2020
Peso ya Zaka
Oktoba 2020


Peso ya Zaka

Mwandishi anaishi Chihuahua, México.

Picha
Tithing Pesos

Sofia aliamka mapema. Leo ilikuwa siku maalumu sana. Alikuwa anakwenda kuuza maji ya limao kwenye mauzo ya gereji ya shangazi na mjomba wake. Mama alitengeneza dumu kubwa la maji ya limao kwa ajili yake.

Sofia alitengeneza bango. Aliandika “Maji ya Limao!” kwa maandishi ya rangi ya chungwa na njano. Alibandika kwenye meza ndogo. Halafu yeye akaketi chini kusubiri.

Mara mtu akaja. “Naweza kupata kikombe kimoja?” aliuliza. Aliweka peso kadhaa kwenye dumu lake.

“Hakika!” Sofia alisema. Alimtilia kikombe cha maji ya limao.

Kidogo kidogo watu walikuja kuangalia mauzo ya kwenye gereji. Na kidogo kidogo walinunua maji matamu ya limao. Asubuhi ilipita kwa furaha. Ghafla maji ya limao yote yalikwisha.

Sofia alitikisa dumu lake. Pesos zililia. Alikuwa nazo nyingi!

“Kazi nzuri!” Baba alisema.

Sofia hajawahi kuwa na pesa nyingi kabla. Ninakwenda kununua yo-yo”

Baba alitabasamu. “Je, unajua mama na mimi tunafanya nini tunapopata pesa?”

Sofia alitikisa kichwa chake.

“Tunalipa zaka,” Baba alisema. Baba wa Mbinguni ametupa kila kitu. Anatuomba kwamba tumrudishie Yeye sehemu ndogo. Tunalipa zaka kwa sababu tunampenda Yeye.”

Sofia alitabasamu. Alitaka kumwonyesha Baba wa Mbinguni kwamba anampenda pia.

Baba alimsaidia Sofia kuhesabu peso zake. Kila alipohesabu 10, aliweka moja katika bahasha. Baba alimsaidia kuandika namba kwenye bahasha ndogo nyeupe. Waliiweka karatasi katika bahasha pamoja na zile peso. Kisha wakaifunga. Sofia alikuwa anakwenda kumpa askofu kesho kanisani.

Je, unajisikiaje? Baba alimwuliza Sofia.

“Furaha sana! Na bado ninapesa kwa ajili ya yo-yo.” Alihisi Baba wa Mbinguni alikuwa na furaha kwa uchaguzi wake. ●