2019
Sehemu Mpya ya Watoto ya Liahona
Aprili 2019


Kidijitali Pekee

Sehemu mpya ya Watoto ya Liahona

Kuanzia 2019, kurasa za watoto za Liahona zimebadilika kwa njia tatu kuu:

  • Sehemu iliyosimama pekee. Sasa watoto watapata kufikia hadithi za kujenga imani na shughuli kwenye kurasa za watoto zinazoitwa Rafiki. Liahona itaendelea kuleta makala ya watu wazima, vijana wazima na vijana.

  • Kurasa zaidi. Mwongezeko kutoka kurasa 14 hadi 24 inamaanisha hadithi, shughuli, na mawazo zaidi za kuwafundisha watoto nyumbani na kwenye msingi. (Mawazo ya kufundishia yameainishwa na nyenzo mpya za Njoo Unifuate.)

  • Karatasi Mpya. Karatasi hii mpya ni rahisi kukata, kuweka rangi au kuchora.

Rafiki itajumuishwa kwenye Liahona bila malipo zaidi na itasafirishwa pamoja na jarida. Kwa wakati huu, Rafiki haiwezi kuagizwa peke yake.

Kila mtu anayepokea Liahona anaweza kuwa na nafasi ya kuwapa watoto kufikia Rafiki. Wale wasio na mtoto nyumbani, wanaweza kumpa mjukuu, rafiki au jirani, au mwalimu wa msingi ambaye anaweza kumpa mtoto kwenye kata au tawi.

Ili kuagiza au kulipia au kumpa mwingine kama zawadi nenda kwenye store.lds.org, wasiliana na kituo chako cha usambazaji au karani wa kata au tawi lako.

Acha Liahona kufahamu jinsi unavyotumia Rafiki mpya nyumbani na kanisani kwa kuandika barua pepe kwa liahona@ldschurch.org.