2020
Halo kutoka Madagacar
Oktoba 2020


Halo kutoka Madagascar!

Picha
Hello from Madagascar

Habari, sisi ni Margo na Paolo.

Tunasafiri kuzunguka ulimwengu kujifunza kuhusu watoto wa Mungu. Jiunge nasi tunapozuru Madagascar!

Madagaska ni kisiwa kilichopo pwani ya mashariki ya Afrika. Kina mimea mingi na wanyama wengi ambao hawapatikani sehemu yo yote duniani—komba wa bukini mwenye mkia wa duara!

Wavulana hawa wanasaidia kubeba majagi ya maji kwa ajili ya familia zao Je, unaisaidiaje familia yako?

Kanisa ni dogo katika Madagaska, lakini linakua! Kwa sasa kuna kata 14 na matawi 26 huko.

Aina zaidi ya vinyonga huishi nchini Madagaska kuliko mahali pengine popote ulimwenguni!

Miti hii mikubwa ya mibuyu inaweza kuhifadhi maji mengi kwenye mashina yake hadi lita 120,000!

Watu wengi nchini Madagaska hula wali mara mbili au tatu kwa siku, wakati mwingine na mboga, maharagwe, au nyama.

Neno “rafiki” Kimalagalasi ni namana Ikiwa ungekutana na rafiki mpya huko Madagaska, ungewaambia nini?

Kutana na baadhi ya marafiki zetu kutoka Madagaska!

Ninajua kwamba Yesu Kristo ni Mwokozi wetu.

Nathan, miaka 7, Jimbo la Antananarivo, Madagaska

Russell M. Nelson ni nabii wa Mungu.

Nomena, miaka 6, Jimbo la Antananarivo, Madagaska

Je, wewe unatokea Madagaska? Tuandikie Tungependa kusikia kutoka kwako.

Asante kwa kutalii Madagascar pamoja nasi. Tutaonana wakati mwingine!