Misaada ya Kujifunza
Mfano


Mfano

Hadithi fupi iliyotumika kufafanua na kufundisha kweli au kanuni ya Kiroho. Mfano uko katika msingi wa kulinganisha kitu au tukio la kawaida na ukweli, na maana au ujumbe wa mfano unayoonyeshwa bila kutajwa mara kwa mara hufichwa kwa msikilizaji ambaye huwa hayuko tayari kiroho kuupokea (Mt. 13:10–17).

Yesu mara kwa mara alifundisha kwa mifano. Kwa orodha ya mifano yake muhimu, ona Upatanifu wa Injili katika kiambatisho.