2020
Vidokezo 7 vya Kushinda Matumizi ya Ponografia
Oktoba 2020


Vijana Wakubwa

Vidokezo 7 vya Kushinda Matumizi ya Ponografia

Mwandishi anaishi Utah, Marekani.

Katika kufanya kazi na vijana wakubwa waseja kujaribu kushinda utumiaji usioweza kuidhibitika wa ponografia, nimepata baadhi ya vidokezo ambavyo vinaweza pia kusaidia.

Picha
flow chart

Stick figure art kutoka Getty Images

Wakati niliposimikwa kama askofu mpya wa kata ya vijana wakubwa waseja, kulikuwa na safu ya vijana wakubwa waseja nje ya mlango wa ofisi yangu wakisubiri kukutana na mimi. Kisia kile tulichojadili katika mahojiano yale ya kwanza.

Ponografia.

Na kwa miaka mitatu iliyofuata, nikijaribu kuwasaidia vijana wakubwa kushinda tabia isiyodhibitika kilikuwa ni kipengele kikubwa cha wito wangu, hivyo nilijua nilihitaji kujifunza kadiri nilivyoweza. Nilifunga, niliomba, nilienda hekaluni, nikashauriana na viongozi wengine, nilirejelea nyenzo zote zilizopo, nilihudhuria madarasa ya uponaji wa uraibu, na nilijifunza kutoka kwa wale wanaofanya kazi za kutafuta uponaji. Ninataka kushiriki baadhi ya mawazo yaliyojaa-matumaini kuhusu yale niliyojifunza.

1. Jua Kuwa Wewe ni Mtoto wa Wazazi wa Mbinguni Wanaokupenda

Ikiwa unajitahidi kushinda matumizi yasiyo dhibitika ya ponografia, unaweza kuhisi kama unajiondoa kutoka kwa Baba wa Mbinguni kwa sababu unafikiri haustahili kupendwa au kusaidiwa mpaka utatue hili. Hivi ndivyo Shetani anataka—kukutenga na kila mtu ambaye anakupenda na wazo kwamba unaweza kushinda ponografia peke yako na ndipo utakapostahili kupendwa.

Kwa sababu ya asili yako ya uungu, wewe daima unastahili kupokea matumaini, mwongozo wa kiungu, na ufunuo binafsi kutoka kwa Baba wa Mbinguni na ile nguvu ya uponyaji ya Yesu Kristo ili kushinda ponografia.1 Usijiondoe kutoka Kwao au kutoka kwa watu ambao wanakupenda.

2. Ondoa Aibu

Nimejifunza kuwa kuondoa aibu ni muhimu kushinda ponografia. Aibu ni kuhisi kama umevunjika, umeharibiwa, au mtu mbaya. Kuamini maoni haya mabaya kuhusu wewe mwenyewe kunaweza kweli kukufanya unase kwenye mzunguko wa uraibu. Kujisikia majuto kwa kitu ambacho umekifanya ni sehemu ya mchakato wa toba na kunaweza kukusaidia kubadilisha tabia yako. Lakini aibu inakufanya uhisi kama tabia yako yote ni mbaya na kwamba wewe umepita kiasi hustahili msaada kutoka kwa Mwokozi.2

Baba wa Mbinguni anataka wewe uwe na matumaini kamili katika Yesu Kristo na baraka za Upatanisho Wake. Aibu inaangalia nyuma kukushikilia wewe katika mzunguko wa maji ya uongo na kujichukia mwenyewe. Tafadhali kaa mbali na barabara ya aibu.

3. Usiwe Mwepesi wa Kutumia Kibandiko cha “Uraibu”

Watu wengi hujipa majina wenyewe kama wenye “uraibu” wa ponografia. Nakuonya usijichukulie jina hilo isivyo sahihi. Vijana wengi wanaopambana na ponografia kwa kweli hawana uraibu.3 Na kutumia vibaya jina hili kunaweza kuifanya iwe vigumu kukomesha matumizi ya ponografia kwa sababu ya aibu, kupungua kwa matumaini, na kuji-dharau kutokanako na hilo.

4. Tengeneza Mpango Binafsi wa Maandishi wa Kujizuia

Mpango binafsi wa kujizuia ni hati yenye sehemu-tatu ambayo inaweza kukusaidia wewe kushinda ponografia.

