2020
Njia Zaidi ya Moja za Kujifunza Maandiko
Oktoba 2020


Kidijitali Pekee: Vijana Wakubwa

Njia Zaidi ya Moja za Kujifunza Maandiko

Hata kama hupendi kusoma, kuna njia nyingi za kujifunza maandiko.

Ninapenda wito wangu wa sasa kama mpiga kinanda wa Msingi. Wiki chache zilizopita watoto walikuwa wakifanya mazoezi ya wimbo. Nilihisi Roho wakati walipoimba:

Tafuta, tafakari, na omba

Ni vitu ambavyo lazima nivifanye.

Roho ataongoza, na, ndani kabisa,

Nitajua maandiko ni ya kweli.1

Lakini swali pia liliingia ndani ya kichwa changu. Vipi ikiwa—kama aya ya kwanza ya wimbo inavyopendekeza—“hupendi kusoma maandiko matakatifu”? Nadhani mada ya usomaji imekuwa kwenye akili yangu hivi karibuni kwa sababu rafiki zaidi ya mmoja ameshiriki kwamba wanapambana na shida ya kusoma. Na watu wengi ninaowajua hawafurahii kusoma! Je, kuna njia ambayo kwayo bado wanaweza kuwa na uzoefu mzuri wa maandiko na kukuza “ushuhuda kwamba ni ya kweli”?

Watu wanaonekana kujifunza vizuri zaidi wakati taarifa inapowasilishwa kwa njia nyingi tofauti, kama vile kwa kuona na kwa maneno, na masomo yanarudiwa baada ya muda. Kwa kuzingatia hilo, nilijaribu kufikiria njia nyingi tofauti za kusoma maandiko kadiri ambavyo ningeweza. Sasa, kwa ruhusa, si kila kitu kwenye orodha hii kingeweza kuhesabika kama kujifunza maandiko kwa kutafakari na kwa kina ambako manabii wamefundisha kwamba ni muhimu kwenye shuhuda zetu—baadhi ya hivi ni mawazo ya haraka, ya kuburudisha—lakini nimegundua vinaweza angalau kuchochea mawazo mapya ya kwako mwenyewe. Acha tutoe juhudi zetu kubwa kwenye kujifunza injili ili tuweze, kama wimbo unavyosema, “kufikia uelewa” pamoja!

Mawazo ya Kujifunza Maandiko

  1. Tambua maneno ambayo yamerudiwa katika baraka zako za patriaki na utafute maneno sawa na hayo kwenye maandiko.

  2. Unapokuwa ukisoma, chora picha kuhusu mawazo yako katika shajara ya kujifunzia au pembezoni mwa kitabu chako cha kiada cha Njoo, Unifuate.

  3. Jenga kielelezo kidogo cha hadithi ya maandiko.

  4. Piga simu kwa ndugu aliye mbali na msome pamoja kwa simu.

  5. Andika orodha ya maswali uliyonayo kwa Mungu na kisha utafute majibu unaposoma.

  6. Angalia video kutoka BookofMormonVideos.org au BibleVideos.org.

  7. Fungua maandiko kwenye sura yoyote na uanze kusoma.

  8. Imba wimbo wa kanisa na kisha angalia maandiko yaliyoorodheshwa mwishoni mwa wimbo.

  9. Tembelea topics.ChurchofJesusChrist.org na soma kitu kinachokupendeza.

  10. Angalia picha ya sanaa mtandaoni inayooelezea hadithi ya maandiko unayosoma.

  11. Soma tu vichwa vya habari vya sura na sehemu vya kitabu.

  12. Piga muziki wa kupendeza wakati ukisoma kwa sauti.

  13. Tafuta njia ambazo kila sura ya maandiko inahusiana na hekalu.

  14. Ikiwa kwa kawaida unasoma maandiko ya kidijitali, jaribu kusoma nakala zilizochapishwa, au kinyume chake.

  15. Paka rangi au chora eneo la tukio au hadithi.

  16. Jifanye kama umepewa jukumu la kuzungumza juu ya mada kanisani, na ujifunze kwa ajili ya hilo.

  17. Baada ya kusoma sura ya maandiko unayoipenda, iandike tena kwa maneno yako mwenyewe.

  18. Fuata maelezo ya tanbihi chini ya ukurasa katika mstari unaoupenda, halafu fuata maelezo ya tanbihi chini ya ukurasa katika mistari uliyoelekezwa kwayo, halafu fuata maelezo hayo ya tanbihi chini ya ukurasa, n.k.

  19. Badilishaneni kusoma mistari kwa sauti na marafiki na kuzungumza juu ya kile mnachosoma.

  20. Tumia Mwongozo wa Mada kujifunza neno moja au mada moja.

  21. Angalia maandiko yote katika maelezo mwishoni mwa mahubiri ya mkutano mkuu.

  22. Weka andiko mahali unapoliona kila siku na jaribu kulikariri wiki hii.

  23. Andika kadi kwa watu pamoja na maandiko ya kufariji yaliyoandikwa ndani.

  24. Tumia Maktaba ya Injili kusikiliza maandiko yanaposomwa kwa sauti kubwa.

  25. Chora ratiba ya matukio wakati unaposoma Kitabu cha Mormoni.

  26. Tafuta “rafiki wa maandiko” na andikianeni arafa ya mstari kila asubuhi.

  27. Anza kutoka sura ya mwisho ya Kitabu cha Mormoni na usome mpaka mwanzo.

  28. Soma maandiko ambayo yanajumuisha ushuhuda, kisha andika ushuhuda wako.

  29. Ikiwa unapiga chombo cha muziki, jaribu kuandika wimbo ambao unabeba hisia za mstari.

  30. Uliza wanafamilia au marafiki kuhusu vifungu vyao vya maandiko wanavyovipenda.

  31. Unaposoma, chora vitu vilivyoelezewa, kama upinde uliovunjika wa Nefi.

  32. Soma na kariri mistari inayotumika kufundisha masomo ya umisionari, yanayopatikana katika sura ya tatu ya Preach My Gospel.

  33. Soma kitabu kutoka katika Biblia ambacho hujawahi kukisoma kabla.

  34. Chunguza maisha ya shujaa wa maandiko na uandike ripoti ya wasifu.

  35. Igiza hadithi ya maandiko kama sehemu ya jioni ya nyumbani au shughuli nyingine ya Kanisa.

  36. Tafuta nukuu kutoka kwa kiongozi wa Kanisa kwenda sambamba na kila sura unayomaliza.

  37. Soma visaidizi vya usomaji wa maandiko, kama Dibaji ya Kitabu cha Mormoni au Kamusi ya Biblia.

  38. Tumia muda wako katika mazingira ya asili na fikiria kuhusu jinsi kile unachokiona kinavyohusiana na injili, kisha tafuta mstari kuhusu kile ulichojifunza.

Una maoni yako mwenyewe? Yashiriki na marafiki zako!

Muhtasari

  1. “Tafuta, tafakari, na omba,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 109.