2020
Yeye Bado Ni Wetu
Oktoba 2020


Yeye Bado Ni Wetu

Mume wangu na mimi tulikuwa tunakwenda kuunganishwa, lakini ibada hii takatifu ilikuwa ni kubwa zaidi kuliko sisi wawili.

Picha
photo of baby and temple

Kielelezo na Joshua Dennis

Baada ya miaka saba ya matumaini na kusubiri kupata watoto, mume wangu na mimi hatimaye tulibarikiwa kumpata binti. Alicie alikuwa ni nuru ya maisha yetu, lakini aliishi kwa miezi mitano pekee kabla ya kufa kwa ugonjwa wa kichomi.

Hili lilikuwa tukio gumu sana katika maisha yangu. Kila siku nilirudi nyumbani kutoka kazini na kukaa na kulia. Shemeji zangu mara nyingi walikaa nami ili kunipa nguvu. Niliendelea kuomba kwa ajili ya mtoto mwingine, lakini hakuna aliyekuja. Nilikuwa nimepotea katika huzuni.

Shemeji zangu walianza kutuhimiza mimi na mume wangu twende kwenye Hekalu la Suva Fiji ili kuunganishwa. Hatukuwahi kwenda hekaluni, na tuliamua kwamba hii itakuwa ni njia nzuri kwetu ya kutafuta matumaini na uponyaji.

Hakuna ambacho kingeniandaa mimi kwa kile nilichojisikia siku ile! Nilijua kuwa mimi na mume wangu tungeunganishwa pamoja milele. Elimu hii ilinijaza shukrani na upendo. Lakini sikuelewa kwamba ibada hii takatifu ilikuwa ni kubwa zaidi kuliko sisi wawili.

Hekaluni nilijifunza kwamba Alicie angeweza kuunganishwa na sisi. Nililia machozi ya furaha nilipokuja kujua mafundisho haya matakatifu. Binti yetu atakuwa wetu milele yote. Ninashuhudia kwamba Mungu ametupa kila kitu tunachohitaji kwa ajili ya furaha katika nyumba Yake takatifu.

Tokea miaka hiyo, mume wangu na mimi tumebarikiwa mtoto wa kiume na watoto watatu tulio waasili. Bado hatuwezi kamwe kumsahau Alicie. Kwa sababu ya ibada za hekalu, binti yetu ni sehemu ya familia yetu milele.

Ninapokutana na mtu aliyepoteza mtoto, ninahisi maumivu yao. Lakini pia ninaelewa kuwa maumivu haya siyo mwisho. Kupitia kumpoteza Alicie, na pia kwa kuyapitia majaribu mengine, ninajua kuwa Mungu yupo kwa ajili yangu. Wakati ninapovunjika moyo au kulalamika juu ya vitu, ninajua kuwa Mungu daima yupo pale.

Ninajua nitamwona tena Alicie, na kwamba ukweli unaendelea kumjaa mume wangu na mimi pamoja na shangwe tele.