2020
Kwenye Hoja
Oktoba 2020


Kwenye Hoja

Ikiwa niliwahi kuwa na changamoto ya afya ya akili, bado ninaweza kutumikia misheni?

Picha
missionaries walking

Ndiyo. Wale wote “wenye kutamani kumtumikia Mungu … wameitwa kwenye kazi hiyo” (Mafundisho na Maagano 4:3). Kule tunakohudumu sio muhimu kuliko jinsi tunavyohudumu. Na mtu yeyote anayefikiria kutumikia misheni watakuwa afya zao za mwili na akili zimefikiriwa.

Kama una shauku ya kuhudumu misheni, ongea na askofu wako. Anaweza kukusaidia kuanza mchakato wa kuomba. Sehemu ya mchakato huo itajumuisha kushauriana na madaktari na wataalamu wengine, na pia viongozi wa Kanisa na wazazi. Mashauriano haya hayakusudii kutathmini ikiwa wewe ni “mzuri wa kutosha” kwa Bwana lakini ni kusaidia kuamua chaguo bora kwa ajili ya huduma yako.

Wito wa kuhudumu unaweza kuja kwa yeyote mwenye nia ya kuhudumu. Jukumu unalopokea la kutumika katika eneo fulani au kwa njia fulani linaweza kutegemea sababu nyingi. Watu walio na changamoto za kiafya (pamoja na afya ya akili) wakati mwingine wamejaribu kuzuia taarifa hii katika mchakato wa maombi, wakifikiria kwamba itawasaidia kupokea kazi wanayotaka. Lakini ikiwa wewe ni mwaminifu kabisa juu ya historia yako ya matibabu (pamoja na afya ya akili), Bwana atakubariki. Yeye anatarajia ufanye yote uwezayo ili kuboresha afya yako. Na msaada mwingi wa matibabu unaopokea nyumbani unaweza kuendelea katika eneo la misheni.