2020
Tumaini Letu, Nuru Yetu, Nguvu Yetu
Oktoba 2020


Neno la Mwisho

Tumaini Letu, Nuru Yetu, Nguvu Yetu

Kutoka Jioni ya matangazo na Viongozi Wakuu wenye Mamlaka kwa ajili ya waelimishaji wa dini

Wakati nilipotawazwa kuwa Mtume, mpendwa Rais Thomas S. Monson (1927-2018) alisema kwamba ningekuwa shahidi maalum wa jina la Yesu Kristo ulimwenguni kote. Sikuchukulia jukumu hilo kiwepesi. Nilijisomea kwa makini maandiko, nikimtambua Bwana kwa majina na vyeo vyake. Haya yote ambayo nitashiriki nanyi ni kutoka kwenye vifungu vya maandiko ambavyo vinatukumbusha juu ya tumaini letu lililo ndani Yake.

Yeye ni Tumaini la Israeli (Yeremia 17:13), Nyota Angavu na ya Asubuhi (Ufunuo 22:16), Mchungaji Mwema (Mafundisho na Maagano 50:44), Mshauri (Isaya 9:6; 2 Nefi 19:6), Mfalme wa Amani ( Isaya 9:6; 2 Nefi 19:6), Mkombozi (Warumi 11:26), Nuru ya Ulimwengu (Yohana 8:12), na Kuhani Mkuu wa mambo mema yajayo (Waebrania 9:11). Ana uwezo wa kuokoa (Alma 34:18) Mafundisho na Maagano 133:47) na Yeye aliye na uwezo wote (Mafundisho na Maagano 61:1).

Ushawishi wa Kristo, alama, na kufikia kwake vyote vimetuzunguka. Yeye yuko hapo wakati tunaposita na tunapojitahidi kusonga mbele. Na ikiwa tutateleza, “nuru Yake inayong’aa gizani” (Mafundisho na Maagano 6:21) inang’aa kupita yote. Anatupenda katika masaa yetu ya nuru na ya giza.

Kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo siyo kazi ya kubuni. Njia Yake imewekwa alama nzuri za nyayo Zake Tunapomfuata Yeye, tunakuja kupenda kile akipendacho Yeye. Tunapofanya upya maagano yetu pamoja Naye kila wiki tunapokula sakramenti takatifu, tunakua katika kumwelewa Yeye kama Mkombozi wa ulimwengu (Mafundisho na Maagano 93:9), Roho wa Kweli (Mafundisho na Maagano 93:9), na Neno (Mafundisho na Maagano 93:8).

Wapendwa, huyo ndiye Mwokozi ninayemjua, ambaye ninampenda na ninamstahi kwa moyo wangu wote. Kutoka kina cha nafsi yangu ninatoa ushuhuda juu Yake na juu ya wema na rehema Zake. Ameahidi, “Ninyi ni marafiki zangu, na mtapata urithi pamoja nami” (Mafundisho na Maagano 93:45).

Yesu Kristo daima ni jibu la shida na changamoto ambazo ni sehemu ya uzoefu huu wa maisha katika mwili wenye kufa. Katika kuelewa misheni Yake na injili Yake, upendo wetu Kwake na imani yetu na kumtegemea kwetu Yeye hutupa sisi nguvu.