2020
Kushiriki Injili
Oktoba 2020


Kushiriki Injili

“Mjifunze kwangu … nanyi mtapata raha nafsini mwenu” (Mathayo 11:29).

Picha
Sharing the Gospel

Mtu niliyefanya kazi kwake alinipa nakala ya Kitabu cha Mormoni. Lakini sikukisoma kwa takribani miaka miwili. Jumapili moja, nilikichukua Kitabu cha Mormoni na kwenda kwenye njia ya reli nje ya mji ambako nilikuwa naishi huko Zimbabwe. Nilikaa chini na kuanza kusoma.

Mwanzoni, ilikuwa vigumu kuelewa. Lakini nilisoma ushuhuda wa Joseph Smith tena na tena. Maneno yake yaliugusa moyo wangu.

Baadaye, mtu mmoja alinialika kuja kanisani. Mwanzoni, nilikuwa na wasiwasi, kwa hivyo nilikaa kwenye safu ya nyuma. Lakini watu walipoanza kushiriki shuhuda zao juu ya Mwokozi Yesu Kristo na Kitabu cha Mormoni, nilihisi kitu cha ajabu ndani.

Sio muda mrefu baada ya hii, wamishonari walikuja mtaanii kwangu. Punde nilibatizwa. Miaka kadhaa baadaye, nilipata heshima ya kuhudumia misheni na kufundisha injili na wengine wengi.

Kanisa limekua sana Zimbabwe. Lakini bado kuna mengi tunayoweza kufanya ili kushiriki injili, bila kujali tunaishi wapi. Kupitia maombi, kusoma maandiko, na jioni ya nyumbani, unaweza kukuza ushuhuda wako na kukaa karibu na Baba wa Mbinguni. Ushuhuda wako unaweza kubariki maisha ya watu wengi duniani kote. ●