2020
Mwite Baba
Oktoba 2020


Mwite Baba

Kama nitaendesha kwa nguvu, Yu alifikiria, naweza kufika nyumbani kabla ya mitaa kufurika.

“Changamkeni, kwa kuwa nitawaongoza” (Mafundisho na Maagano 78:18).

Picha
Call Dad

Yu alitoka nje ya shule iliyosongamana kwenda njia ya watembea kwa miguu. Kichwa chake kilikuwa kimejaa ukweli wa hesabu kutoka darasa lake la baada ya shule. Watu waliharakisha na miamvuli. Mabonge manene ya mvua yalikuwa yakianguka kwa kasi, na mtaa ulikuwa umejaa maji.

Rafiki yake Yu, Lin, alitoka nje karibu yake. “Unapaswa kumwita baba yako aje kukuchua,” Lin alisema. “Bwana Zhang anasema kuna mafuriko katika baadhi ya sehemu za mji.”

“Ninaweza kufika nyumbani mimi mwenyewe.”

“Lakini angalia hayo maji yote!” Lin alisema, akionyesha maji yakitiririka kwa kasi katika mfereji.

Kwa muda mfupi, Yu alikuwa na hisia za ucheshi. Je, Lin alikuwa sahihi? Huenda anapaswa kumwita Baba ili amchukue kwenda nyumbani kabla mitaa haijafurika maji. Lakini yeye na Baba walikuwa na malumbano jana usiku, na Yu alikuwa bado na hasira. Hakutaka kumwomba Baba msaada.

Yu aliifungua baiskeli yake na kusema kwaheri kwa Lin. Kama nitaendesha kwa nguvu, yeye alifikiria, naweza kufika nyumbani kabla mitaa haijafurika.

Aliendesha kwa bidii, lakini punde mikono yake ilikuwa baridi, nguo zake zilikuwa zimelowa, na alikuwa amechoka. Kwa mara nyingine, wazo likamjia la kumwita Baba. Je hisia zilikuwa zimetoka kwa Roho Mtakatifu? Wamisionari waliokuwa wamembatiza walisema kwamba Roho Mtakatifu angeweza kuwa mwongozo wake. Yu alitupa macho angani. Anga lilikuwa la kijivu sana kiasi kwamba hakuweza kuona juu ya majengo. Lakini bado alikuwa amemkasirikia Baba.

Yu alipuuzia hisia na kuendelea kuendesha. Maji yalizidi kujaa kwamba wenye maduka walifunga maduka yao. Watu walihamisha vitu vyao kwenda ghorofa za juu. Yu alimwona mama akiwasukuma watoto wake wawili kuvuka mafuriko katika boti ndogo ya plastiki.

Maji sasa yalivuka vifundo vya miguu yake, Yu hakuweza tena kuendesha baiskeli yake. Alishuka na kusukuma. Labda alikuwa amechelewa sana kumpigia Baba, na mvua ilikuwa bado ikinyesha. Ngurumo ziliongezeka na radi ikaangaza juu yake. Yu aliogopa. Na alikuwa amechoka sana! Aliangalia mbele. Nyumbani bado kulikuwa mbali. Hakupaswa kumpuuza Roho Mtakatifu kwa sababu ya hoja ya kijinga.

Yu alisimama ili kusema ombi fupi. Hakuweza kusikia sauti yake juu ya mvua na radi, lakini alijua kwamba Baba wa Mbinguni angeweza kumsikia.

“Baba wa Mbinguni,” Yu aliomba. “Tafadhali nisaidie nifike nyumbani salama.” Alipomaliza, alihisi nguvu ya kuendelea.

Mwishowe, Yu aliweza kuiona nyumba yake kwenye kilima. Akihisi baridi, kuchoka, na kwa namna fulani akiwa amepoteza kiatu, Yu alijikokota kupanda kilima. Alimwona Baba akimngojea nje. Baba alikimbia kushuka chini ya kilima kukutana naye, akirusha maji wakati akikimbia.

Wakati Baba alipomfikia, aliweka mikono yake kumzunguka Yu. “Nilikuwa na wasi wasi sana!” Baba alisema. “Ulipaswa kunipigia simu!”

“Nilidhani tumekasirikiana,” Yu alisema.

“Sijawahi kukasirika na kuacha kukusaidia,” Baba alisema. Kisha akaichukua baiskeli ya Yu na kuisukuma hadi mwisho wa kilima.

Hata ngurumo za radi zikilia kati ya majengo marefu na mvua kubwa ikianguka chini, hisia nzuri ilijaza moyo wa Yu. Alijisikia amani na usalama akiwa anamfuata Baba nyumbani. ●