2020
Sakramenti na Mimi
Oktoba 2020


Kutoka kwa Urais wa Kwanza

Sakramenti na Mimi

Imechukuliwa kutoka “Mkutano wa Sakramenti na Sakramenti,” Liahona, Nov. 2008, 17-20.

Picha
The Sacrament and Me

Sakramenti ni sehemu muhimu sana ya mkutano wa sakramenti. Tunapopokea sakramenti, sisi tunaahidi daima kumkumbuka Mwokozi. Ili kuifanya sakramenti iwe maalum, tunatakiwa …

  • Kuvaa vizuri ili kuonyesha tunaiheshimu sakramenti.

  • Kukaa kimya kabla ya mkutano kuanza.

  • Kuimba wimbo wa sakramenti.

  • Kufikiria juu ya Yesu na kuahidi daima kumkumbuka Yeye.

Sakramenti inatusaidia kumsikia Roho Mtakatifu. Inatusaidia kukaa kwenye njia ya kurudi nyumbani kwetu mbinguni. ●

Kuonyesha Upendo kwa Yesu

Tunaweza kuonyesha upendo wetu kwa Yesu kwa kuwa na staha wakati wa sakramenti. Unafanya nini wakati wa sakramenti?

  • Naketi kimya.

  • Nafikiria wimbo wangu ninaoupenda wa sakramenti.

  • Nafikiria juu ya hadithi kuhusu Yesu.

  • Ninaomba kwa Baba wa Mbinguni.