Sehemu ya 1: Orodhesha visababishi vyako. Kusababishwa ni hatua ya kwanza katika mzunguko unaokupeleka kwenye kutazama ponografia.

Kuna aina kadhaa za visababishi:

  • Hali: mazingira ambayo hutengeneza kisababishi kwa sababu ya mawazo na tabia za zamani (kama kuwa katika chumba hicho hicho au wakati fulani wa siku)

  • Mfadhaiko/wasiwasi/upweke/matukio ya kiwewe: hisia ngumu au hali zinazokusababisha ugeuke kwenye ponografia kama njia ya kuepuka na kukabiliana na hisia hizi.

  • Picha ya Kutazama: kuona pasipo kukusudia kitu ambacho sio cha kiponografia lakini chenye kusisimua kupitia mitandao ya kijamii, sinema, picha, nk.

Sehemu ya 2 Weka mpango wa jinsi ya kupunguza visababishi.

Kwa mfano, ikiwa una kisababishi cha hali kama kujisikia kukosa usingizi usiku sana, kuzima simu yako dakika 30 kabla ya kulala au kulala bila simu yako chumbani kwako inaweza kusaidia. Ikiwa ponografia ni njia ambayo unapambana na hisia ngumu, tafuta njia za kushughulikia hisia hizi vizuri. Je, mazoezi au dawa inaweza kukusaidia kupunguza mfadhaiko au kiwango cha wasiwasi?. Je, kwenda matembezini na marafiki au kujiandikisha katika darasa la chuo kunaweza kupunguza upweke? Fikiria yale unayosumbuka nayo na ni chaguzi gani zinaweza kukusaidia.

Pia, usidharau nyenzo za kiroho. Maombi, kusoma maandiko, huduma, na mahudhurio ya kanisani na hekaluni ni zana zenye nguvu ambazo ni muhimu katika kupunguza visababishi na kukusaidia kuendelea kuwa imara.

Sehemu ya 3: Panga nini unaweza kufanya wakati umepata msisimko. Kwa kila kisababishi, andika mpango wako wa hatua kadhaa.

Kwa mfano, unapochochewa, unaweza kuzima simu yako haraka, kutuma ujumbe au kupiga simu kwa mtu, nenda matembezini au mazoezini, soma kutoka Kitabu cha Mormoni, au fanya kitu chochote ambacho kinaweza kukusaidia kuelekeza mawazo yako.

Andika hatua ambazo zinafaa kwako! Wakati mwingine visababishi vitapita bila kupitia hatua zako zote za mpango wa kujizuia. Lakini hatua zako zinaweza kusaidia kukuondoa katika wakati huu. Mara baada ya kichocheo kupita, sahihisha mpango wako wa kujizuia kile kilichowezekana na jinsi kinavyoweza kubadilishwa ili kuwa bora zaidi wakati ujao. Weka sehemu ambayo unaweza kuona kila siku.

Picha
flow chart part 2

5. Elewa Kushindwa dhidi ya Kushindwa Tena

Kushindwa ni pale unapoharibu, lakini mara moja unarekebisha na kutumia kama uzoefu wa kujifunza kuboresha mpango wako wa kujizuia. Kushindwa tena ni pale unapokata tamaa, kuzidi, na hujali.

Jua kuwa kushindwa ni sehemu ya kuboresha mpango wako wa kujizuia. Usihitimishe kusema umepoteza maendeleo yako yote au kazi yote ambayo umeifanya haihesabiki—kwa sababu inahesabika. Angalia mbele kwa mtazamo chanya na ujue kuwa wewe uko siku moja karibu kupona.

Wakati unaposhindwa jiulize mwenyewe:

  • Ni nini kilitendeka?

  • Kwa nini kisababishi hiki ni tofauti?

  • Je, umekuwa na mfadhaiko hivi karibuni? Je, ulikuwa ukijisikiaje kihisia?

  • Je, kukaa kwa muda bila kusoma maandiko kumekudhoofisha?

  • Je, hujafanya mazoezi kwa wingi hivi karibuni?

  • Je, kuna kitu katika mpango wako wa kujizuia sio chenye msaada?

  • Je, unaweza kufanya nini tofauti wakati mwingine?

Andika chini kile unachojifunza na endelea!

