2020
Watu Waaminifu Walimfuata Yesu
Oktoba 2020


Hadithi za Maandiko

Watu Waaminifu Walimfuata Yesu

Soma kuhusu hili katika 3 Nefi 17 hadi 4 Nefi 1.

Picha
Jesus breaking bread

Vielelezo na Apryl Stott

Wakati Yesu alipowatembelea Wanefi na Walamani, Aliwafundisha kuhusu ubatizo na jinsi ya kula sakramenti. Alianzisha Kanisa.

Picha
Jesus blessing children

Yesu alimbariki kila mtoto. Malaika wakaja! Yesu aliwaponya wagonjwa na kuomba kwa ajili yao. Kisha Akarudi mbinguni.

Picha
woman sharing food

Baada ya Yesu kuondoka, watu waliendelea kufanya kile Alichowafundisha. Kila mmoja alifanya kazi pamoja na kushiriki kile walichokuwa nacho, hivyo hakuna aliyekuwa maskini. Viongozi wa Kanisa waliwabariki wale waliokuwa wagonjwa.

Picha
people talking around a fire

Badala ya kugombana, watu walichagua kupatana. Kila mmoja alifuata amri za Mungu. Na walikuwa na furaha kwa muda mrefu!

Picha
children blowing bubbles

Maisha yangu yatakuwa ya furaha zaidi wakati ninapofuata amri za Mungu. Ninaweza kushiriki vile nilivyo navyo pamoja na wengine. Ninaweza kuwasaidia watu kupatana. ●