akizuia maandamano ya mazishi na kimiujiza akimrejesha kijana aliyekufa kwenye uzima. Lakini kuna mengi zaidi ya kuelewa kuhusu mazingira. Kama ilivyo kwa miujiza yote, lakini hasa kwa huu, muktadha ni muhimu kuelewa tukio hili. Nikiwa nimefundisha Chuo Kikuu cha Brigham Young Kituo cha Yerusalemu, nitashiriki nanyi baadhi ya utambuzi binafsi kuhusu muujiza huu.

Naini ilikuwa ni kijiji kidogo cha wakulima wakati wa Yesu, kikijikumbatiza kati ya Mlima More, ambao unaelezea upande wa mashariki wa Bonde la Yezreli. Mji wenyewe ulikuwa nje ya njia iliyotumika mara kwa mara. Ufikiaji wake ulikuwa kwa kupitia njia moja tu. Wakati wa kipindi cha Yesu, makazi haya yangekuwa madogo na masikini kiasi, na yamebaki hivyo tangu awali. Nyakati zingine katika historia yake, mji huu umezungukwa na nyumba chache kama 34 na watu 189 tu.1 Leo ni makazi ya takribani wakazi 1,500.

Luka anaanza maelezo yake kwa kukumbusha kwamba Yesu alikuwa Kapernaumu siku moja kabla na alimponya mtumwa wa Akida (ona Luka 7:1–10). Kisha tunajifunza kwamba “siku moja baadaye” (mstari wa 11; msisitizo umeongezwa), Mwokozi alienda kwenye mji ulioitwa Naini, akisindikizwa na kundi kubwa la wafuasi. Mpangilio ni wa muhimu sana. Kapernaumu iko katika ufuko wa kaskazini wa Bahari ya Galilaya, futi 600 (m. 183) chini ya usawa wa bahari. Naini ni kama maili 30 (km 48) kusini magharibi mwa Kaprenaumu kwenye futi 700 (m.213) juu ya usawa wa bahari, hivyo kuhitaji nguvu, kupanda juu ya kilima kwenda Naini. Ili kutembea kutoka Kapernaumu kwenda Naini, ingechukua angalau siku moja au mbili. Hivi karibuni iliwachukua kundi la wanafunzi vijana wa Chuo Kikuu cha Brigham Young Kituo cha Yerusalemu masaa 10 kutembea safari hii kwenye njia za lami. Hii inamaanisha kwamba pengine Yesu aliamka mapema sana au yawezekana alitembea wakati wa usiku ili aweze kuzuia maandamano ya mazishi “siku moja baadaye.”2

Picha
map of Galilee

Yesu alipoukaribia mji baada ya safari ya kuchosha, kijana yawezekana alikuwa kwenye miaka 203 alikuwa amebebwa kwenye kitanda cha mazishi. Luka anatuambia kwamba kijana huyu alikuwa mwana pekee wa mjane, na baadhi ya wanazuoni wanatafsiri maneno ya Kigiriki kumaanisha kwamba hakuwa na mtoto mwingine.4 Kundi kubwa la wanakijiji walimsindikiza katika janga hili baya la kifamilia.

Kwa kawaida, kufiwa mwana kungekuwa ni janga kwa yeyote, lakini fikiria kidokezi cha mjane huyu. Ingeweza kumaanisha nini kijamii, kiroho, na kifedha kuwa mjane bila ya mrithi katika Israeli ya kale? Katika utamaduni wa Agano la Kale, iliaminika kuwa wakati mume alipokufa kabla ya uzee, ilikuwa ishara ya hukumu ya Mungu kwa ajili ya dhambi. Hivyo, baadhi waliamini kwamba Mungu alikuwa akitoa adhabu juu ya huyu mjane aliyenusurika. Katika kitabu cha Ruthu, wakati Naomi alipoachwa mjane katika umri mdogo, aliomboleza, “Bwana amenirudisha sina kitu, na Mwenyezi Mungu amenitesa (Ruthu 1:21, Tafsiri ya Kiwango cha Kimataifa).5

Siyo tu kulikuwa na maumivu ya kiroho na kihisia, lakini mjane huyu wa Naini alikuwa pia akikabiliwa na ukata wa fedha—hata kuonyesha njaa usoni.6 Baada ya ndoa, mwanamke alikabidhiwa kwa familia ya mumewe kwa ajili ya ulinzi wa kifedha. Kama mume angekufa, basi utunzaji wake ungekabidhiwa kwa mwanawe wa kuzaa. Sasa wakati mwana wa kuzaa na wa pekee wa mjane huyu alikuwa amekufa, alikuwa mwishoni mwa kamba yake kifedha. Kama mwanawe alikuwa kwenye miaka 20, yawezekana mjane huyu alikuwa mwanamke wa umri wa kati, akiishi katika mji mdogo, wa mashamba yaliyojitenga, na sasa alijikuta fukara kiroho, kijamii na kifedha.

