2020
Huduma ya Kila siku ya Marta
Oktoba 2020


Huduma ya Kila Siku ya Marta

Mama huyu na binti yake wanafanya kazi kwa bidii ili kuishi injili pamoja. Na Marta anaweza kuishi injili kwa kumhudumia mama yake kwa njia za kipekee.

Picha
Marta smiling

Picha na Leslie Nilsson

Marta ni binti wa miaka 11 kutoka Ureno, na kama wasichana wengi wa umri wake, anapenda kutumia muda na marafiki zake, kula chakula, na kucheza na wanasesere wake. Pia anafurahi kutumia muda pamoja na mama yake. Lakini kuishi na mama yake inamaanisha kwamba Marta anaishi tofauti kidogo na watoto wengine

Mama yake Marta, Sonia alizaliwa na upungufu wa misuli mwendo ambayo inafanya iwe vigumu kwake kutembea. Yeye hajapooza kabisa, lakini anahitaji cha kutembelea. Hawezi kuvaa mwenyewe, kuoga mwenyewe, au kupanda kitandani mwenyewe. Hii inakuwa vigumu kwa yeye kuishi peke yake. Marta ameweza kumhudumia Sonia kwa miaka kadhaa iliyopita kwa kumsaidia vitu ambavyo hawezi kufanya yeye mwenyewe.

Picha
Marta with her mother

“Ninaweka mazingira safi ili mama yangu aweze kuzunguka kiurahisi,” anasema Marta. “Pia ninapumzika kucheza ili niwe na muda kumwangalia mama yangu na kuona kama anahitaji msaada. Nikiwa ninacheza na ananiita, nitakwenda haraka kwa sababu linaweza kuwa jambo la haraka.

Lakini Sonia anajaribu kumwacha Marta kuishi maisha ya kawaida kadiri awezavyo. Kama Sonia hahitaji msaada wowote, ana hakikisha kwamba Marta anapata muda wa kucheza na rafiki zake.

Picha
Marta walking with her mother

Kuishi Imani Yao

Marta ana nafasi ya kuishi injili kila siku kwa kumtumikia mama yake. Yeye huchukua majukumu mengi ambayo watoto wengine kwa kawaida hawana. Kwa mfano, huamka mapema kumsaidia mama yake kuwa tayari kwa kazi kabla ya shule. Bila msaada wa Marta, Sonia asingeweza kuzunguka au kwenda kufanya kazi kila siku.

Picha
Marta and mother sitting at a table

Marta na Sonia wanahudhuria kanisani pamoja. Sonia alibatizwa akiwa na miaka nane, hivyo Marta amekulia Kanisani. Sonia anamfundisha Marta kuhusu umuhimu wa injili kila siku. Njia moja wapo ya kufanya hivi ni kuwa na picha nyingi za Yesu Kristo katika nyumba yao.

“Ninajua kwamba Mungu anaishi na kwamba Yesu Kristo kweli yupo,” Sonia anasema. “Na ninataka kila mmoja ajaye nyumbani kwangu ajue kwamba imani ni muhimu sana kwangu. Pia ni muhimu kwangu kuyafundisha haya kwa Marta ili kwamba akue na elimu hii ya Yesu Kristo.”

Marta amechukua ambacho mama yake amemfundisha na anaendelea kujifunza zaidi kuhusu injili yeye mwenyewe. Njia mojawapo anayopenda kujifunza ni kwa kusoma maandiko, ambayo humsaidia kuanzisha uhusiano wenye nguvu na Baba wa Mbinguni na Mwokozi. “Nikiwa nasoma maandiko, ninahisi kwamba Kristo yupo pembeni mwangu,” anasema.

Picha
Marta with her mother

Kutafuta Faraja

Wakati inaweza kuwa vigumu kuwa na majukumu mengi, kwenda kanisani kila juma kunamsaidia Marta kupata faraja anayohitaji ili kuendelea kumsaidia mama yake. “Wakati wanasema sala mwanzoni na mwisho wa mkutano wa sakramenti, ni amani sana” yeye anasema. “Wakati nipo huko, nyakati zingine ninahisi kama Baba wa Mbinguni ananiambia kuwa mimi ni mtu mzuri na kwamba lazima niendelee kuwa mtu mzuri kumsaidia mama yangu.”

Wakati wowote anapohisi hivi, anakumbushwa jinsi gani anashukuru kwa ajili ya mama yake. Anahisi kwamba Baba wa Mbinguni amewaleta malaika ili kumsaidia yeye. “Nadhani kwamba Yeye ananiimarisha mimi ili kuamka na kuwa mwenye furaha na kuona fahari juu ya mama yangu,” Marta anasema.

Moja ya masomo ambayo Sonia na Marta wamejifunza pamoja ni kwamba maisha si rahisi au makamilifu—kwa kila mtu. Sonia anasema, “Hakuna magumu yangu yanayonifanya nisikitike. Ninajua kuwa Mungu alinipa mwili huu na damu na mifupa namna hivi kwa sababu mimi ni maalum, na Mungu aliniambia naweza kuifanya. Ninafanya niwezavyo Ninaweza kufanya zaidi, lakini leo ninajisikia vizuri mimi mwenyewe. Ninajivunia kile ninachofanya, kile nilicho nacho, na kile nitakacho fanya kesho.”

Marta pia anatambua kuwa mambo yataenda sawa, hata ingawa maisha yanaweza kuwa magumu nyakati anapomtunza mama yake. Anaona kuwa kila mmoja ana changamoto tofauti. “Hakuna maisha ya mtu yaliyo kamili,” anasema. Lakini hata na changamoto zake binafsi, Marta bado anapata vitu vizuri katika kila hali—uhusiano alio nao na mama yake ni mfano mmoja. “Mama yangu ana mapungufu wa kimwili, lakini kiakili na Majarida ana akili sana. Hakika sisi ni marafiki wazuri.”

Picha
Marta with her mother

Kutazama Mbele.

Kwa hivyo ni nini kilichoko katika wakati ujao kwa Marta na Sonia? Marta anasema, “Ninataka kuwa karibu na mama yangu, na kwa kweli ninataka kuolewa, kuwa na watoto, na kuwa na familia. Lakini katika siku za usoni, ikiwa naweza, nataka kununua nyumba kwa ajili ya familia yangu na mama yangu kwa sababu nisingetaka kuwa mbali naye hata kwa siku moja!”

Sonia anahisi matumaini juu ya siku za usoni vile vile na daima atashukuru kwa wenza na upendo wa Marta. Inashangaza kuwa na binti mzuri. Ni vizuri sana kuwa na Marta maishani mwangu. Yeye ni zawadi kutoka kwa Mungu. Alimuandaa Marta kukaa hapa pamoja na mimi.”