6. Amini katika Nguvu ya Uponyaji ya Mwokozi

Yesu Kristo anaweza kukusaidia katika mchakato endelevu wa toba, na Yeye ana nguvu za kukuwezesha unapojitahidi kushinda ponografia. Anaelewa jinsi unavyohisi na anasubiri kuchukua mzigo huo kutoka kwako. Usidhani kama kumgeukia Yeye kunamwongezea mzigo. Tayari ameshalipia dhambi zako. Badala yake, fanya bidii, umkaribie Mwokozi, na umwombe akusaidie kupona, kubadilisha tamaa zako, na kukupa nguvu zaidi ya kusonga mbele.

Kama Mzee Ulisses Sores wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alivyofundisha: “tunapoendelea daima kujitahidi kushinda changamoto zetu, Mungu atatubariki kwa vipawa vya imani ya kuponywa na vya kutendeka kwa miujiza. Yeye atafanya kwa ajili yetu kile ambacho hatuna uwezo wa kukifanya wenyewe.”4

7. Usifanye Hivi Peke Yako

Uhusiano na urafiki pia vinaweza kukupa nguvu na kukusaidia kufanikiwa. Unapaswa kuwa na mtu ambaye anaweza kukusaidia kuwajibika na kukuona ukipitia siku zako bora zaidi na mbaya zaidi. Wanapaswa kukusaidia bila kukuhukumu. Nawe unaweza pia kutoa msaada huo huo kwao. Tafuta ushauri kutoka kwa viongozi wako wa Kanisa au wanafamilia. Na ikihitajika, mtaalamu au mshauri wa kitaalam wa afya ya akili pia anaweza kukusaidia kugundua sababu za kwanini unaweza kuwa unasumbuka kutazama ponografia.

Kumbuka Kwamba Ninyi Ni Wazazi na Viongozi wa Kesho

Ninyi ni kizazi cha kwanza kutawala upatikanaji wa ponografia kwa masaa 24 kwa wiki. Naamini changamoto hii inafikia kilele katika kizazi chenu kwa sababu mtakuwa na zana bora na busara za kuwaongoza wengine mbali au nje ya mtego huu wakati ninyi mkiwa wazazi na viongozi siku moja. “Baba wa Mbinguni hajatuweka sisi hapa duniani ili tushindwe bali kwa utukufu tufanikiwe.”5

Ingawa vidokezo hivi vinaweza kusaidia katika juhudi zako za kushinda ponografia, usiogope kugeukia rasilimali zingine pia. Safari ya kila mtu ya kupona inaonekana kuwa tofauti. Tafuta kile kinachokusaidia. Usikate Tamaa. Chukua siku hii moja kwa wakati mmoja. Unaweza kufanya hivi. Hakika unaweza (ona Wafilipi 4:13). Na utakuja kuwa mtu ambaye ulikusudiwa kuwa.

Muhtasari

  1. Dada Joy D. Jones alielezea tofauti kati ya thamani na ustahili katika “Thamani zaidi ya Uzani,” Lihona, Nov. 2017, 14.

  2. Ona Wendy Ulrich, “Sio Dhambi kuwa Dhaifu,” Liahona, Apr. 2015, 23; “Shame versus Guilt: Help for Discerning God’s Voice from Satan’s Lies” (makala ya kidigitali-pekee), Ensign, Jan. 2020.

  3. Ona Dallin H. Oaks, “Kupona kutoka kwenye Mtego wa Ponografia,” Liahona, Oct. 2015, 52. Rais Oaks anaelezea tofauti kati ya viwango tofauti vya kuhusika na ponografia: “(1) mfiduo wa macho, (2) utumiaji wa mara chache, (3) utumiaji mkubwa, na (4) utumiaji usioweza dhibitika (kutawaliwa na mazoea mabaya).” Inasaidia kutambua kuwa sio kila mtu anayetumia ponografia ana “tawaliwa na mazoea mabaya”. Kuna tumaini la kushinda ponografia, bila kujali ni kiwango gani cha kujihusisha ulichonacho.

  4. Ulisses Soares, “Beba Msalaba Wetu,” Liahona, Nov. 2019, 114.

  5. Richard G. Scott, “Learning to Recognize Answers to Prayer,” Ensign, Nov. 1989, 30.