Picha
widow of Nain with the Savior

Kwa usahihi kwenye dirisha jembamba la wakati ambapo wanakijiji walikuwa wamembeba mwana wa mjane huyu ili kumzika, Yesu alikutana na maandamano na alikuwa na “huruma juu yake” (Luka 7:13). Kwa kweli, haya yaweza kuwa maelezo pungufu sana ya Luka. Yesu kwa kiasi fulani alihisi hali ya ufukara wote wa mjane huyu. Pengine alitumia usiku akijibwaga kwenye sakafu yake ya udongo, akimsihi Baba wa Mbinguni kujua sababu. Pengine aliuliza wazi wazi kwa nini Baba wa Mbinguni alimtaka awe na maisha marefu katika dunia hii. Au pengine alikuwa na hofu ya upweke uliobaki ambao angeupata. Sisi hatujui. Lakini tunajua ya kwamba Mwokozi alichagua kuondoka Kapernaumu haraka, ambapo ilimhitaji Yeye kutembea usiku ili kuzuia maandamano ya mazishi muda muafaka kabla hawajauweka mwili ardhini.

Ndiyo, alipoona uso wake uliojaa machozi wakati akitembea nyuma ya maandamano, Yesu alihisi huruma tele kwa mwanamke huyu—lakini inaonekana kwamba huruma Yake ilikuja kutokana na hisia Yeye alizopata muda mrefu kabla ya Yeye “kutokea” kuzuia msafara ule wa mazishi. Aliwasili pale wakati muafaka wa mahitaji yake.

Yesu kisha alimwambia mjane “usilie” (mstari wa 13). Bila kuwa na woga wa kutoheshimu tambiko, “Aligusa jeneza,” na maandamano “yakasimama.” Kisha Akaamuru, “Kijana, Nakuamuru, Amka.

Picha
widow with son

“Yule maiti akaketi, na akaanza kusema. Na [Yesu] akampa mama yake” (mistari 14–15). Kiuhalisia, umati wa wanakijiji na wafuasi wa Yesu waliingiwa na hofu pale huzuni yao ya pamoja ilipobadilika kuwa shangwe halisi. Wote “wakamtukuza Mungu, wakisema, nabii mkuu ametokea kwetu” (mstari wa 16). Lakini muujiza huu ulikuwa pia kuhusu kuiokoa nafsi moja iliyokata tamaa. Yesu alijua kwamba kuna kitu hakikuwa sawa kabisa kwa mwanamke huyu—mtu ambaye alidharauliwa katika utamaduni wao. Hali yake ilihitaji umakini Wake wa haraka, hata kama ingembidi kusafiri mbali kuwepo pale kwa uangalifu kwa wakati muafaka. Alijua hali yake ya kukata tamaa, na Alikuja haraka. Rais Thomas S. Monson (1927–2018) alizungumzia ukweli usiopingika aliposema, “Siku moja, tutakapoangalia nyuma kwenye vile vilivyokuwa vinaonekana kama bahati katika maisha yetu, tutatambua kuwa labda havikuwa bahati kabisa.”7

Sasa, kama tukio hili lilivyo la kuinua, ni lazima liwe zaidi ya hadithi nzuri ya Biblia kwetu. Linathibitisha pasipo makosa kwamba Yesu alijua kuhusu mjane huyu masikini, aliyesahaulika, na fukara. Hasa tunapohisi kusahaulika au kutoonekana au tusio na thamani, lazima tukumbuke: Yesu alikuja kwa mjane katika wakati wake wa uhitaji mkubwa, na Yeye atakuja kwetu vilevile. Kwa kuongezea, somo la pili tunaloweza kupata kutokana na mfano wa Mwokozi ni umuhimu wa kunyoosha mkono kuwabariki wengine wanaotuzunguka. Wengi ndani ya mduara wako watakuwa wamevunjika moyo kwa nyakati tofauti. Ikiwa unaweza kuwaambia kuhusu “Dada Naini” na jinsi Bwana alivyojua kwa hakika kuvunjika kwake moyo na janga lake kuu la binafsi, ingeweza kubadilisha usiku kuwa mchana. Kumbuka ugunduzi wenye hisia kali wa Rais Spencer W. Kimball (1895–1985): “Mungu anatuona, na anatuchunga. Lakini mara nyingi ni kwa kupitia mtu mwingine kwamba anakidhi mahitaji yetu.”8

Picha
widow hugging her son

Kati ya miujiza yote ya Yesu wakati wa muda Wake duniani, kwangu mimi, michache ni ororo na yenye huruma kama kuhudumu Kwake kwa mjane wa Naini. Unatukumbusha kwamba tuna thamani Kwake na kwamba kamwe Yeye hatatusahau. Hatuwezi kusahau hilo.

Muhtasari

  1. Ona E. Mills, Census of Palestine 1931: Population of Villages, Towns, and Administrative Areas (1932), 75.

  2. Ona S.Kent Brown, The Testimony of Luke (2015), 364.

  3. Ona Brown, The Testimony of Luke, 365.

  4. Ona Brown, The Testimony of Luke, 365.

  5. Katika Isaya 54:4 Bwana anamwambia mjane Israeli kuwa “mashutumu ya ujane wako hutayakumbuka tena” (Tafsiri Mpya ya Kiingereza).

  6. Ona Brown, The Testimony of Luke, 365.

  7. Thomas S. Monson, katika Joseph B. Wirthlin, “Masomo Niliyojifunza katika Safari ya Maisha,” Liahona, Mei 2001, 38.

  8. Teachings of Presidents of the Church: Spencer W. Kimball (2006), 82.