2020
Ikiwa Wewe ni Mwathiriwa wa Unyanyasaji
Oktoba 2020


Ikiwa Wewe ni Mwathiriwa wa Unyanyasaji

Unyanyasaji ni Nini?

Unyanyasaji ni kutelekezwa au kutendewa vibaya na wengine (kama vile mtoto, mtu mzee, mtu mwenye ulemavu, au mtu mwingine yeyote) katika njia inayoleta madhara kimwili, kihisia au kijinsia. Unakwenda kinyume na mafundisho ya Mwokozi.

“Msimamo wa Kanisa ni kwamba unyanyasaji katika namna yoyote ile hauwezi kuvumilika” (General Handbook: Serving in The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints [2020], 38.6.2). Unyanyasaji unakiuka sheria za Mungu na pia unaweza kuwa ni ukiukaji wa sheria za jamii.

Aina Mbalimbali za Unyanyasaji

Unyanyasaji wa Kimwili: Tabia ya ukali au ya vurugu ya mtu mmoja kwa mwingine ambayo husababisha kuumia kwa mwili.

Unyanyasaji wa Kingono: Tendo la ngono lisilohitajika au mgusano, na wakosaji kutumia nguvu, kutoa vitisho, au kuchukua fursa kwa waathiriwa ambao hawawezi kutoa idhini. Matendo yote ya kingono kati ya mtu mzima na mtoto ni unyanyasaji bila kujali idhini.

Unyanyasaji wa Maneno na Kihisia: Mpangilio wa tabia ambao mtu mmoja na kwa makusudi anamshambulia mtu mwingine kwa njia zisizo za kawaida, kama vile maneno makali, vitisho, udanganyifu, au kudhalilisha. Hii husababisha hali ya kushuka kwa hali ya kujithamini na utu wa mtu. Ingawa sio ya kimwili, aina hii ya unyanyasaji inaumiza ustawi mzima wa akili ya mtu na hali ya kihisia.

Nawezaje Kupata Msaada

Bwana anatarajia sisi kufanya yote tuwezayo ili kuzuia unyanyasaji na kulinda na kuwasaidia wale ambao wamekuwa waathiriwa. Hakuna mtu yeyote anayetarajiwa kuvumilia tabia ya unyanyasaji. Ikiwa inatokea hivi sasa au ilitokea zamani sana, unaweza kupata nyenzo za kukusaidia katika abuse.ChurchofJesusChrist.org.